HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » Hamisa afunguka, amtaka Diamond Awaambie Ndugu Zake Waache Dharau na Wamheshimu


Mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye ni mama mtoto wa Diamond Platinumz amefunguka kupitia ukuraasa wa Instagram wa Baba mtoto wake, Diamond Platinumz mara baada ndugu wa msanii huyo kuongea maneno yaliyoonesha kumkejeli.


Kufuatia maneno hayo ambayo yamezagaa katika mtandao wa Instagram Hamisa ameibuka na kuandika waraka mzito akimtaka Diamond Platinumz kuoa mwanamke ambaye ndugu, maneja na mashabiki wa Diamond wanamtaka aoe kwani katika andiko lake ameonesha kukerwa na baadhi ya maneno yaliyoongelewa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye mara baada ya wimbo wa Iyena kutoka.

Ambapo katika wimbo huo Diamond ameonekana akifunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake Zarinah Hassan.

Ndo uoe Huyo Mwanamke ambae anatakiwa na Ndugu zako … na manager zako bila kusahau mashabiki … sio kutwa mie mtoto wa watu naandamwa na kukaliwa mie kooni!!! Sijakuita wala kukufunga kamba ……

Kila siku maneno mimi Kwani alishindwa kukufata kukushauri ? Mpaka akimbilie kwenye MaTv na Mitandao ? Unapokaa hapajui , number ya simu yako pia hana? …. kwani mie hayo maTv hayaombi kuniombi kunihoji mbona nakaa kimya ? Tena saa ingine nakaa Kimya kuwastiri kwa mengi na pia dee akikua asione hii migogoro lakin ndugu zako hawabebeki its too much 🙌🏽 talk to Your familia maana wewe ni mwananume na uwezo wa kuyamaliza ……… 

Na pia waambie unahitaji Mke sio House girl wa Nyumba🤚🏽… Mwanamke kazi yake kukupikia Ule , au nlikua sikupikii tena sio wewe tu na Ndugu zako mkala na kusaza ? … leo imekua hamisa hajui kupika kusafisha nyumba kwahiyo chumba chako tukimaliza lalana huwa anasafisha nani ? 

Au walitaka niende kuwafulia vyupi vyao nikimaliza niwapigie deki mpaka chumbani kwao ? Wakishindwa kuniheshimu basi waambie waheshimu damu yako . The End !

Mobeto amefunguka hayo kufuatia post mbalimbali zilizokuwa zikitumwa na watu wa karibu wa Diamond Platinumz wakidai kuwa wamemkumbuka sana Zari hivyo wanataka arudi ili ndoa iweze kufungukika.

Wimbo wa Iyena pamoja na mistari yake umewaibua watu wengi na mashabiki wengi ambao wameonekana kumshambulia kwa maneno mwanadada Hamisa Mobetto.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: