MKUU wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Bi Assumpter Mshama ametoa amri ya kufungia machinjio mapya yaliyopo Mtaa wa Mtakuja Pangani Kibaha Mkoani Pwani kwa muda usiofahamika kutokana na kukithiri kwa uchafu unaotishia afya za walaji wa eneo la Kibaha na Vitongoji vyake
Bi Assumpter ametoa amri hiyo muda mfupi uliopita baada ya kufanya ziara ya kushtukiza machinjioni hapo.
Aidha Bwana Afya Ramadhan Mohammed ambaye husimamia shughuli za machinjio hayo amekiri kuwa machinjio hayo yanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa hi pamoja na ukosefu wa maji na umeme.
No comments:
Post a Comment