Mwakilishi UWT vijana Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya akikabidhi msaada kwa Capten wa timu ya Kigoma Sisters, Sophia Mwasikili kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma.
Mwakilishi UWT vijana Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya pamoja na Kaimu Katibu wa Vijana moa wa Kigoma, Adam .M. Kagoma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wanawake wa Mkoa ya Kigoma Sisters
Na Ripota Wetu, Kigoma
WADAU mbalimbali wa maendeleo na soka wameombwa kuiunga
mkono timu ya Wanawake wa Mkoa ya Kigoma Sisters ili waweze
kuendelea kufanya vema kwenye michuano mbalimbali
wanayoshiriki.
Ombi hilo limetolewa leo na moja ya viongozi wa UWT Mkoa wa
Kigoma Miriam Ntakisivya pamoja na Kaimu Katibu wa Vijana
mkoa huo Adam Kagoma baada ya wao kukabidhi chakula kwa
Nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili.
Lengo la chakula hicho ni kuwapa nguvu kwa lengo kuwapa
hamasa ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi za ndani na zile
watakazocheza nje ya Mkoa Kigoma.
Akizungumza baada ya kukabidhi chakula hicho Ntakisivya
amesema ni vema wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakaendelea
kuichangia timu hiyo kwani inafanya vizuri na ana uhakika
ikisaidiwa itafika mbalimbali kisoka.
"Nitoe ombi watu waendelee kuipambania timu yetu ya Mkoa
ambayo kwa sasa inafanya vizuri.Pia nimpongeze Miss Ubungo
mwaka 2014 Diana Kato kwa kuguswa na kuchangia kile
alichokuwa nacho,"amesema.
Amesema watu watakapoisaidia timu hiyo mbali ya kuwafanya
wachezaji na viongozi kuandaa mazingira mazuri ya kimchezo pia
itatoa nafasi ya timu hiyo kutatua changamoto ambazo
wanakabiliana nazo ambazo nyingine zinatokana na kutokuwa na
vyanzo vya kutosha kumaliza yale ambayo wanakabiliana nayo.
No comments:
Post a Comment