Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi. Flora Alphonce akisikiliza maelezo kutoka kwa Kelvin Simon kutoka Kampuni ya Swissport Tanzania awakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi. Flora Alphonce akimkabidhi zawadi Kelvin Simon kutoka Kampuni ya Swissport Tanzania wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja.
Afisa Mtoa Taarifa Mwandamizi wa Usafiri wa Anga Babuu Kipira (kushoto) pamoja na Afisa Habari na Uhusiano Mwandamizi wa TCAA Zuhura Lwamo wakimsikiliza Kapteni Mackiyu Kanjwangya, rubanikutoka Shirika la Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) alipokuwa anatoa mrejesho kuhusu huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Afisa Mtoa Taarifa Mwandamizi wa Usafiri wa Anga Babuu Kipira akimkabidhi zawadi Kapteni Mackiyu Kanjwangya, rubani kutoka Shirika la Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi Flora Alphonce akimkabidhi zawadi Afisa uratibu wa Safari za ndege kutoka Equity Aviation Frank Lymo mara baada ya kupata huduma kwenye ofisi ya utoaji wa taarifa za usafiri na Usalama wa Anga zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi Flora Alphonce akimkabidhi zawadi Afisa uratibu wa Safari za ndege kutoka Equity Aviation Mohamed Amani mara baada ya kupata huduma kwenye ofisi ya utoaji wa taarifa za usafiri na Usalama wa Anga zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi. Flora Alphonce akimkabidhi zawadi Mfanyakazi wa Kampuni ya ndege ya Auric Jackline Kishiwa wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi Flora Alphonce akimkabidhi zawadi Afisa Mwandamizi wa uratibu wa Safari za ndege kutoka Shirika la Ndege la Coastal Yahya Rwanda mara baada ya kupata huduma kwenye ofisi ya utoaji wa taarifa za usafiri na Usalama wa Anga zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi Flora Alphonce akimkabidhi zawadi Kapteni kutoka rubani kutoka Shirika la Ndege la Coastal, Desmond Mugisha mara baada ya kupata huduma kwenye ofisi ya utoaji wa taarifa za usafiri na Usalama wa Anga zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mhandisi. Flora Alphonce akizungumza na mteja mara baada ya kusikiliza maelezo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja.
Menejimenti ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani kupitia ofisi yake ya utoaji wa taarifa za usafiri wa Anga iliyopo kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) imekutana na Marubani pamoja na Maofisa wa utoaji wa taarifa za usafiri na Usalama wa anga.
Akiongoza zoezi hilo lililoratibiwa na Kitengo cha Uhusiano cha TCAA, Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Uongozaji ndege Flora Alphonce aliwakumbusha wateja kuwa, TCAA ipo katika wiki ya huduma kwa wateja na Mamlaka ipo tayari kupokea mrejesho hasi na chanya kutoka kwa wateja wake inayowahudumia kupitia ofisi hiyo.
Akitoa maoni yake Rubani Mackiyu Kajwangya kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ameipongeza TCAA kwa kazi nzuri. Rubani huyo mwenye uzoefu wa takriban miaka 20 alisema hajaona tatizo kutokana na huduma za Mamlaka.
Kwa upande wake Mohamed Amani Afisa wa kuratibu safari za ndege kutoka Shirika la ndege la AURIC, alisema huduma za Mamlaka ni nzuri na vibali vinatoka kwa wakati hata usiku wa manane akipiga simu moja tu anapata huduma, pia amepongeza maboresho ya mifumo(portal system)kwani imeboresha huduma zaidi.
Katika wiki hiyo kampuni kadhaa ikiwemo TANAPA, AURIC, Coastal na wengine zilihudumiwa. Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo ni ‘Above and Beyond’ ikilenga zaidi utoaji wa bora za juu ya kiwango za zaidi.
No comments:
Post a Comment