HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » WAZIRI MKUU AIPONGEZA WIZARA YA UCHUKUZI KWA UFANISI WA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI, AITAKA KUONGEZA KASI KUELEKEA DIRA 2050


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa hatua zilizopigwa katika kuendeleza miundombinu na huduma za uchukuzi kupitia ushirikiano na sekta binafsi, huku akisisitiza kuongezwa kwa kasi, ufanisi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo Novemba 16, 2026, wakati akifungua Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza, akieleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuongeza uwekezaji na kuboresha utoaji wa huduma za uchukuzi

Amesisitiza kuwa pamoja na hatua zilizofikiwa, sekta hiyo inapaswa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi, kuimarisha matengenezo ya miundombinu na usalama, pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za upungufu wa fedha na ucheleweshaji wa miradi

Akitoa salamu za Wizara, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali imeendelea kupiga hatua katika kuendeleza miundombinu ya reli, barabara, bandari na anga, sambamba na kuimarisha mifumo ya udhibiti na usimamizi wa sekta hiyo

Amesema mkutano huo unaofanyika Novemba 16–18, 2026, wenye kaulimbiu ya “Kuharakisha Utoaji wa Huduma Jumuishi za Uchukuzi, Ufadhili Endelevu na Uwajibikaji wa Sekta kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050” ni jukwaa muhimu la kutathmini mafanikio, kubaini changamoto na kuweka mikakati ya kuongeza ufanisi wa sekta

Awali, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Abubakar Assenga, ameipongeza Serikali kwa uwekezaji katika miundombinu ya uchukuzi na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa miradi ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi na taifa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akionesha tuzo mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na wadau mbalimbali wa Usafirishaji wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza.
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisoma hotuba pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Abubakar Assenga akitoa salamu za Kamati ya Bunge wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) 








 Mkutano ukiendelea


Picha za pamoja


«
Next
This is the most recent post.
»
Previous
Older Post

No comments: