Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, imewaona washitakiwa sita kati ya saba katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Erasto Msuya kuwa wana kesi ya kujibu.
Mshitakiwa wa nne, Jalila Zuber ameachiwa huru baada ya uamuzi wa Jaji Salma Maghimbi, kueleza kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashitaka haukumgusa kiasi cha kufanya awe na kesi ya kujibu. Jaji Maghimbi ametoa uamuzi huo leo Mei 14.
Washitakiwa ambao wameonekana wana kesi ya kujibu ni mshitakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed, mshitakiwa wa pili, Shaibu Jumanne, mshitakiwa wa tatu, Mussa Mangu, mshitakiwa wa tano, Karim Kihundwa, mshitakiwa wa sita, Sadick Jabir na mshitakiwa wa saba, Ally Majeshi.
No comments:
Post a Comment