Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika kikao chake Maalam cha Pili kilichofanyika tarehe 19 Disemba, 2024 chini ya Mwenyekiti wake CPA. Prof. Sylvia S. Temu imeidhinisha matokeo ya mitihani ya 100 ya Bodi kwa Watahiniwa waliofanya mitihani hiyo iliyofanyika mwezi Novemba 2024 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi hiyo ya NBAA.
Akitoa taarifa Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) , CPA. Pius A. Maneno amesema kuwa matokeo hayo yameidhinishwa kufuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 12 vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani.
Amesema Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 7,566 kati ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mitihani watahiniwa 658 sawa na asilimia 8.7 hawakuweza kufaya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali hivyo idadi ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo walikuwa 6,908 sawa na asilimia 91.3, kati ya hao watahiniwa 3,764 sawa na asilimia 49.7 walikuwa Wanawake na watahiniwa 3,802 sawa na asilimia 50.3 walikuwa Wanaume.
CPA. Maneno amesema jumla ya watahiniwa 299 wamefaulu mitihani ya Shahada ya Juu ya Uhasibu nchini yaani CPA (T). Kati ya watahiniwa hao wanawake ni 161 sawa na asilimia 53.8 na Wanaume ni 138 sawa na asilimia 46.2. Idadi hii inafanya jumla ya watahiniwa waliofaulu mitahani ya CPA kufikia 13,879 tangu mitihani hiyo ianze mwaka 1975.
Kati ya watahiniwa 299 waliofuzu kutunukiwa Cheti cha Taaluma ya juu ya Uhasibu wengi wao wametoka katika vyuo mbalimbali ambapo watahiniwa 85
sawa na asilimia 28.4 wametoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), watahiniwa 61 sawa na asilimia 20.4 wametoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), watahiniwa 30 sawa na asilimia 10.0 wametoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, watahiniwa 22 sawa na asilimia 7.4 wametoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na watahiniwa 17 sawa a asilimia 5.7 wametoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
Amesema jumla ya watahiniwa 15 wamefaulu mitihani ya CPA(T) linganifu (Equivalent Qualification) kati ya hao wanawake ni 08 sawa na asilimia 53.3 na wanaume ni 07 sawa na asilimia 46.7 ambapo mpaka sasa jumla ya watahiniwa waliofaulu mitihani hii wamefikia 328 tangu mitihani hii ianze Novemba 2014.
Pia amesema katika ngazi ya awali ya Uandishi na Utunzaji wa Hesabu(ATEC I) watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 110 kati ya hao watahiniwa 09 sawa na asilimia 8.2 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 101 sawa na asilimia 91.8.
Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 101 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 82 ambao ni asilimia 81.2 wamefaulu mitihani yao na kati ya hao watahiniwa 44 sawa na asilimia 43.6 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu na watahiniwa 38 sawa na silimia 37.6 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiniwa 19 sawa na asilimia 18.8 hawakufaulu mitihani yao.
Aidha amesema katika hatua ya pili ya Cheti yaani ngazi ya uandishi na Utunzaji wa Hesabu (ATEC II) waliojisaliwa walikuwa 171 kati ya hao watahiniwa 16 sawa na asilimia 9.4 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 155 sawa na asilimia 90.6.
“Kati ya watahiniwa 155 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 100 ambao ni asilimia 64.5 wamefaulu mitihani yao ambapo kati ya hao watahiniwa 40 sawa na asilimia 25.8 wanastahili kutunukiwa Barua za Ufaulu na watahiniwa 60 sawa na asilimia 38.7 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii na watahiniwa 55 sawa na asilimia 35.5 hawakufaulu mitihani yao” Alisema Maneno
Amesema katika ngazi ya taaluma hatua ya awali watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 1,069 kati ya hao watahiniwa 108 sawa na asilimia 10.1 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 961 sawa na asilimia 89.9.
Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 961 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 748 ambao ni asilimia 77.8 wamefaulu mitihani yao ambapo kati yao watahiniwa 286 sawa na silimia 29.8 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu wa mitihani na watahiniwa 462 sawa na asilimia 48.1 wamefaulu baadhi ya masomo hivyo watahiniwa 213 sawa na asilimia 22.2 hawakufaulu mitihani yao.
Aidha amesema katika hatua ya kati waliojisaliwa walikuwa 4,013 kati ya hao watahiniwa 363 sawa na asilimia 9.0 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 3,650 sawa na asilimia 91.0, kati ya watahiniwa hao 3,650 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 2,696 sawa na asilimia 73.9 wamefaulu mitihani yao kati ya hao watahiniwa 593 sawa na asilimia 16.2 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu na watahiniwa 2,103 sawa na asilimia 57.6 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiniwa 954 sawa na asilimia 26.1 hawakufaulu mitihani yao
Katika hatua ya mwisho, waliosajiliwa walikuwa 2,203 kati ya hao watahiniwa 162 sawa na asilimia 7.4 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 2,041 sawa na asilimia 92.6.
Kati ya watahiniwa 2,041 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 1,232 sawa na asilimia 60.4 wamefaulu mitihani mitihani yao ambapo kati ya watahiniwa 319 sawa na silimia 15.6 wanastahili kutunukiwa barua za ufaulu na watahiniwa 913 sawa na asilimia 44.7 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiiwa 809 sawa na asilimia 39.6 hawakufaulu mitihani yao.
CPA. Pius Maneno amesema Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA inatoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.
Pia matokeo ya mitihani ya 100 ya Bodi yanapatikana kwenye tovuti ya NBAA ambayo ni www.nbaa.go.tz.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) , CPA. Pius A. Maneno
No comments:
Post a Comment