Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendesha warsha kwa njia ya mtandao kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ili kuwaongezea ujuzi.
Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema lengo la warsha hiyo ni kuwakumbusha majukumu yao ili kuendana na mitaala ya Bodi ambapo mwaka huu watahiniwa wanaanza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa kutumia mitaala mipya.
Maneno amesema kwa Wakufunzi wa Vituo hivyo kwamba, kwa mwaka huu ambapo mitaala mipya imeanza kutumika wametakiwa kujadili vyema ili wanapokwenda kutoa elimu wawe na uelewa mzuri ili watahiniwa kufanya vyema kwenye masomo yao.
Vilevile amewaasa wakufunzi wa vituo hivyo vya kufundishia masomo ya Bodi kuendesha masomo kwa njia ya mtandao ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji, kuwafikia wanafunzi wengi na kuendana na teknolojia.Mthibiti Ubora Mwandamizi kutoka NACTVET Bonaventure Ackles akitoa mada kwa wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi kuhusu namna nzuri ya kufundisha watahiniwa kwenye masomo mbalimbali.Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CPA Dkt. Emmanuel Christopher akitoa elimu kuhusu njia bora ya kusimamia vituo vya kufundishia kwa Wakufunzi wa Vituo waliokuwa wanafuatilia kwa njia ya mtandao.
Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Indiael Kaaya akitoa maelezo kuhusu namna ya kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufaulu watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ili kuweza kuongeza ufanisi kwenye taaluma ya Uhasibu.
Mtaalamu wa Sarafu Mtandao, CPA Sandra Chogo akitoa elimu kuhusu sarafu mtandao kwa Wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi waliokua wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao.
Afisa Idara ya Elimu na Mafunzo (NBAA), Salimu Kasumari akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na Wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo akitoa mrejesho kuhusu namna mitihani ya Bodi ya mwezi Novemba itakavyofanywa baada ya maboresho ya mitaala mipya wa masomo ya mitihani hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza kwa njia ya mtandao na wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wakati wa kufunga warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment