Ghorofa lenye urefu wa futi 1,100
nchini Dubai limeungua moto upande mmoja leo afajiri katika tukio
ambalo hata hivyo wakazi wake wote wametoka salama.
Moto huo ulisambaa kwa kasi katika
ghorofa hilo la makazi ya watu lililorefu zaidi kuliko yote duniani
na kusababisha mtafaruku kwa wakazi wake huku kukiwa na joto la 45c.
Picha za video zinaonyesha jinsi
moto huo ulivyokuwa unapanda juu katika ghorofa hilo lenye ghorofa
86, huku sehemu ya moto ukiangukia gari zilizoegesha chini.
Ghorofa refu la makazi Dubai likiwa linawaka moto leo alfajiri
No comments:
Post a Comment