Na Christina
Mwangosi, MOHA
Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Magereza nchini Dk. Juma Malewa amesema Jeshi la Magereza nchini litatoa
elimu ya namna kila Mtanzania hata aishie kwenye nyumba za ghorofa ama maeneo
yenye nafasi ndogo ya kuanzisha kilimo cha mbogamboga, anavyoweza kutumia eneo
dogo kuendeshea shughuli za kilimo cha mbogamboga wakati huu Maonyesho ya
SabaSaba yanayoendelea katika Viwanja vya SabaSaba jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali Dk. Malewa
amesema kuwa pamoja na kuandaa Shamba Darasa kwa ajili ya kutoa elimu ya shughuli
mbalimbali za kilimo, Jeshi la Magereza
limeandaa bidhaa mbalimbali ambazo zitaonyeshwa wakati wote wa Maonyesho
pamoja na kuuzwa wakati wote wa Maonyesho hayo.
Dk. Malewa amesema miongoni
mwa bidhaa hizo ambazo ziko kwenye Banda la Magereza ni samani mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi na
nyumbani ikiwemo makabati ya vyombo na nguo,
meza na viti, madawati kwa ajili
ya shule za msingi na sekondari,
vitanda, sofa, ‘dressing table’ pamoja
na viatu vya ngozi vya kike na kiume.
Amesema Jeshi la Magereza
pia litauza pia majiko sanifu
yanayotumia kuni kidogo, mashuka, foronya, vikoi pamoja na sabuni zenye
ubora kwa ajili ya kufua nguo ambazo zinatengenezwa katika Kiwanda cha Sabuni
kilichopo Mkoa wa Mbeya.
Amesema Jeshi la Magereza
katika kipindi hiki cha Maonyesho litatoa elimu ya shughuli za kilimo cha
kisasa bure na kwa wale wananchi ambao maeneo yao yanafikika Wataalamu wa Magereza
wanaweza kuwatembelea wananchi kwenye maeneo yao na kuwafundisha namna ya
kuanzisha kilimo hicho kinachojulikana kama ‘kilimo cha jikoni’.
No comments:
Post a Comment