HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » DUKA LA KADI ZA KISASA ZA MIALIKO MBALIMBALI YA SHEREHE LAZINDULIWA MWENGE

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Kampuni ya 'R plus event cards', Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya 'R plus event cards', Bi. Rehema Moses na Mkurugenzi Mkuu, Raimond Njuu (kushoto) wakishuhudia.
 Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akimuonyesha kadi mbalimba mgeni maalum wa ufunguzi wa Duka, Doris  Mollel  katika hafla iliyofanyika Mwenge.

Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi. Doris Mollel amezinduwa tawi jipya la duka la kadi la Kampuni ya 'R' Plus Events Cards' Mwenge, Sokoni Jijini Dar es Salaam huku akiwataka wajasiliamali wadogo na wakubwa wauzaji wa bidhaa hizo kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ili wajipatie kipato. Bi. Mollel ametoa kauli hiyo alipokuwa akizinduwa tawi hilo, linalofunguliwa kusogeza huduma za uuzaji kadi za kisasa jumla na rejareja kwa wananchi eneo hilo. 
 Pamoja na hayo, Bi. Doris Mollel aliwashauri wananchi kupenda kununua bidhaa halisi na kuachana na bidhaa feki kwani zimekuwa na madhara huku zikilikoseshea taifa mapato. Alisema bidhaa nyingi feki haziingii kwa utaratibu rasmi nchini hivyo licha ya madhara kwa watumiaji zimekuwa zikilikosesha taifa mapato. 
 "...Nashauri Watanzania wenzangu tupende kununua bidhaa halisi zinazoendana na thamani ya fedha tunazotoa. Uzuri sasa hivi wauzaji wengine wamekuwa wawazi wanakwambia hii ni bei rahisi kwa kuwa ni feki na hii ndio bidhaa halisi...tujenge utamaduni wa kutumia bidhaa bora na halisi kwa manufaa yetu na taifa," alisisitiza Bi. Doris Mollel.
 Aidha aliipongeza kampuni ya Plus Events Cards wauzaji wa kadi na maua ya maharusi kwa kusogeza huduma zake eneo la Mwenge na kutoa fursa kwa wajasiriamali kuwatembelea kwa ajili ya kusambaza bidhaa hizo Dar es Salaam na hata mikoani. Aliongeza kuwa hatua hiyo si tu imesogeza huduma kwa wahitaji bali imetoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata bidhaa za kadi kirahisi na kuzisambaza kwa wahitaji Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya R Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses ameiomba Serikali kujenga mazingira ya ulipaji kodi na malipo anuai ya vibali vya biashara kufanyika eneo moja ili kupunguza urasimu ambao wamekuwa wakiupata wafanyabiashara wanapoitaji kulipia tozo hizo.
 Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa kauli hiyo kwenye uzinduzi wa tawi jipya la uuzaji kadi jumla na rejareja kwa ajili ya matukio mbalimbali ya sherehe eneo la Mwenge, Sokoni jijini Dar es Salaam. Bi. Moses alisema wapo wafanyabiashara waadilifu ambao wanajua umuhimu wa kulipia tozo mbalimbali na vibali vya biashara wanazozifanya lakini baadhi wamekuwa wakikwazwa na urasimu uliopo katika ufuatiliaji wa vibali hivyo na mtawanyiko wa ofisi anuai za kufanyia malipo, jambo ambalo linachangia kujikuta wanashindwa kulipia kwa wakati. 
 Mfanyabiashara huyo mwanamama na Mtanzania wa kwanza kusambaza bidhaa hizo za kisasa aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa vibali vyote na malipo kuwa yakifanyika eneo moja ili kumrahisishia mfanyabiashara kukamilisha vibali husika kwa wakati, na kumpunguzia mfanyabiashara vikwazo ambavyo wakati mwingine vimekuwa vikimpotezea muda mwingi katika ufuatiliaji. Aidha alivishauri vyombo vya kudhibiti ubora wa bidhaa kuongeza nguvu ili kudhibiti baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakichapisha kadi feki nchini na kuwalaghai watanzania kuwa ni halisi, jamboa ambalo linawaharibia wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa halisi.

 Alisema kampuni yake ambayo imekuwa ikisambaza kadi za kisasa za matukio mbalimbali ya sherehe jumla na rejareja kutoka nchini China ipo tayari kuwasaidia wajasiliamali waaminifu kutoka popote nchini kufanya biashara hiyo bila udanganyifu ili kumpatia mlaji wa mwisho bidhaa halisi kwa bei nzuri.
 Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akiwa na Mwenza wake wakikata keki mara baada ya duka hilo kufunguliwa.
 Hapa ikikatwa keki ya pongezi na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards.
 Mgeni Maalum, Doris Mollel akiwa na Mmiliki wa Duka, Rehema Moses na wadau mbalimbali waiofika katika duka  hilo.
Picha ya pamoja ya wageni waalikwa baada ya uzinduzi

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: