Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Usiku ulipoingia nikaanza kuhesabu maumivu, nikalala nikiwaza nifanye nini, nikatamani kumpigia simu Hadija nimuombe radhi, nikatamani kwenda kwa yule mganga aliyenipeleka Gululi nikaombe anisaidie na hata kama atataka nimpe penzi nifanye hivyo. Nikawaza kwenda kwa mchungaji, mawazo yote hayo yalinijaa tele.
Nikaona jambo la kwanza kufanya ni kumpigia simu kwanza Hadija hata kumpigia magoti nifanye tu, maana kanigusa kunako, hata kama atataka hela yoyote mimi nitampa ili mradi tu anipe mume wangu.
Wakati nawaza hayo kuna kitu kikaniambia niangalie kwanza whatsapp namba ya Hadija, nikaona kuna picha moja ameipiga ndani ya Mall akiwa na begi la nguo. Eti status ameandika “mambo ya shopping upoo!” halafu akaweka na viemoji vya ndege inaruka.
Kwa status ile alizidi kunitia hasira nikaghairi kabisa mpango wa kumnyenyekea na kumpigia magoti. Nikanyanyuka kutoka kitandani na kuvaa nguo zangu nikabeba na kisu cha jikoni na kunyata ili dada na mama wasisikie kama naondoka, nilipopita karibu na chumbani kwa mama nilisikia akiangusha maombi.
UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA KUTUMIWA
UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA KUTUMIWA
ITAENDELEA JUMATATU
No comments:
Post a Comment