HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » Katibu Mkuu CHADEMA aripoti Polisi

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ameamua kwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini hapa.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene imesema Dk Mashinji ameambatana na wasaidizi wake kutoka makao makuu ya chama hicho.
“Katibu mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)” amesema.
Awali, leo Jumatatu Dk Mashinji alisema hawezi kwenda kuripoti kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.
Kamanda Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

“Nina taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’. Ni wakati wowote naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo, wakinihitaji watakuja kuniambia,” amesema Dk Mashinji akizungumza na Mwananchi leo. 
Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma. 
Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.


Chanzo: Mwananchi

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: