Kwa mujibu Citizen Kenya imeripoti leo Juni 8, 2018 na mashahidi katika eneo hilo, wamedai kwamba tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Alhamisi, Juni 7, 2018 na ilipofika saa 2:00 usiku waliamua kuvunja mlango wa nyumba ambao ulikuwa umefungwa kwa siku nzima ya jana jambo ambalo halikuwa la kawaida.
Mwili wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Elizabeth Ojwang, ulikutwa umeviringishwa mfuko wa plastiki shingoni, kando na mwili wa mtoto wake uliokutwa na majeraha mbalimbali katika mwili yaliyosababishwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
Akithibitisha tukio hilo kamanda Jeshi la Polisi, kaunti ya Muhoroni, John Kamau amesema kwamba Jeshi hilo linaendelea kumtafuta binti wa kazi kwa mahojiano ambaye alitoweka baada tukio hilo na kuongeza kuwa msichana huyo anaweza kuwa mtuhumiwa wa kwanza wa mauji hayo.
Sababu kubwa ya mauaji hayo bado haijajulikana, Jeshi la Polisi ilichukua miili ya marehemu hao na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Kisumu kwa uchunguzi zaidi
No comments:
Post a Comment