Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Basi mama aliporudi tu alikuwa na mshumaa wa kijani na pakiti zaidi ya kumi za chumvi ya mawe, nilidhani amechanganyikiwa. Lakini hakuwa hivyo.
“Mwanangu, sijawahi kufanya hivi lakini bibi yangu aliwahi kuniambia inafanya kazi kwa mtu aliyefanyiwa limbwata. Mshumaa wa kijani unaweza kumvuta mtu aliyekuwa mbali lakini ili kumfanya abaki ndani, inabidi chumvi hii ndiyo itumike,” alisema mama.
Kwa kuwa nilikuwa na majonzi yangu, nilimuangalia tu sikumjibu chochote, akawasha ule mshumaa akinitaka nitazame kile kiini cha moto pale karibu na utambi. Halafu nitamke majina ya mume wangu na mwanangu Kendrick.
Nilimuangalia mama “like; really u gonna make me do this voodoo shit ! Maa?” lakini nikaamua kufanya kama alivyosema maana yeye ni mkubwa na ameona mengi duniani.
Basi nikaungalia ule mshumaa pale kwenye ulimi wa moto na kutaja jina la mume wangu, mama aliniambia nifanye vile mara saba, halafu nikamtaja mwanangu mara saba pia. Halafu nikamuona anainuka na dada na kwenda pale mlangoni wakamwaga ile chumvi na kuingia ndani kule nilipolala na Mr X, pale mbele ya kitanda mama akamwaga tena chumvi na kuchora kama mstari hivi mkabala na kitanda changu.
UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA KUTUMIWA
UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA KUTUMIWA
ITAENDELEA IJUMAA
No comments:
Post a Comment