Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
SERIKALI
imeendelea kuboresha huduma za afya katika jimbo la Vunjo wilayani
Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo imetoa vifaa tiba katika kituo cha Afya
cha Himo vyenye dhamani ya milioni 74 pamoja na gari la kubebea
wagonjwa.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt.
Charles Kimea alisema kuwa, kutolewa kwa vifaa hivyo vitasaidia kituo
hicho cha afya kutoa huduma bora kwa wananchi kwani kipo katikati ya
Jimbo hilo ambapo wananchi wa kata nyingi hutegemea huduma hapo.
“Tunamshukuru
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hata mimi nilikuwa na wasiwasi hata
nilipomuomba kukipandisha hadhi kuwa kituo cha Afya haikuwa na majengo
ya Wodi , maabara jengo la mama na mtoto pamoja na mochwari lakini kwa
sasa serikali imeanza kuboresha kwa kuleta vifaa tiba” alisema Dkt.
Kimei.
Mbunge huyo alisema kuwa, katika kampeni za mwaka 2020
walifika kituo hapo na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwine Mollel na
kumweleza shida na adha zilizokuwa zikiwakumba wananchi ambapo kitua
hicho kilikuwa hakituo huduma masaa 24 na kuomba kipandishwe hadhi.
Alisem
kuwa, katika jimbo la Vunjo baada ya sense ya watu 2022 ilionyesha kuwa
katika jimbo hilo kulingana na idadi ya watu kila kata ilistaili kuwa
na kituo cha afya ambapo tatizo lilionekana zipo kata hazina maeneo ya
kujengewa vituo vya afya hivyo kwa sasa wamelenga kuboresha kati zenye
maeneo kwa kujenga vituo vya afya.
Aliongeza kuwa, baada ya
kupata vifaa tiba hivyo kituo hicho cha Afya ktalazimika kuongezewa
wataalam wa afya ambao watatumia vifaa hivyo kutolea huduma za afya.
Kwa
upande wake, Mganga Mfawidhi katika kituo hicho, Dkt. Sudi Mohamed
alisema kuwa, wamepokea vifaa tiba ambavyo ni drip stendi, mashuka 60,
magodoro 15, vifanda vya wagonjwa na vifaa vingine ambapo alisema kuwa
vifaa hivyo vitasaidia kuboresha huduma kwa wananchi .
-
No comments:
Post a Comment