Polisi nchini Ungereza wameonya kuwa
kunauwezekano wa kutotambulika kwa watu waliokufa kwenye moto
uliounguza ghorofa magharibi mwa Jiji la London.
Vikosi vya huduma za dharura
vimeendelea kwa siku tatu, vikiendelea kutafuta miili ya watu
iliyoungua katika ghorofa hilo la makazi ya watu la Grenfell Tower.
Watu 17 wamethibitishwa kufa hadi
sasa, ila idadi yao waloikufa moto inatarajiwa kuongezeka na kunahofu
huenda ikazidi watu 60.
Waombolezaji wakiomboleza kwa kuweka mashada ya maua na kuandika ukutani ujumbe wa maombolezo
No comments:
Post a Comment