HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MSANII WA BONGO FLEVA 'NILLAN' AMPONDA SHILOLE KWA KUHARIBU SHOW SIKUKUU YA PASAKA


Na Mwandishi Wetu
MSANII wa Bongofleva anayetamba na kibao cha ‘Njenje’ Gilbert Paul maarufu kama ‘NILLAN’ (pichani kulia) ameponda kitendo kilichofanywa na msanii  mkubwa katika  tasnia hiyo Zuwena Yusufu ‘Shilole’ cha  kuharibu Show iliyotarajiwa kufanyika mkesha wa siku ya mkesha wa Pasaka na hivyo kusababisha hasara kwa promota.

Nillan aliyetarajiwa kufanya show siku pamoja na msanii mwingine Nuhu Mziwanda alisema kitendo kilichofanywa na Shilole siyo cha kiungwana kutokana na heshima kubwa aliyonayo msanii huyo kwa Taifa hili.


“Ukweli kitendo hicho mimi kama msanii chipukizi kimeniumiza sana, sikutaraji kingeweza kufanywa na msanii mkubwa na maarufu kama Shishi, namuheshimu kama dada yangu lakini kwa hili amejishushia heshima” alisema Nillan.


Show hiyo iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya  Merry Merry Entertainment, ilishindwa kufanyika baada ya Shilole kuchelewa kufika ukumbini hali iliyosababaisha mashabiki waliofika mahali hapo kulalamika warudishiwe fedha zao na baadae kuondoka.


Akizungumzia baada ya tukio hilo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Merry Mussa mbali na kulaani kitendo hicho cha Shilole alisema  ni lazima sharia itafuata mkondo wake kwa msanii huyo kulipa hasara yote iliyotokana na kitendo alichokifanya.


“Haiwezekani mtu tukubaliane afike  ukumbini saa  2 usiku, yeye anakuja  muda anaotaka, na hapo hapo hata kushuka kwenye gari hakushuka, hiyo ni dharau na kamwe sikubaliani na kitendo hicho hata kidogo” alisema Merry.


Shilole aliyetarajiwa kutoa burudani  siku hiyo ya mkesha wa Pasaka katika ukumbi wa Heinken uliopo Kijichi, aliwasili ukumbini hapo saa 7 za usiku tofauti na makubaliano na Promota aliyeandaa show hiyo.


Hata hivyo alipotafutwa Shilole kuzungumzia suala hilo alidai kufika ukumbini hapo kama taratibu zilivyo za wasanii kufika kwenye show mbalimbali hivyo haoni kama kuna kosa lolote alilifanya kuhusiana na show hiyo.

Kwa upande wake Nuhu Mziwanda aliyewah kuwa mahusiano na msanii huyo alikwenda mbali na kusema kitendo kilichofanywa na mpenzi wake huyo wa zamani ni ushamba na kumtaka kurudisha fedha alizochukua kutoka kwa promota.
Alisema anashangazwa kwanini Shilole alikubali kupokea fedha hizo na kuahidi kufanya show lakini badala yake akaingia mitini na kuibukia ukumbini muda ambayo show ilipaswa iwe mwishoni.


Akizungumzia suala hilo Meneja wa kampuni ya Ochu Entertainment  inayomsimamia msanii Nillan, Felix Mkuya alisema kitendo kilichofanywa na Shilole ni cha kushangaza na hakipaswi kufanywa na  wasanii wa hapa nchini.


“Imagine watu wametumia gharama kubwa kuandaa ile Show, kila msanii alishapewa hela yake mkononi, sasa kwanini yeye afanye vile, Nuhu Mziwanda alifika ukumbini mapema saa 12 jioni, alikadhalika kwa Nillan…sasa vipi Shilole afanye vile” alihoji Mkuya.

KALA JEREMIAH AWACHANA WANAOJISIFIA

Msanii wa miondoko ya 'HipHop' nchini Tanzania, Kala Jeremiah awachana wasanii wenzake kuwa waache tabia ya kuharibu misingi ya 'HipHop' kwa kutunga nyimbo zenye mashairi ya kujisifia vitu walivyokuwa navyo na kusahau misingi ya muziki huo
Kala Jeremiah amebainisha hayo baada ya kelele za wadau wengi wa muziki wa aina hiyo kudai wasanii wengi wa kizazi hiki wanashindwa kuimba nyimbo zenye kuleta ujumbe wenye uhalisia katika jamii na matokeo yake wengi wanaangukia kwenye mashairi yasiyokuwa na tija.
"Kwangu mimi naamini 'Hip hop' ni kitu kinachotakiwa kije na ujumbe au kiwe na kitu fulani ndani yake, 'actually' ilikuwa hivyo zamani hapa bongo, yaani wimbo unakuta una ujumbe mzuri ambao unalenga jambo moja kwa kulichambua kwa kina, yaani hadi msikilizaji anapata hamu ya kushawishika kurudia na kurudia. 'Hip hop' ni uhalisia". Alisema Kala Jeremiah
Aidha msanii huyo aliendelea kuwachana kwa kusema marapa wengi wa bongo siku hizi hawaeleweki wanaimba nini ?, wanakazi ya kuwachanganyia vitu mashabiki
Kwa upande mwingine msanii huyo amewasisitizia wasanii wote kuzingatia nguzo za muziki wanaofanya na endapo wanataka kufanya biashara basi itakuja baada ya kufanya kazi nzuri.

Mh Temba atapeliwa shilingi milioni 100

Rapper kutoka TMK Wanaume Family Mh Temba ameelezea sababu za yeye kuwa kimya ni kutokana na kutapeliwa pesa na mfanyakazi wa bandari jijini Dar es Salaam. Temba amekuwa akimposti tapeli wake kupitia ukurasa wake wa Instagram ishara ya kumwinda tapeli huyo na kutangaza donge nono kwa atakayefanikiwa kumpata.

Kupitia kipindi cha Zero Planet ya Ice Fm temba amesema, “Nilishindwa kutoa kazi kwasababu hapa juzi kati nilikua na matatizo sikuweza kuyazunguma sana kwenye media. Kuna jamaa alifanya wizi kakimbia na pesa, ndio maana project zangu hazikuweza kutoka, alinidhulumu pesa nyingi sana.”
Alipoulizwa juu ya kiwango na biashara waliokuwa wanafanya na huyo jamaa, Temba alisema, “tulikuwa tunafanya kazi ya magari, huyo jamaa alikuwa anafanya kazi bandarini alikuwa anadili na haya magari ambayo watu wameshindwa kuyalipia ushuru kwahiyo si tunatoa pesa tunaenda kuyauza, tulikuwa na chama chetu cha washikaji kama 18 hivi kila mtu akatoa pesa kama milioni mia moja na kitu hivi,” ameongeza.
Amesema kumbe hata safari ya South Africa walivyoenda kushoot video ya ‘Waache Waowane’ ya Chege, Temba naye alikwenda kushoot video ya wimbo wake mpya japo hakufanikiwa na majanga yalipoanzia baada ya kuona jamaa hawatumii mkwanja kutoka kwenye biashara zao. Walivyorudi bongo ndio wakajua kuwa jamaa kawapiga mkwanja.
Temba na Chege kwa sasa wanafanya vizuri na wimbo mpya uitwayo ‘Go Down.’

NAPE AWAKINGIA KIFUA MASTAA WALIOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UNGA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewakingia kifua mastaa waliotuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, akieleza kuwa busara inahitaji katika kupambana na vita hiyo.

Licha ya kuunga mkono jitihada za serikali kupambana na biashara hiyo haramu, Nape amedai kuwa kuwatuhumu mastaa bila kuwa na uthibitisho ni kubomoa ‘brand’ zao walizohangaika kuzitengeneza kwa miaka mingi.
“Kutengeneza brand ni kazi kubwa sana, kuibomoa brand inaweza kuwa ni jambo la siku moja, tena la sekunde,” Nape amewaambia waandishi wa habari Jumapili hii.
“Kusema bana huyu kichaa the brand is destroyed. Lakini lazima kukaa chini kufikiria kwamba mwisho wa siku tunataka tupate matokeo gani. Ni vizuri kuliangalia tunalifanya katika namna ambayo inalinda haki ya mtuhumiwa ya kumpa room ya kesho na kesho kutwa kama ikithibitika kwamba hahusiki bado aliregain brand ama heshima ambayo atakuwa ameitengeneza,” aliongeza.
“Suala la njia iliyotumika niiache public ijadili na itaamua. Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwahiyo hawajabiki kutuuliza, akitaka anaweza kutuuliza. Lakini kwamba tulihusishwa hatukuhisishwa.”
Wema Sepetu, Vanessa Mdee, Mr Blue, TID ni miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

STEREO AMPIGIA MAGOTI CHEMICAL KUMUOMBA PENZI

Rapa Stereo akipiga magoti kumuomba Chemical akubaliane na ombi lake.

Msanii wa muziki wa hip hop Stereo ambaye siku za karibuni alitangaza wazi nia yake na hisia zake juu ya kuhitaji kwa udi na uvumba penzi la Chemical, Ijumaa hii akitutana live na mwanadada huyo na mkumpigia magoti kueleza kile kinachomsibu moyoni mwake.
Rapa huyo alikukutana na Chemical katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV na kuamua kuitumia nafasi hiyo kumchana kile kinachomsibu.
“Nathubutu kusema ukweli mbele ya umati wa watu wanaotazama hapa muda huu na ambao wanasikiliza kupitia redio wanaona na kunisikia kijana ambaye nampenda Chemical,” Stereo alisema akiwa amepiga magoti pamoja na kumshika mkono mrembo huyo.
“Hii sio siri tena Umma mzima utambue, nipo serious,” aliongeza.
Baada ya kauli hiyo, Chemical alisema “Nimeshakusikia” huku akidai hajawai kupitia experience ya mwanaume kumtokea live namna hiyo.

SELINE AFUNGUKA KUHUSU WASANII WA KIKE WA BONGO

Msanii wa kike aliyewahi kuwa chini ya usimamizi wa label ya The Industry iliyo chini ya kundi la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii Aika na Nahreel, Seline amefunguka kuhusiana na wasanii wa kike kutumia skendo kwa kujiongezea umaarufu.

Akizungumza na Mtangazaji Pk5tz wa kipindi cha Extra Fleva cha Uplands FM ya Njombe, Seline ambaye sasa yupo chini ya usimamizi wa Producer Mona Gangstar wa Classic Sound, amesema kitu anachokichukia kwa sasa ni wasanii wa kike kutumia skendo kwa ajili ya kupromote kazi zao.
Seline amedai wakati mwingine ni nzuri sababu zinamfanya msanii azungumziwe ingawa wakati mwingine ni vyema msanii akaamini katika kipaji alichonacho kwakuwa skendo zina changamoto yake.
Kwa upande mwingine, akizungumzia kuhusu uzoefu wa kuwa chini ya label, Seline amewatupia lawama wasimamzi wanaosimamia wasanii bila kuwa taaluma na hiyo.

BEN POL AJIBU TUHUMA ZA KUIBA IDEA YA WIMBO WAKE PHONE

Hit maker wa Moyo Mashine ambaye kwa sasa anafanya vizuri kupitia wimbo wake wa Phone, amemshauri Producer Sappy kufanya kazi kuliko kutengeneza maneno.

Ben Pol anaonesha kumshangaa Sa
ppy kwa kitendo cha kusema amewachukulia wimbo wao wakati sivyo. “Unajua sijaelewa kabisa hii issue ilivyokaa kwa sababu huu wimbo nimeandika neno moja moja,” Ben amemuambia mtangazaji wa Ice Fm, Gami Deetz
Mkali huyo wa Phone amefananisha kitendo hicho kama kujenga nyumba yako inaisha halafu baadaye anatokea mtu anasema nyumba ni yake. Alipoulizwa kwanini Sappy kaamua kufanya hivyo Ben Pol amesema, “Labda anataka aonekane, afanye kazi ataonekana haina haja ya kutengeneza drama.”
Kwa upande mwingine, Ben Pol amesema tarajia album kutoka kwake ambayo itatoka mwezi ujao (February) ikiwa na ngoma 12 ikiwepo Moyo Mashine Remix ft Chidnma, Phone ft Mr Eazi, Natuliza Boli, Bozimba ft Chidnma n.k.

YOUNG KILLER – SINAGA SWAGA INAIRUDISHA HIP HOP YA BONGO KWENYE MSTARI WAKE

Rapper Young Killer anadai kuwa wimbo wake mpya, Sinaga Swaga umekuja kuirudisha ‘real hip hop’ kwenye mstari.

Amedai kuwa kipindi cha hivi karibuni rappers wengi wa Bongo wamekuwa wakilegeza ngoma zao ili kuvutia biashara, lakini yeye ameamua kukaza.
“Dhumuni la kufanya hii ngoma, nimetaka kuwaonesha kwamba hip hop yetu bado ipo na ina nguvu kubwa na ina uwezo wa kufika mbali zaidi ya hapo ambapo ipo endapo tutaendelea kuisupport na kuipa nafasi,” rapper huyo amemuambia mtangazaji wa Pride FM, Eddy Msafi.

Rapper huyo amesisitiza kuwa masikio ya mashabiki wa muziki Tanzania yanahitaji ngoma za aina ya Sinaga Swaga na si kupewa nyimbo za kuimba na kuchezeka tu.