HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

HII NDIO HISTORIA YA MUZIKI WA DISCO TANZANIA

Image may contain: 12 people, indoor
Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Nimeona nikae chini niipitie maandiko ya mhenga moja aliyeandika habari ya DISCO iliyokua na kichwa cha habari "WAHENGA TULITESA SANA ENZI ZETU DISCO LA MCHANA (BOOGIE) NA MA-DJ WAKALI!!!" mwandishi wa habari hiyo amejitahidi sana kuelezea kwa mapana ya ufahamu wake jinsi gani alivyoujua muziki wa Disco wa enzi zile waliwemo maDj wake.

Mimi nimeamua kuweka sawa baadhi ya mambo Dj Kalikali yeye alishapiga muziki YMCA wakishirikiana na Dj Niga Jay na kuna wakati pia walipiga pamoja na Dj John Peter Pantalakisi na muda mwingi John Peter Pantalakis walikua wakishirikiana na Dj Chogy Sly Dico la Born City na kuna kipindi fulani Dj Kalikali alikua Dj wa Disco la RSVP ambalo Mbowe walianzisha tawi la DICO  katika hotel ya New Africa ghorofa ya saba.
Image may contain: 5 people, including Richie Dillon, people smiling, people standing and outdoor
Muziki wa Disco unasafari ndefu maDj wengi wa zamani walikua wanamuziki wa bendi na baadae kubadili mwelekeo na kuwa maDj kwa mfano Dj Sweet Francis na Dj Addy Sally chimbuko lao walitokea kwenye bendi na baadae miaka ya 1970 wakahamisha mawazo yao na kuwa maDj wakati huo kukiwa na Disco la Banda Beach, Sea View na madisco mengine Kilimanjaro Hotel Summit

Nataka nikupe historia ya musiki na disco theque.Africana Gogo Disco lilianza mwaka 1971 na aliyeanza kupiga disco hapo ni Bhoka Wilson (Mzimbabwe) wakati ule ikiitwa Southern Rhodesia naye alikuwa cabbaret singer Simba Grill Kilimanjaro hotel. August 1972 Dj Sweet Fransis akawa Dj hapo mpaka Nov.1973 kisha akawa Dj. Judy Kingui (Msouth Africa ambaye alikuwa mkewe Kingui aliyekuwa mwenye The Rifters Band. Judy alikuwa Dj.hapo Gogo Disco mpaka 1975.

Katika historia ya muziki wa disco Tanzania ambayo inabeba Madj wengi wengine wakiwa wametangulia mbele ya haki 
Disco la XTC ambalo maDj hawa wamepitia David , Lawrance , Pailonga, TNT Jackson

Disco la Valentinos/Continental haliwezi kutajwa bila ya watu hawa Ibrahim G ,Camal, Mr A, Salai, Meb, Guru, Sabry Kube


Disco la Rungwe 110 halijakamilika bila ya watu hawa Chogy Sly JP Pantelakis, Roma Pop Juice, Amon Washington, Agib Show, Ibony, Ntimizi, Bhester, Kim and the boyz, John Bure na wengineo
Image may contain: 5 people, including Muhidin Issa Michuzi, people smiling, people standing, stripes, beard and outdoor
Dj Sweet Francis jina kamaili ni Francis James Bundala,mwaka 1964 alianzisha bendi iliyoitwa The Screemers na Dj Sweet Francis akiwa mwimbaji(singer) hapo ndipo alipopewa jina la SWEET baada ya kusikia sauti yake na jinsi alivyokuwa akiimba iliwakuna sana na wakawa wanasema "YOUR VOICE IS SO SWEET " na ndiyo hapa akawa anaitwa Sweet. Hiyo ni hapa Dar.Bendi The Screamers ilidumu muda mfupi. Mwaka 1965 alianzish a bendi nyingine ya watu 5 wakaiita The Hot Five wakawa wanapiga bugi kila Jumapili mchana hapo Arnatoglo hall Mnazi mmoja. Wakawa wanashindana na bendi ilikuwa inaitwa The Flamming Star.

 Mwaka 1967 June The Hot Five ikavunjika. 1967 Sept. Dj Sweet Francis na aliyekuwa Solo guitarist wakaanzisha bendi nyingine wakapata watu wengine 3 ambao walianza kuwafundisha ambao walikuwa mpiga bass, mpiga rythym na drummer. Bendi wakaiita The TONICS. Mwimbaji- Sweet, Solo- Michael Jackson, Rythym- Green Jackson. Bass- John Morand na Drums- Charles Alowasa. 

Baada ya mazoezi makali mwezi November1967 wakaapata mkataba wa kupiga muziki kila siku hapo Splendid Hotel iliyokuwa inamilikiwa na mtaliano aliyeitwa MOSKA mtaa wa Samora zamani ukiitwa Independence Ave.

Siku moja wakati wanapiga muziki jamaa mmoja ambaye hawakuwa na mazoea naye akaja kwenye stage akaomba apige bongos wakamruhusu, wakati Dj Sweet Francis anaimba na yule jamaa akawa amapiga bongos vizuri sana Dj Sweet Francis akawaambia wenzake kuwa anafaa kuwa drummer lakini wenzake walimkatalia na baada ya kuwasihi sana walikubali kwa sharti kuwa amfundishe kupiga drums mpaka ajue. 
Image may contain: 10 people, including Ahmed Chande and Peter Moe, people smiling, people standing and outdoor
Baada ya kumfundisha kwa muda mfupi akaona ameelewa na baada ya kumpa nafasi kwenye stage alipiga drums na wenzangu wakamfurahia, huyo alikuwa anaitwa Adam Salehe Mwambile (R.I.P.) na tangu siku hiyo Dj Swett Francis akamwambia kuazia leo utaitwa ADDY SALLY,  ilikuwa mwezi April 1968, hilo ndiyo lilikuwa chimbuko la ADDY SALLY. 

May 1968 mkataba ulimalizika hapo Splendid  wakaamua kwenda mikoani.Wakati wote huo Dj Sweet Francis alikuwa mfanyakazi wa NPF sasa ni NSSF.

Dj Sweet Franacis aliamua kuacha kazi maana alivutiwa sana na muziki. July 1968 walifika Arusha wakiwa wanamuziki 5 na fundi mitambo aliyejulikana kwa jina Joseph Magali. 

Yule drummer wa kwanza .walimwacha baada ya kumwona Dj Addy Sally anafaa zaidi. March 1970 Dj Sweet Francis walirudi Dar. May1970  Dj Sweet Francis na Addy waliacha bendi kwa kutoelewana na Michael Jackson ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Bendi.

July 1970 Dj Sweet Francis alienda Mombasa na kuanza kuimba na Sunshine club. Mwezi Sept.1970 Dj Sweet Francis alimwita Dj Addy Sally Mombas akawa anapiga drums Central night club, May 1971 wakarudi wote Dar. 
Image may contain: 1 person, sitting
Wakati huo The Tonics wakiwa Nairobi waliwaita Dj Sweet Francis na Addy Sally huko, Dj Sweet Francis alikataa ila Dj Addy Sally akaenda.

Dj Sweet Francis akawa anaimba mara moja moja Simba grill Kilimanjaro Hotel wakiwa na bendi kutoka Spain iliyoitwa Los Valdos na hotel ikiwa ya chini ya raia kutoka Israel aliyejulikana kwa jina la LEVY na meneja mkuu wa hotel akiitwa FERGUSON raia wa Canada.


Kwa vile Africana hotel ilijengwa kutokana na faida ya pesa za Kilimanjaro hotel hivyo mmiliki alikuwa mmoja na mwaka 1971 ilianzishwa Gogo Disco baada ya kuhamisha disco kutoka Summit, Kilimanjaro hotel kwenda Afrikana.  Bokha Wilson alikuwa msanii wa Cabaret Simba grill pia kuwa Dj. Summit akahamishiwa Gogo disco hotel Africana. August 1972 Bokha Wilson akarudishwa Simba grill na Dj Sweet Francis akapelekwa Africana Hotel kuwa Disc Jockey Gogo Disco Theque.

Wote waliotajwa hapo mwanzo wameshatangulia mbele ya haki isipokuwa Dj Sweet Francis na Bhoka Wilson hatuna taarifa zake, miaka ya 80 alikuwa Ujerumani. baada ya kuwa Dj wa Gogo disco.
Image may contain: 3 people
Image may contain: one or more people and outdoor
Dj Sweet Francis alipanda kwenye stage na kuanza kuimba, cha ajabu kila mtu aliufurahia sana huo wimbo na walimshangilia sana na aliporudi mezani kwake, yule jamaa ambaye hakumjua alisimama akampa mkono akasema " Kumbe hapa tumekaa na mwanamuziki mzuri hivi, (akaendelea) Sikia kijana mimi najenga hotel hapo mtaa wa Uhuru na karibu kumalizika, hivyo ikiwa tayari wewe nataka uanze muziki hapo. Dj Sweet Francis akamkubalia, Hotel ikawa tayari Nov.1979  na kabla ya Dj Sweet Francis hajajiunga na Keys Hotel alipiga Disco kwa muda mfupi Mbowe Hotel na hapo ndipo alipomfundisha Dj.Jerry Kotto na Dj Sweet Francis akaanza kupiga Disco Keys Hotel  Dec.1979.

Baada ya Addy Sally kurudi toka Lusaka, mwezi April 1980 wakawa pamoja hapo Keys Hotel akiwa vyombo vya Disco vipya kabisa vikiitwa M3. waliendelea pamoja hapo Keys Hotel lakini kufika Dec.1980 Dj Sweet Francis walishindwa kuelewana na Addy, ikabidi Addy aondoke.

Jan.1981 Dj Sweet Francis akawa na Dj. Seydou na baada ya muda kidogo Dj.Seydou akaondoka baada ya mzee Ndesamburo (R.I.P) kununua vyombo vya Disco na baada ya hapo Dj Sweet Francis akapiga Disco na Dj Johnson Pantaleo (R.I.P) na ndiye Dj Sweet Francis aliyemuacha Keys hotel,
June 1981 ndio ukawa mwisho Dj Sweet Francis wa kupiga disco.
Image may contain: 5 people, people sitting
Mwezi Sept.1981 Dj Sweet Francis alienda Ujerumani na nchi zingine za Ulaya, alirudi Dar. Sept.1983 baada ya mapumziko 1993 Oct. akaanza tena kuwa Cabaret singer hapo International Pub, Kijitonyama nyuma ya Sayansi na Teknolojia mpaka June-August 1994.  Sept 1994 Simba Grill Kilimanjaro Hotel. Nov.2003--June 2004 Cine Club. Hii ndiyo historia yake katika tasnia ya muziki. Mwanamuziki na Disc Jockey "SWEET FRANCIS."

Baada ya kumalizana na hiyo historia ndefu na nzuri ya Dj Sweet Francis sasa turudi tena kwenye historia ya Disco wakiwemo maDj wake.

Disco la Motel Villa pamoja na madj wengi kupitia hapa lakini dj maarufu wa hapo alikua Kim and The Boys ambaye pia kuna wakati alikua maarufu katika kupromoti madansa.

Paul Mc Ghee alianzia Morogoro akiwa na disco la Biribi likiwa chini ya usimamizi wa kaka yake Joseph Kusaga anayeitwa Justine Kusaga. Baadae Disco lilikua chini ya usimamizi wa Joe Kusaga nakubadilika jina na kua Mawingu Dj alikua Paul Mc Ghee na baadae Disco lilihamia Dar likiwa linapiga muziki wake Salender Bridge na ndio ukawa mwanzo wa kukua kwa Disco hilo na kuendelea kupiga Motel Agip, Pool side hotel ya Kilianjaro kila Jumapili, New Africa ghorofa ya Saba, Twiga na baadae wakaanzisha Disco la Bolingo Tazara, na kuendelea kupanua wigo wao mpaka Arusha. Clouds walikua na maDj wengi na Disco hili lilikuza vipaji, vijana wengi wa enzi hizo wakiwemo Boni Luv, Stev B (R.I.P.), Rankim Ramadhani (R.I.P.) na wengine wengi wakiwasaidia maDj Jesse Malongo, Dj Young Ray akiwemo Joseph Kusaga  mwenyewe.

 Hapa ni baadhi ya maDj waliokua chini ya Joe Kusaga Dj Jesse Malongo, Sterwat Chiduo (Dj Young Ray), Elliud Pemba, Dj Louis, Ebonite Who jack, Julius Tandau, Julius Kagaruki, Boni. Luv, Stev B (R.I.P.), Clouds Ma Dj tulikuwa Elliude Pemba (Elliwood), Jesse Malongo (Babyface), Joseph Kussaga (Emperor), Stuart Chiduo (Young Ray), Julius Tandau (Jet), Richard Mazula (Ebonite woo Jack)
Elliud Pemba (Dj Elliwood) safari yake ya muziki imeanzia Clouds pale Motel Agip Snack Bar, Kilimanjaro Pool Side, Seventh Floor New Africa Hotel, Dar es Salaam Institute na Twiga.

Dj Ellud Pemba ndio niliyemwachia Dj Boni luv U Dj mwaka 1992 baada ya kwenda Shule na 1994 Kuanza kazi nyingine ITV.


Disco la Space 1900 wakati huo likiwa chini ya usimamizi Sudi Ally Salehe lilianzia Mbowe chini ya maDJ Saydou na Gerry Kotto na Sudi Ally Salehe walikua washirika na Dj Saydou walichangia vyombo vya muziki disco pamoja.

Hamisa afunguka, amtaka Diamond Awaambie Ndugu Zake Waache Dharau na Wamheshimu


Mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye ni mama mtoto wa Diamond Platinumz amefunguka kupitia ukuraasa wa Instagram wa Baba mtoto wake, Diamond Platinumz mara baada ndugu wa msanii huyo kuongea maneno yaliyoonesha kumkejeli.


Kufuatia maneno hayo ambayo yamezagaa katika mtandao wa Instagram Hamisa ameibuka na kuandika waraka mzito akimtaka Diamond Platinumz kuoa mwanamke ambaye ndugu, maneja na mashabiki wa Diamond wanamtaka aoe kwani katika andiko lake ameonesha kukerwa na baadhi ya maneno yaliyoongelewa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye mara baada ya wimbo wa Iyena kutoka.

Ambapo katika wimbo huo Diamond ameonekana akifunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake Zarinah Hassan.

Ndo uoe Huyo Mwanamke ambae anatakiwa na Ndugu zako … na manager zako bila kusahau mashabiki … sio kutwa mie mtoto wa watu naandamwa na kukaliwa mie kooni!!! Sijakuita wala kukufunga kamba ……

Kila siku maneno mimi Kwani alishindwa kukufata kukushauri ? Mpaka akimbilie kwenye MaTv na Mitandao ? Unapokaa hapajui , number ya simu yako pia hana? …. kwani mie hayo maTv hayaombi kuniombi kunihoji mbona nakaa kimya ? Tena saa ingine nakaa Kimya kuwastiri kwa mengi na pia dee akikua asione hii migogoro lakin ndugu zako hawabebeki its too much 🙌🏽 talk to Your familia maana wewe ni mwananume na uwezo wa kuyamaliza ……… 

Na pia waambie unahitaji Mke sio House girl wa Nyumba🤚🏽… Mwanamke kazi yake kukupikia Ule , au nlikua sikupikii tena sio wewe tu na Ndugu zako mkala na kusaza ? … leo imekua hamisa hajui kupika kusafisha nyumba kwahiyo chumba chako tukimaliza lalana huwa anasafisha nani ? 

Au walitaka niende kuwafulia vyupi vyao nikimaliza niwapigie deki mpaka chumbani kwao ? Wakishindwa kuniheshimu basi waambie waheshimu damu yako . The End !

Mobeto amefunguka hayo kufuatia post mbalimbali zilizokuwa zikitumwa na watu wa karibu wa Diamond Platinumz wakidai kuwa wamemkumbuka sana Zari hivyo wanataka arudi ili ndoa iweze kufungukika.

Wimbo wa Iyena pamoja na mistari yake umewaibua watu wengi na mashabiki wengi ambao wameonekana kumshambulia kwa maneno mwanadada Hamisa Mobetto.

HEINEKEN YANOGESHA FAINALI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA UEFA CHAMPIONS LEAGUE JIJINI DAR

Baadhi ya mashabiki wa Real Madrid wakiongozwa na Jamillah Mwarangi (katikati) wakisherehekea fiaiali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions League George & Dragon Bar iliyopo Masaki. Real Madrid walifanikwa kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken.
Shabiki wa Real Madrid Roseema Maro akihohiwa na Jimmy Kabwe baada ya ushindi wa fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions. Real Madrid walifanikwa kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken.
Shabiki Wa Real Madrid Alex Kushuma (kulia) akitoa pongezi za dhati baada ya Real Madrid kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken. Kushoto ni Jimmy Kabwe aliyesherehesha fainal za UEFA Champions League George & Dragon Bar Masaki.
Albert Kadino (wakwanza kulia) akipokea zawadi yake kutoka Mkuu wa kitengo cha biashara (Key Accounts Manager) Heineken Tanzania Bi Fatma Mnaro baadha ya kutabiri ushindi wa magoli 3-1 wa Real Madrid. Real Madrid walifanikwa kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken.
Shabiki wa Real Madrid Roseema Maro akihohiwa na Jimmy Kabwe baada ya ushindi wa fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions. Real Madrid walifanikwa kuwafunga Liverpool 3- 1 na kuibuka washindi kwa mara ya tatu mfululizo wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Champions League inayodhaminiwa na kinywaji cha Heineken.


Fursa hii ya aina yake iliwalenga wapenzi wa soka, wateja wa Heineken Tanzania na ilifanyika katika sehemu nane tofauti nchini.

Heineken imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na itaendelea kuwa mmoja wa wadhamini wakubwa wa ligi hiyo hadi kufikia mwaka 2021. ---

Ulikuwa ni usiku wenye shamra shamra na msisimko wa aina yake pale ambapo wapenzi wa soka, na watu maarufu walipokutana kwa pamoja Msasani jijini Dar es Salaam kushuhudia fainali za Klabu Bingwa Barani Ulaya kwa mwaka 2018.

Zaidi ya mashabiki 2600 wa Kitanzania, waliweza kufurahia fursa ya kipekee ya kutazama fainali hizo katika mazingira safi ambapo miamba wa soka Liverpool kutoka nchini Uingereza walikutana na miamba wa Hispania Real Madrid. Katika mtanange huo Real Madrid .walitawazwa mabingwa baada ya kuwalaza Liverpool .kwa mabao 3 – 1.

Ikiwa mmoja wa wadhamini wakuu wa ligi hiyo maarufu na inayotizamwa na mamilioni ya watu kote duniani, Heineken iliweza kuwaleta pamoja Watanzania chini ya bia yao pendwa ya Heineken na kupata fursa ya kutazama fainali hizo.

Meneja wa Heineken Afrika Mashariki Njeri Mburu alisema, “Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni moja kati ya ligi zinazohusisha wachezaji wakubwa. Timu zote bora barani Ulaya zinashiriki ligi hii. Kwa uapnde mwingine, bia ya Heineken ni bia inayojulikana na kutumiwa na watu wengi kote duniani na kwa hiyo kuna uhusiano kati ya Heineken na ligi ya mabingwa. Mwaka huu, wateja wetu siyo tu hawatafurahia kutazama ligi bali pia kushiriki fursa zinazokuja na ligi,”

Aliongeza “Bia ya Heineken inatengeneza msisimko katika ligi hii kubwa duniani kwa kuwaleta pamoja kwa mamna ya pekee ambayo ni Heineken tu wanafanya. Kwa Tanzania, Heineken imetoa haki za kipekee kwa mashabiki kuweza kushirikia katika kutizama fainali katika mazingira tulivu na ya aina yake kwenye maeneo mbali mbali kama Red Sea Arena, George & Dragon na Club 777. Fainali hii pia ilitizamwa katika shehemu tofauti tofauti 8 katika shehemu mbali mbali nchini,”

Njeri aliongeza kuwa, wateja wa Heineken waliweza kushiriki pamoja na kubadilishana taarifa za matukio wakati wakitazama fainali kupitia kibwagizo #ShareTheDrama

“Tunafurahi kuwa bia ya Heineken ni bia ya Watanzania na siku zote wamekuwa sehemu ya kile tunachokifanya na hata wanam kunywa zaidi bia yetu,” aliongeza

Alisema ikiwa kama bia yenye jina kubwa, siku zote imekuwa ikidhamini na kuwekeza kwenye michezo ambayo inayowagusa wateja wake na kuwaleta pamoja katika masoko yanayochipukia kama Tanzania.

Wakati wa fainali hizo, Heineken iliwazawadia wateja wake bidhaa mbali mbali zi zinazotokana na ligi hiyo.

Aunty Ezekiel Awataka Watu Waache Kumdharau Mpenzi Wake Kisa Dansa

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amewatolea povu zito watu wote ambao wamekuwa wakimdharau mpenzi wake lakini pia Baba wa mtoto wake Mose Iyobo kisa ni mchezo shoo.

Aunty Ezekiel ameweka wazi kuwa hapendezwi na dharau hizo kwani ingawa wao wanaweza wakawa wanamuona yeye kama Dansa tu lakini yeye anamuona kama mkurugenzi fulani.

Aunty alisema amekuwa akifuatilia kwenye mitandao ya kijamii na kuona watu wakimchukulia poa Iyobo lakini anawaambia tu, yeye kwake anamuona kama mkurugenzi.

"Waache kumchukulia poa Moze wangu. Mimi namuona kama mkurugenzi fulani hivi, wao wakiona mtuanacheza muziki hawajui kama ni kazi, hawathamini na kuonesha dharau tu mitandaoni”.

Mose Iyobo ni Dansa maarufu kutoka WCB ambaye kwa muda mrefu ameonekana kwenye steji na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz akiwa anakata viuno.

Aunty Ezekiel na Mose Iyobo walikutana miaka minne iliyopita na mara moja watu walianza kumponda Aunty kwa kutoka na Mose Iyobo jambo ambalo hakujali.

Harmonize aeleza undani wa video ya faragha ya Diamond na Hamisa

Msanii Harmonize amedai kuwa video ya faragha iliyovuja mtandao ikimuonyesha Diamond akiwa na wanawake wawili ambao miongoni mwao alikuwepo Hamisa Mobetto, ilikuwa ni sehemu ndogo ya movie waliyokuwa waki-shoot.

Harmonize ameiambia Citizen Radio kuwa movie hiyo inalenga kuwafundisha wanaume ambao wamekuwa na tabia za kuwadhalilisha wanawake.

“Walikuwa wanashuti movie ambayo inaelezea wanaume ambao wanadhalilisha wanawake. Sasa ili iweze kuleta attantion, ile iweze kulata item of bisness, iweze kuleta value wakamtumia Diamond kama mtu ambaye ameshaonekana katika mahusiano tofauti tofauti,” amesema Harmonize.

Utakumbuka April 19, 2018 Diamond Platnumz aliomba radhi Watanzania kutokana na kusambaza video hizo, hiyo ilikuwa ni baada ya kuitwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo alisema kuwa amejifunza sheria za makosa ya kimtandao na kuhaidi kutorudia tena.

Katarina Amvaa Ebitoke

Mchekeshaji wa kike Bongo aliyejizolea umaarufu mpaka nje ya nchi Katarina Karatu, amesema kauli ya Ebitoke kwamba Tanzania hakuna wachekeshaji wa kike, amekosea kwani wako wengi sana.

Katarina amesema licha ya kwamba hajisikii kumuongelea Ebitoke, lakini kauli aliyoitoa haileti maana na inavunja moyo, kwani wachekeshaji wapo wengi isipokuwa mashabiki ndio wanaamua nani ni mkali zaidi.

“Yule ni mtu mzima anajua anachofanya kwa hiyo kuanza kumuongelea sijisikii kwanza, nahisi sifanyi kitu sahihi, kuhusu wachekeshaji wa kike kwanza anakosea, wapo wengi tu kuna watu wanafanya vizuri, ni mashabiki wanaamua nani ni bora na nani anavamia fani, ila kuhusu yeye sihitaji kumuongelea sana kwa sababu zangu binafsi”, amesema Katarina.

Mchekeshaji huyo ameendelea kwa kusema kwamba ili kuthibitisha kuwa wachekeshaji wazuri Tanzania wapo, hivi karibuni amepata mwaliko nchini Kenya ambapo atapanda jukwaa moja na wachekeshaji kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki, Anne Kansiime wa Uganda, Idirs Sultan wa Tanzania na wengine wa Kenya.

Wema Sepetu amcharukia Hamissa Mobeto

Msanii wa Bongo muvi nchini, Wema Isaack Sepetu amesema amejiwekea mipaka na mwanamitindo Hamisa Mobeto kwani amesema mazoea yakizidi sana na mlimbwende huyo hupelekea mushkeri.

Wema amesema hayo pindi alipoulizwa juu ya uhusiano wake na mlimbwende Hamissa Mobeto mara baada ya kuzaa na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Diamond Platinumz na kujikuta anapunguza urafiki waliokuwa nao hapo awali.

”Hamisa ni kama Mdogo wangu, lakini kuna wakati sijui mazoea yakizidi sana kunaleta mushkeri kidogo, kwahiyo kila mtu anatakiwa kubaki kwenye mipaka yake,” amesema Wema.

Amezungumza hayo katika hafla fupi iliyoandaliwa na wasanii wa Bongo muvi ya kumpongeza mwanadada huyo kwa kujishindia tuzo za Sinema Zetu zilizoandaliwa na Azam Tv mwezi uliopita.

Aidha, Wema aliwashukuru wasanii wenzake kwa hafla hiyo na kusema ameyasikia maneno ya baadhi ya wasanii walioponda baada ya yeye kupata tuzo hizo, lakini anazichukulia kama changamoto za kimaisha.

Azam Tv ilitoa tuzo hizo usiku wa Pasaka, Aprili 1, 2018 ambapo Wema Sepetu alishinda tuzo mbili ambazo ni tuzo ya ”Best Views Choice” yaani tuzo iliyopendekezwa na mashabiki na sio majaji, na Tuzo nyingine ni Muigizaji bora wa kike.

Shamsa Ford Amjia Juu Harmonize Kwa Kuingilia Ndoa Yake

Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.

Siku ya jana Wolper, Harmonize na Sarah walikuwa kwenye vita kali ya Kwenye mitandao ya kijamii na katika harakati hizo Harmonize alianika orodha nzima ya wanaume ambao Wolper amewahi kujivinjari nao na mmoja kati ya watu hao ni Chidi Mapenzi.

Chidi Mapenzi ni mume halali kabisa wa Shamsa Ford kwahiyo baada ya kusikia mumewe katajwa Kwenye orodha hiyo alishindwa kujizuia kwani alikuja juu na kumtaka Harmonize amkome mumewe na asimuingize Kwenye ugomvi wao.

Shamsa alienda kukomenti maneno haya Kwenye posti ya Harmonize:

"Harmonize nakuheshimu sana mdogo wangu pls nisingependa kuona jina la mume wangu Kwenye huo ujinga wenu. Chidi kwenu anaweza akawa mshkaji kwangu mimi ni mume, kulikuwa hakuna haja ya wewe kuweka jina lake wakati unajua ana maisha mengine. Tusichukuliane Poa”.