MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jumuiya Tatu za Zigi Juu,Zigi Chini na Kuhuhwi zilizopo kwenye Bonde la Mto Pangani katika eneo Amani wilayani Muheza na mradi wa maji mserereko kwa ajili ya vijiji vya Mashewa,Kimbo na Shembekeza
MKUU wa wilaya ya Muheza,Mhandisi
Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
MKUU wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua
Mgeyekwa akizungumza katika uzinduzi huo
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza akizungumza katika uzinduzi huo Jumanne Omari
Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP ambao wamefadhili mradi huo akizuungumza katika uzinduzi huo |
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza akizungumza katika uzinduzi huo Jumanne Omari
Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi
kushoto akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa
wa Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni
vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo
serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi kushoto
akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni
vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo
serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na uchimbaji haramu
wa madini katika eneo la Hifadhi ya Amani wilayani Muheza
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martini Shigella akitembelea maeneo hayo kujionea athari ambazo
zimetokana na uchimbaji haramu wa madini kwenye eneo la vyanzo vya Maji
Amani na Hifadhi ya Msitu
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martini Shigella akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jumuiya ya
watumiaji wa Maji na Mradi wa Maji Mserereko kwa vijiji vya
Masheww,Kimbo na Shembekeza wilayani Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi
Zena Saidi
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martini Shigella katikati akizundua mradi huo kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo anayeshuhudia mwenye kilembe
cheusi kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Mhandisi Zena
Saidi
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martini Shigella kushoto akimtwisha ndoo mkazi wa eneo hilo
kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa kwanza kulia ni
Kaimu
Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga,Mhandisi Laurian Rwebembeza kushoto
ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martini Shigella kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya
Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Tanga,Mhandisi Zena Said
Sehemu za wananchi wakishuhudia uzinduzi huo |
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ameitaka wizara ya
Madini kuacha kuendelea kutoa leseni za uchimbaji wa madini eneo hifadhi ya
Amani wilayani Muheza huku wakitaka zilizotolewa kufutwa kutokana na uharibifu
wa mazingira unaoendelea kwenye eneo hilo.
Kwani uchimbaji huo umekuwa na madhara makubwa kuharibu
mazingira kutokana na kutumia kemikali
ambazo huingia kwenye maji na hivyo kuleta adhari kubwa kwa binadamu
ambayo huyatumia kwa matumizi mbalimbali.
Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Jumuiya za
watumiaji maji Bonde Dogo la Mto Zigi katika Uzinduzi wa Jumuiya tatu za Zigi
Juu,Zigi Chini na Kihuhwi zilizopo Bonde la Pangani.
Mradi huo wa Maji wa Mserereko ulihusisha vijiji vya
Mashewa,Kimbo na Shembekeza wilayani Muheza Mkoani
Tanga.
Alisema pia licha ya kupiga marufuku hiyo lakini
watahakikisha wanawachukulia hatua watumishi watakaoshirikiana na wachimbaji
kwa kuwakamata na kuwapeleka kwenye vyombo vya dola ili kuweza kukomesha tatizo
hilo.
“Labda nisema tu sisi kama mkoa tumepiga marufuku
uchimbaji wa madini katika eneo hili la Amani lakini pia tunaitaka Wizara ya
Nishati wasiendelea kutoa leseni za madinina mtu atakayekwenda kuchukua leseni
hela yake itakuwa
imeibiwa”Alisema
“Lakini pia niseme pia kwa wale ambao leseni wamepewa
zifutwe kwani kuendeleza uchimbaji huo kunaweza kusababisha madhara makubwa
sana kwa uharibifu wa mazingira “Alisema.
Alisema iwapo uharibifu huo utaendelea utasababisha hata
upatikanaji wa maji kutokuwa mzuri hasa ukizingatia uwepo wa mahitaji
muhimu ya maji
kuongezeka kutokana na mradi
wa bomba la mafuta watu watashindwa kupata maji.
“Natambua kuwepo kwa wawakilishi kutoka shirika la
maendeleo la Umoja wa Mataifa la (UNDP) na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF)
ambao wanafadhili mradi wa usimamizi wa pamoja na rasilimali za maji kupitia
usimamizi endelevu wa matumizi bora ya ardhi katika mabonde madogo ya mito Ruvu
na Zigi”Alisema.
Alisema changamoto za kupungua kwa maji unazidi
kuongezeka na kuathiri shughuli za kiuchumi ikiwemo za kijamii hususani za
uzalishaji wa chakula,viwanda,umeme na kulinda
bayoanuai.
“Upungufu huu huchangia na sababu mbalimbali zikiwemo
mabadiliko ya tabia ya nchi na shughuli za kibinadamu zinazoongezeka siku hadi
siku hasa za uchimbaji wa madini,ukataji ovyo wa misitu
“Alisema
Naye Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi alisema utalii
ikolojia umekuwa ukikua kila ambapo kwa mwaka 2007 /2008 watalii walishuka na
kufikia 320 na kupanda mpaka mwaka jana 685 ambo ni watalii ambao wana mchango
mkubwa kuileta mapato nchi.
Alisema pia kuanzishwa kwa miradi inayo saidia kuzua kasi
ya uharibu wa mazingira kwa wananchi kuboresha kipato chao imesaidia kupunguza
kwa asilimia kubwa uharibifu wa mazingira.
“Miradi ya ufungaji vipepeo, kilimo cha uyoga ambacho
wanashirikiana
na Unesco muhoga,karafuu,iliki ufugaji swa samaki,nyuki kwa wadau hao umesaidia
kwa asilimia kubwa wananchi waweze kupata kipato
“Alisema.
Kwa upande wake,Kaimu Afisa
Madini Mkazi Mkoa wa Tanga,Mhandisi Laurian Rwebembeza amesema hakuna
leseni yoyote itakayotolewa kwa wachimbaji wa madini eneo la Amani
wilayani Muheza kutokana na maeneo yao kutengwa kwa
ajili ya uhifadhi.
Licha ya hivyo lakini pia wamefuta leseni 14 za wachimbaji wa madini ikiwemo kutoa tahadhari kwa watakaoendelea na zoezi hili kuacha mara moja kabla hawajakumbana na
mkono wa kisheria.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
ajili ya uhifadhi.
Licha ya hivyo lakini pia wamefuta leseni 14 za wachimbaji wa madini ikiwemo kutoa tahadhari kwa watakaoendelea na zoezi hili kuacha mara moja kabla hawajakumbana na
mkono wa kisheria.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment