Mkuu wa Jeshi la Anga la Namibia Air Vice Marshal Teofilus Shaende na ujumbe wake wametembelea Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC).
Katika ziara hiyo Air Vice Marshal Shaende amepata fursa ya kufahamishwa kuhusu mafunzo yanayotolewa, mafanikio yake kitaifa na Kimataifa na mkakati wa sasa wa serikali wa kuboresha chuo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Aristid Kanje akitoa maelezo kuhusu Chuo hicho kwa Mkuu wa Jeshi la Anga la Namibia Air Vice Marshal Teofilus Shaende na ujumbe wake waliotembelea Chuo hicho.
Mkuu wa Jeshi la Anga la Namibia Air Vice Marshal Teofilus Shaende akizungumza mara baada ya kupewa taarifa za Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC)
Baadhi ya maafisa wa Jeshi la Namibia na Tanzania wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Aristid Kanje
Mkuu wa Jeshi la Anga la Namibia Air Vice Marshal Teofilus Shaende (wa tatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Aristid Kanje (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wake wametembelea Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC).
No comments:
Post a Comment