HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » TCAA YASHIKA NAFASI YA PILI KATIKA TUZO ZA NBAA ZA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA 2025


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeshika nafasi ya pili katika kundi la Mamlaka za Udhibiti wa Kisekta (Industry and Sectoral Regulators – IPSASs Category) katika Tuzo za Uandaaji Bora wa Taarifa za Fedha kwa mwaka 2025, zilizoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika tarehe 26 Novemba 2026 katika viwanja vya APC, Bunju, jijini Dar es Salaam, ambapo TCAA ilitambuliwa kwa ubora wake katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Naibu Katibu Mkuu - Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, aliyemwakilisha Waziri wa Fedha. Kwa upande wa TCAA, tuzo hiyo ilipokelewa na Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka, Bw. Lembris Laanyuni, kwa niaba ya Mamlaka.

Utambuzi huo unaakisi juhudi endelevu za TCAA katika kuimarisha uwazi, usahihi na uwajibikaji katika taarifa za fedha, kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa hizo.

Mafanikio haya yanathibitisha dhamira ya TCAA ya kuzingatia misingi ya utawala bora, kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha usimamizi madhubuti wa rasilimali za umma.
Naibu Katibu Mkuu - Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua akikabidhi tuzo mshindi wa pili katika kundi la Mamlaka za Udhibiti kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka, Bw. Lembris Laanyuni katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Naibu Katibu Mkuu - Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa TCAA wakiongozwa na  Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka, Bw. Lembris Laanyuni (katikati) mara baada a kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa pili katika kundi la Mamlaka za Udhibiti katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA). Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Prof. Sylvia Shayo Temu na watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, wa NBAA, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi 
Picha ya pamoja

«
Next
This is the most recent post.
»
Previous
Older Post

No comments: