Watu wawili mkoani Singida wameuwawa katika matukio mawili tofauti likiwemo la jambazi kuuwawa na polisi wakati wakirushiana risasi , na tukio lingine mtu mmoja kusukumwa na kuangukia nje katika basi dogo lililokuwa katika mwendo wakasi.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida Mrakibu mwandamizi wa polisi Stella Mutabihirwa ,amesema jambazi aliye tambulika kwa jina la Salumu Issa amekufa wakati akipelekwa hospitali baada ya kupigwa risasi na askari ambaye yeye pia askari ilimpiga kwanza risasi na jambazi wakati alipokuwa akitaka kutoroka.
Katika tukio la pili kamanda Mutabihirwa amesema jeshi la polisi lina mshikilia Shabani Mnghwira utingo wa basi dogo aina ya hice lenye usajili wa namba T.544 DFS, lililo kuwa likitokea Singida kwenda Igunga mkoani Tabora kumpiga kibao abiria moja mvulana kisha kumsukumia nje na kuangukia kisogo kwenye barabara ya lami na kupoteza maisha kwa madai ya kufunga mlango wa gari kwa nguvu.
Tukio la jambazi kuuwawa limetokea katika kijiji cha Mukulu kata ya Mughunga wilayani Singida na askari kufanikiwa kukamata bastola iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na risasi ishirini na sita,tukio lingine la utingo kumsumkuma abiria kutoka kwenye gari ambalo likiwa katika mwendo hadi nje ya barabara kisha kupoteza maisha limetokea katika kijiji cha Mseko kata ya Sheluhi wilayani Iramba.
No comments:
Post a Comment