Mhe.
Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo ameendelea na ziara yake ya kikazi
na kukagua mradi wa ukarabati wa skimu ya umwagiliaji ya Usense, mkoani
Katavi tarehe 20 Julai 2024 na kuongea na wanakijiji wanufaika wa mradi
huo.
Mradi
wa Usense upo katika eneo la ukubwa wa hekta 106 ambapo Waziri Bashe
amewaambia wanakijiji malengo ya Serikali ni kuboresha na kuongeza
huduma mbalimbali kwa ustawi wa jamii zao.
Amewaeleza
malengo hayo ni kuanza ujenzi wa awamu mbili wa kuvuta mkondo wa maji
kupitia ujenzi wa mfereji wa maji; na baadae bwawa la maji ili
kurahisisha shughuli za umwagiliaji wa kilimo.
Katika
kufanikisha awamu hizo mbili, Waziri Bashe amemwelekeza Bw. Raymond
Mndolwa, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
kutengeneza daraja la kivuko ambalo litawezesha wakulima kuwa na umbali
wa kilomita 1.8 kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji badala ya
kutembea umbali wa kilomita 7 ambazo wamekuwa wakitembea hadi sasa.
Waziri
Bashe ameomba wanakijiji hao wasiuze ardhi ili miradi hiyo iwe na
manufaa makubwa kwa familia zao na vizazi vijavyo. Aidha, Waziri Bashe
anaendelea na ziara yake mkoani Kigoma tarehe 21 Julai 2024 ambapo
atakagua mradi wa umwagiliaji wa Lueche mkoani humo.
No comments:
Post a Comment