HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

KITUO CHA AFYA HIMO JIMBO LA VUNJO CHAPATA VIFAA TIBA VYA MILIONI 74


Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

SERIKALI imeendelea kuboresha huduma za afya katika jimbo la Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo imetoa vifaa tiba katika kituo cha Afya cha Himo vyenye dhamani ya milioni 74 pamoja na gari la kubebea wagonjwa.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Charles Kimea alisema kuwa, kutolewa kwa vifaa hivyo vitasaidia kituo hicho cha afya kutoa huduma bora kwa wananchi kwani kipo katikati ya Jimbo hilo ambapo wananchi wa kata nyingi hutegemea huduma hapo.

“Tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hata mimi nilikuwa na wasiwasi hata nilipomuomba kukipandisha hadhi kuwa kituo cha Afya haikuwa na majengo ya Wodi , maabara jengo la mama na mtoto pamoja na mochwari lakini kwa sasa serikali imeanza kuboresha kwa kuleta vifaa tiba” alisema Dkt. Kimei.

Mbunge huyo alisema kuwa, katika kampeni za mwaka 2020 walifika kituo hapo na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwine Mollel na kumweleza shida na adha zilizokuwa zikiwakumba wananchi ambapo kitua hicho kilikuwa hakituo huduma masaa 24 na kuomba kipandishwe hadhi.

Alisem kuwa, katika jimbo la Vunjo baada ya sense ya watu 2022 ilionyesha kuwa katika jimbo hilo kulingana na idadi ya watu kila kata ilistaili kuwa na kituo cha afya ambapo tatizo lilionekana zipo kata hazina maeneo ya kujengewa vituo vya afya hivyo kwa sasa wamelenga kuboresha kati zenye maeneo kwa kujenga vituo vya afya.

Aliongeza kuwa, baada ya kupata vifaa tiba hivyo kituo hicho cha Afya ktalazimika kuongezewa wataalam wa afya ambao watatumia vifaa hivyo kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi katika kituo hicho, Dkt. Sudi Mohamed alisema kuwa, wamepokea vifaa tiba ambavyo ni drip stendi, mashuka 60, magodoro 15, vifanda vya wagonjwa na vifaa vingine ambapo alisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha huduma kwa wananchi .




UFAHAMU UGONJWA WA GOUT, DALILI NA TIBA ZAKE

Gout ni ugonjwa ambao umefahamika kwa miaka mingi sana. Inasadikika kuwa watu wa kwanza kuutambua ugonjwa huu walikuwa watu wa Misri, kunako miaka ya 2640BC. Mtaalamu wao wa tiba Hippocrates aliuita ugonjwa huu “Ugonjwa Wa Kumfanya Mtu Asitembee” na aliuhusisha ugonjwa huu na namna ya mtu anavyoishi. Hadi hivi leo ugonjwa huu ni tatizo la jamii nyingi, ambao huwapa maumivu makali sana wale ambao wameathirika. Kwa bahati nzuri ugonjwa huu hutibika na kuna hatua za kuchukua zinazoeleweka ili usipatwe na ugonjwa huu. Katika ukurasa huu tutatazama ugonjwa wa gout ni nini , chanzo cha ugonjwa wa gout, dalili zake na namna ya kuutibu pale unapokuwa umeathirika.


Gout Ni Nini?

Gout ni namna moja ya Arthritis, ugonjwa ambao hushambulia joints (sehemu za maungio ya mifupa). Huu ndio ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa maumivu makali wanaume. Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa baada ya kukoma hedhi. Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye sehemu linapoanzia dole gumba la mguu. Dalili za ugonjwa huanza kuonekana pale uric acid, tindikali ambayo huzalishwa na mwili katika ufanyaji kazi wake (ambayo haina manufaa kwa mwili) inapobakia katika viungo vya mwili na katika majimaji ya mwili. Uric acid iliyoganda (tophi) huweza kujikusanya na kubaki chini ya ngozi inayozunguka joints, huweza pia kujikusanya ndani ya figo na kusababisha kidney stones (namna ya kokoto ndogo ndani ya figo).

ugonjwa wa gout


Gout inaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye maungio ya mifupa na figo. Endapo hatua za kuutibu ugonjwa huu hazitachukuliwa kwa muda mrefu (miaka 10 au zaidi), madhara ya kudumu humtokea mgonjwa.


Chanzo Cha Gout Ni Nini?

Gout kutokea kimsingi pale tindikali aina ya uric (uric acid) inapozidi kiwango katika mwili wa binadamu hali ambayo kiutaalamu huitwa hyperuricemia. Tindikali hii ni matokeo ya kuvunjwavunjwa na mwili kwa aina fulani za chakula kama nyama,nyama ya mbuzi,ng'ombe  na chakula cha baharini. Tindikali hii kwa kawaida huchanganyika na damu na mwisho hutolewa nje ya mwili pamoja na mkojo kupitia figo. Tindikali hii ikitengenezwa kwa wingi mno au isipotolewa nje ya mwili kwa kiwango kinachosatahili, ile inayobakia huganda na kukaa kwenye maeneo ya joints na kusababisha maumivu kwenye joints hizo na maeneo yaliyo karibu. Kuna mazingira ambayo hupelekea hali hii ya uzidifu wa tindikali ya uric katika mwili na mwishowe gout kutokea nayo ni:
Jinsia: Wanaume huzalisha tindikali ya uric kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko wanawake, viwango vya uzalishaji kwa wanawake vikikaribia vile vya wanaume pale tu wanapokoma hedhi.

Urithi: Kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya gout kunakufanya uwe kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu.

Mtindo wa maisha: Unywaji wa pombe huzuia utolewaji wa uric acid nje ya mwili na ulaji wa chakula chenye purine kwa wingi husababisha kiwango cha tindikali ya uric kuwa kikubwa mwilini.

Madini ya lead: Kuwa karibu na madini haya kwa muda mrefu kumeonyesha kuhusika na aina fulani za gout.

Madawa: Baadhi a madawa yameonekana kuongeza kiwango cha uric acid mwilini.

Unene: Unene umedhihirika kuongeza hatari ya kupatwa na gout.

Matatizo ya kiafya: Kama figo hazifanyi kazi vizuri kiwango cha uric acid mwilini kitapanda. Matatizo mengine ya kiafya yanayochangia ni high blood pressure (hypertension), kisukari na hypothyroidism.

Dalili Za Gout

Ugonjwa wa gout huanza ghafla na mara nyingi katikati ya usiku. Ugonjwa huanza kwa kuleta maumivu makali kwenye maungio ya mifupa na mara nyingine kuambatana na uvimbe. Gout mara nyingi hushambulia maungio makubwa ya dole gumba la mguu lakini pia huweza kushambulia maungio ya mikono, ankles, viwiko vya mikono na vidole.

Tiba Ya Gout

Matatizo yaliyo mengi ya gout huondolewa kwa kutumia dawa. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs), colchicine au corticosteroids hutumika kuondoa maumivu kwenye eneo lililoathirika na gout.

Dawa nyingine hutumiwa ili kupunguza uzalishaji wa uric acid (xanthine oxidase inhibitors), mfano allopurinol au kuzisaidia figo ziweze kuondoa tindikali ya uric kutoka katika mwili (probenecid).
Mtindo wa maisha unaweza kusaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa huu au kuzuia usikupate. Yafaa kufanya yafuatayo:
– Kunywa maji mengi, lita 2-4 kwa siku
– Kutokunywa pombe
– Kuweka uzito wa mwili kwenye kiwango kinachofaa
– Kupata mlo uliokamilika (balanced diet)
– Kutotumia vyakula vyenye purines kwa wingi (vinavyozalisha uric acid kwa wingi). Vyakula vya kukwepa ni kama figo za ng’ombe, maharage na njegele zilizokaushwa, nyama pori, uyoga na maini.


IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG

UJUE UGONJWA WA MARBURG UNAOFANANA NA EBOLA


UTANGULIZI
Tarehe 19 0ctober 2017 shirika la afya duniani (WHO) lilitoa taarifa kuhusu kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa MRBURG (MARBURG VIRUS DISEASE) katika nchi jirani ya UGANDA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya UGANDA na shirika la Afya Duniani(WHO) mlipuko huo ulithibitishwa kwa kupitia vipimo vya maabara baada ya kutokea wagonjwa wane ambapo kati yao 3 walipoteza maisha.

Kwa kuzingatia kwamba nchi yetu inapakana nan chi ya Uganda,kutokana na mwingiliano wa watu na shughuli mabali mbaliza kijamii,upo uwezekano wa ugonjwa huu kuvuka mipaka na kuingia nchini kwetu.

NINI MAANA YA MARBURG
Marburg ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kitaalamu kama Marburg virus.
Ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kama homa ya virusi zinazosababisha kutoka damu sehemu za wazi za mwili mfano puani,masikioni,na machoni.
Huathiri binadamu na wanyama kama nyani,ngedele,sokwe na popo.
Ugonjwa huu usafiri kwa kasi na kusababisha vifo vya watu wengi.


NJIA ZA KUPATA MARBURG VIRUS.
Kutoka kwa mtu aliambukizwa au wanyama kwa:

  • Kugusa majimaji ya mwili toka kwa mtu aliyeambukizwa,mfano damu,matapishi,mkojo,jasho,mate,machozi na kamasi
  • Kugusa maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa Marburg
  • Kugusa godoro,shuka,blanket au nguo zilizotumiwa na mgonjwa wa Marburg
  • Kuchomwa na sindano au vifaa visivyo safi na salama
  • Kugusa mizoga au kula wanyama pori kama vile sokwe,nyani,na popo
  • Kula matunda yaliyoliwa nusu na wanyama wenye maambukizi.
Image result for marburg virus



MAKUNDI YENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA MAAMBUKIZI
Kila mtu yupo kwenye hatari ya kuambukizwa.
Makundi yenye hatari Zaidi ni kama
Watu wote wanaoishi na au kuhudumia wagonjwa wa Marburg
Waombolezaji kwa kugusa mwili wa marehemu kama sehemu ya utaratibu wa mazishi
Wawindaji
Watoa huduma za afya.



DALILI ZA UGONJWA WA MARBURG
Dalili huanza kujitokeza kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi

  • Homa kali ya ghafla
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya mwili misuli na viungo
  • Kuharisha majimaji(kunakoweza kuambatana na damu)
  • Maumivu ya tumbo(abdominal pain and cramping)
  • Kutokwa na damu puani,mdomoni,machoni,masikioni,na sehemu ya haja ndogo na kubwa.
  • Kutapika.
 Image result for marburg virus symptoms


TIBA KWA MGONJWA WA MARBURG
Hakuna tiba ya ugonjwa huu wala chanjo.
Mgonjwa hutibiwa kwa kutegemea dalili:
Tiba ya homa na maumivu
Kuongezewa damu na maji mwilini
Tiba lishe

JINSI YA KUJIKINGA
Njia za kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na
Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana
Epuka kugusa damu,matapishi,mkojo,kinyesi,kamasi,mate,machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa huu.
Nawa mikono na maji yanayotiririka na sabuni mara unapomtembelea mgonjwa hospitalini au kumhudumia.
Wahi kituo cha kutolea huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Marburg

#NINI KINATAKIWA KUFANYIKA
Kutoa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa huu na namna ya kujikinga na ugonjwa huu
Kuwajengea uwezo watumishi wa afya namna ya kuwahudumia wagonjwa wenye dalili za ugonjwa huu
Kuimarisha kamati za kukabiliana na maafa / majanga
Kuhakikisha kuwepo kwa dawa na vifaa tiba vya kutosha na vifaa vya kujikinga
Kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa kwa kutoa taarifa kama kuna mtu yeyote atakayeisiwa kuwa na ugonjwa huu.

ANGALIZO
NI muhimu kutoa taarifa mapema kutokana na kuwa ugonjwa huu hauna tiba halisi na huweza pelekea kifo kwa asilimia kubwa,hata hivyo matibabu yake ni kutibu dalili za ugonjwa.


IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG