HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

PICHA: JINSI SHABIKI MAARUFU WA YANGA, ALLY YANGA ALIVYOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI

Shabiki wa Yanga maarufu kwa jina la Ally Yanga amefariki dunia jana  katika ajali ya gari. Ally Yanga alijizolea umaarufu mkubwa katika tasnia ya soka kotokana na jinsi alivyokuwa akivaa na kujichora pamoja na namna yake ya ushangiliaji anapokuwa uwanjani.

Ajali hiyo iliyohusika katika kifo cha Ally Yanga iiltokea jana  mkoani Dodoma
Klabu ya Yanga kupitia Idara ya Habari na mawasiliano wametuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa Ally Yanga kufuatia kifo cha mpendwa wao ambapo wamesema kuwa faraja ya Mungu ikawe na familia hiyo katika kipindi hiki kigumu.

“Uongozi wa Yanga SC umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Ally Yanga, hakika Mungu ni mwema, faraja ya Mungu wetu ikawe kwa familia katika kipindi chote cha majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.”
Aidha, kwa upande wao, Yanga wamesema kuwa wameachwa na pengo kubwa kutokana kutokana na kupoteza shabiki na mwanachama huyo maarufu.

“Pia nasi Yanga kifo chake kina acha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa na alikuwa balozi mzuri kama mwanachama na shabiki mkubwa wa timu yetu, Bwana alitoa, Bwana ametwaa.”




AJALI YATOKEA DUMILA MMOJA AFARIKI, JONAS MKUDE ANUSURIKA

NAHODHA wa Mabingwa wa kombe la Shirikisho na Kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam. Anaandika Mroki Mroki-Mroki Mroki.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo ilipotokea ajali hiyo, Dumila katika shamba la Mitiki, zinaarifu kuwa hakuna watu wawili ambao bado majina yao hajapatikana wameumia na Mkude kupata majeraha madogo na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.

Watu hao walikuwa katika gari aina ya Toyota VX lenye namba za Usajili T 834BLZ na walikuwa wakitokea Dodoma kushuhudia fainali za kombne la Shirikisho la Soka Tanzania uliopigwa jana katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma uliozikutanisha Simba na Mbao.

Simba ilishinda mchezo huo kwa bao 2-1 na kutwaa ubingwa huo na kujipatoia tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

WATU WATATU WAFARIKI RUFIJI BAADA YA MTUMBWI WAO KUZAMA

Watu watatu wamefariki dunia kwa kuzama majini na mmoja kunusurika kifo baada ya mtumbwi waliokuwa wakivukia kuzama bwawani wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo, Ofisa Tarafa ya Ikwiriri, Suleimani Mpangile aliwataja marehemu hao kuwa ni Sijali Abdallah (14), Zuberi Penya (11) wakazi wa Umwe Ikwiriri na Salehe Saidi (31) mkazi wa Dar es Salaam.
Mpangile pia alimtaja aliyenusulika kifo kuwa ni Musa Mkamba ambaye alikuwa akiwavusha marehemu hao.
Alisema chanzo cha vifo hivyo ni mtumbwi waliokuwa wakivukia kujaa maji na kuzama jana Jumamosi saa 3 asubuhi katika bwawa hilo la Umwe.

Wachimbaji wawili wafia ndani ya mgodi

Wachimbaji wawili wa madini katika kijiji cha Masuluti mkoani hapa, Haus Kaijage (32) mkazi wa Bukoba na James Mlawa(22) mkazi wa Magulilwa, Iringa wamefariki dunia baada ya kukosa hewa ndani ya mgodi.
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Masuluti, Venjaslaus Kiunosile amesema tukio hilo limetokea leo (Ijumaa) saa tano asubuhi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari miili ya marehemu imetolewa ndani ya mgodi.
Amesema chanzo cha watu hao kupoteza maisha ni kukosa hewa baada ya kuingiza jenereta la kuvuta maji mgodini kwa lengo la kuvuta maji na baada ya kuliwasha walikosa hewa.
Hata hivyo amesema jeshi la polisi linamshikilia mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa kwa mahojiano
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Mgama, Baraka Mwifune amesema uchunguzi wa awali uliofanywa umeonyesha kuwa watu hao walipoteza maisha kwa kukosa hewa.
Mmiliki wa mgodi huo, Msigwa amesema akiwa njiani kuelekea eneo la mgodi kwa ajili ya kusaidia kutengeneza mashine ya kuingiza hewa katika mgodi huo ndipo alipopata taarifa ya wachimbaji hao wawili kati ya sita kupoteza maisha kwa kukosa hewa.

WANAFUNZI WA LUCKY VICENT WALIOPATA AJALI WAPATA VISA YA KWENDA MAREKANI KWA MATIBABU

Mbunge wa Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu amesema Ubalozi wa Marekani umetoa hati ya kusafiria (visa) kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi watatu wa Shule ya Lucky Vincent kupata matibabu nchini Marekani.
Katika ukurasa wake wa Facebook leo Nyalandu amesema waliopata Visa ni wazazi,watoto na wataalamu wawili wa afya ambao watasafiri kwenda Marekani.
"Wote wamepewa visa asubuhi ya leo Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam. Akina Mama watatu, watoto wote watatu, na Daktari Moja na Nurse Moja. Kansela wa Ubalozi wa Marekani alinipigia simu asubuhi akiwasubiri katika siku ambayo haikuwa ya kazi,” amesema Nyalandu na kuongeza:
“Mungu ambariki sana kwa moyo huu. Napenda pia kutoa taarifa kuwa ndege yao aina ya DC 8 inatarajiwa kutua Leo usiku saa 2:15 majira ya Afrika Mashariki katika uwanja wa KIA. Mungu wa Watanzania awabariki wote kwa sala na dua zenu kwa ajili ya hawa watoto. Sifa na utukufu kwa Mungu wetu.”
Katika taarifa ya awali kwa vyombo vya habari Nyalandu amesema safari ya kuelekea Marekani itakua kesho asubuhi na ndege itatua Charlotte,New York na kisha wagonjwa pamoja na waliowasindikiza wataingia katika ndege nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa hadi katika mji wa Sioux City,Iowa
Watoto hao watatu walijeruhiwa wakati wakiwa katika safari ya masomo wilayani Karatu mkoa wa Arusha jumamosi iliyopita na kusababisha vifo vya wanafunzi 32,walimu wawili na dereva wao.

TRENI YA ABIRIA YAPATA AJALI MOROGORO

Treni ya abiria imepata ajali usiku saa 5 eneo la Stesheni ya Mazimbu Morogoro ambapo mabehewa manne yameegama na matatu yameacha reli.

Ashura Mrisho aliyekuwa anakwenda Tabora amejeruhiwa kwa kuangukiwa na mizigo. Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro kuwapangia usafiri mbadala 

WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA NYUMBA YAO KUANGUKIWA NA MTI .


 Baadi ya wananchi wakiondoa paa la bai ili kuokoa watu waliokuwa kwenye nyumba iliyoangukiwa na mti usiku wa kuamkia leo

Na,Vero Ignatus,Arusha
Kutokana na  mvua inayonyesha mfululizo Mkoani  Arusha imeleta maafa makubwa katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya(55) mkazi wa sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.



Mkasa huo wa kusikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo kung’olewa na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.



Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini Arusha.



Mkumbo aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili wa shule ya sekondari ya Inaboishu.

Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha.



Amesema watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo aliyetambuliwa kwa jina la Giliad  Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki (26) na Best Jonathani(20).



Kamanda Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla.



Alisema na kuitakia pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa sana kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika wakati huu mgumu kwake.



Kamanda Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.



Amesema kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali hiyo.

Aidha kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa jana kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na kufariki pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari hizo siyo za kweli wananchi wazipuuze kabisa 
 Mti ulioanguka ukang'ookana shina lake na kuangukia nyumba na kusababisha maafa hayo ya watu watano wa familia moja.
Jitihada za uokozi zikiendelea 
Miili ikiwa imeshapakiwa ndani ya gari la polisi kwenda kuhifadhiwa hospitalini

LOWASSA AWALILIA WANAFUNZI WALIOFARIKI KATIKA AJALI, MAITI 32 ZAPELEKWA MOCHWARI KATIKA HOSPITALI YA LUTHERAN KARATU.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.
Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema
Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.
Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.
Tutaendelea kuwapa habari zaidi kuhusu tukio hili.