Polisi Mkoani Mtwara imeanza uchunguzi wa kifo cha mtoto Said
Nassoro mwenye umri wa miaka 11, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Chuno katika Manispaa ya Mtwara/Mikindani aliyejinyonga kwa kutumia mtandio.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara, Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio la kujinyonga mtoto huyo.
Kamanda Mkondya amewataka wazazi kufuatilia na kusikiliza matatizo ya watoto wao badala ya kuwa wakali muda wote.
Akizungumza na ITV kuhusu tukio hilo, mjomba wa marehemu, Bwana. Muwanya
Abdalah amesema mtoto huyo amejinyonga usiku baada ya kurudi kuangalia video, na wao kumgundua asubuhi chumbani kwake akiwa ameshajinyonga.
Amedai hilo ni jaribio la pili kwa mtoto Said
Nassoro kutaka kujinyonga, kwa kuamini akijinyonga ataweza kuzuka tena kama picha za video zinavyoonesha, hata hivyo jaribio la kwanza hakuweza kufaulu, baada ya bibi yake aliyekuwa akiishinaye, kumwokoa kwa kukata kamba aliyojitundika.
No comments:
Post a Comment