HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Waliotimuliwa 1993 waibwaga tena BoT

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Jaribio la kupinga hukumu ya kuwarejesha kazini wafanyakazi 31 waliopunguzwa mwaka 1993, limekwama tena baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi ya Benki Kuu Tanzania (BoT) ya kuongezewa muda wa kukata rufaa.
Nje ya Mahakama jana, wakili wa BoT, Sereni Mponda alisema anakusudia kuwasilisha rufaa kwa kutumia kipengele kingine akitaka mahakama ikubaliane na maombi yao ya kukata rufaa nje ya muda, akisema BoT ina nafasi kubwa ya kushinda kwa kuwa kuna suala aliloliita zito la kisheria linalohitaji mwongozo wa Mahakama ya Rufani.
Alidai Mahakama Kuu ilikosea kwa kuamini kuwa mkataba wa hiari uliotumika kuwapunguza wafanyakazi wote ulikuwa batili kwa sababu haukusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Ajira.
Oktoba 2, Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali maombi ya BoT ya kuongezewa muda wa kukata rufaa kupinga uamuzi wa kuwarejesha kazini wafanyakazi hao ambao shauri lao limedumu kortini kwa miaka 22.
Lakini taasisi hiyo kuu ya fedha nchini ikaomba Mahakama ya Rufani irejee hukumu yake ya kutupa maombi yao ya kuongezewa muda wa kukata rufaa, ambayo jana yaligonga mwamba tena.
Watu hao 31 ni miongoni mwa wafanyakazi waliopunguzwa kazi na BoT mwaka 1993 wakati Serikali ikirekebisha uchumi, kwa kupunguza matumizi kulikoambatana na kupunguza watumishi, kazi ambayo Mahakama ilibaini ilifanywa bila ya kuzingatia sheria.
Akisikiliza maombi hayo jana, Jaji Semistodes Kaijage alitaka kufahamu kama kipengele cha 10 cha Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya 2000 kilichotumika kuyawasilisha kilikuwa kinaruhusu mahakama hiyo kusikiliza ombi hilo, lakini baada ya majadiliano na pande mbili, Wakili Mponda alikiri kuwa shauri hilo halifai kusikilizwa chini ya kifungu hicho.
Jaji Kaijage alisema ni lazima Mponda amridhishe kama kipengele cha sheria alichotumia kinawezesha mahakama kusikiliza ombi la kuongezewa muda ili BoT iweze kuwasilisha ombi la kuongezewa muda kuwasilisha taarifa ya kukata rufaa.
Wakili wa wafanyakazi 31 wa BoT, Barnaba Luguwa alimweleza Jaji Kaijage kuwa tatizo la upande wa BoT ni kung’ang’ania kanuni ya 10 badala ya kuangalia vipengele vingine vya sheria vinavyoweza kusaidia kumaliza mgogoro baina ya wateja wake na benki hiyo.

NECTA kuanza kukagua wenye Vyeti FEKI Kuanzia Kesho kwa Watumishi Wote

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Hatua ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.

Katika taarifa yake ya sasa Baraza la Mitihani nchini, limetangaza kuwafuata katika maeneo yao ya kazi watumishi wote walioko katika mamlaka za mikoa, halmashauri na manispaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa vyeti vyao hivyo vya kitaaluma.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na  Edga Kasuga kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwenda kwa Makatibu tawala wa Mikoa, uhakiki utafanyika katika ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 mwaka huu, ingawa ratiba nyingine ya uhakiki imeonyesha zoezi hilo litafikia tamati Novemba 7 mwaka huu.

“Ili kufanikisha zoezi hilo Baraza limetaka kupata orodha (nakala- laini ya soft copy) ya watumishi wote wa umma waliopo katika Mkoa, Halmashauri na Manispaa.

“Nakala za vyeti vya kidato cha nne, cha sita na ualimu vya watumishi wote walioandikishwa na chumba cha kufanyia uhakiki,” inaeleza taarifa hiyo ya Baraza la Mitihani.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani, uhakiki huo utafanywa katika makundi matano katika mikoa tofauti tofauti.

Oktoba 10, mwaka huu kundi la kwanza litafanya uhakiki katika Mkoa wa Mtwara, kundi la pili Singida, kundi la tatu Rukwa, kundi la nne Katavi na kundi la tano litakuwa Geita.

Oktoba 17 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Lindi, la pili Manyara la tatu Songwe, la nne Kigoma na la tano litakuwa Mwanza.

Oktoba 24 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Morogoro, la pili Arusha, la tatu Mbeya, la nne Tabora na la tano Mara.

Oktoba 31 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Pwani, la pili Kilimanjaro, tatu Ruvuma, la nne Shinyanga na la tano Simiyu.

Novemba 7 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Dar es Salaam, la pili Tanga, la tatu Njombe, la nne Dodoma na la tano Iringa.
==


WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUJIANDAA KWENDA KUFANYA KAZI KOKOTE NCHINI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini kuwa tayari kwenda kufanya kazi kokote watakalopangiwa na Serikali kulingana na mahitaji ya eneo husika.

Amesema moja ya wajibu wa watumishi wa umma ni kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania sehemu yoyote walipo ili kuwaletea maendeleo na atakayeshindwa ni vema akatafuta shughuli nyingine nje ya ajira za Serikali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana  jioni (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mkunguni wilayani Mafia.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

Waziri Mkuu alisema kila awamu inakuwa na mkakati wake, watumishi wa umma wanatakiwa kubadilika na kufanya kazi kutokana na awamu iliyoko madarakani inavyotaka

“Hii ni awamu ya kazi zaidi. Hata kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu! si neno la kufurahisha bali lina malengo yanayowataka Watanzania wote wafanye kazi,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mganga Mkuu wa mkoa wa Pwani, Dk. Beatrice Byarugaba kuimarisha huduma katika hospitali ya wilaya ya Mafia na kupeleka madaktari bingwa ili kuwapunguzia wananchi gharama za  kufuata huduma nje ya wilaya hiyo.

Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuimarishwa kwa kitengo cha (TEMESA) kwa kupeleka mafundi watakaomudu kufanya matengenezo ya magari wilayani huko ili kupunguza gharama za kusafirisha magari hadi makao makuu ya mkoa wa Pwani kwa matengenezo pale yanapohitaji matengenezo.

“Namna nyingine mnayoweza kufanya ni kuomba kibali maalumu cha kuruhusiwa kufanya matengenezo ya magari hayo kwenye karakana za watu binafsi zenye mafundi wenye sifa zinazotambulika na Serikali ili badala ya kuyapeleka Kibaha kwa matengenezo,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Ndikilo ameiomba Serikali kuipa kipaumbele hospitali ya wilaya hiyo yenye kuhudumia wananchi zaidi ya 50,000 ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa wataalamu, dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

“Kwa wilaya ya Mafia mgonjwa anapokosa dawa au vipimo maana yake aende Dar es Salaam au Rufuji au Mkuranga kufuata huduma hizo. Jambo hili linawagharimu sana wananchi hasa wa hali ya chini. Naiomba Serikali ituangalie  kwa jicho la huruma,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa alitaja changamoto nyingine inayowakabili wananchi wa wilaya hiyo kuwa ni usafiri wa majini kutokuwa na uhakika kutokana na kukosekana kwa meli rasmi ya abilia yenye usalama na staha.

Alisema kwa sasa wananchi wengi wanasafiri kwa kutumia majahazi na boti ndogo ambazo si salama na kwa sababu hiyo aliiomba Serikali kutafuta namna ya kutatua tatizo hilo linaloikabili wilaya hiyo kwa muda mrefu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi 469 katika kada za afya, elimu barabara, maji na utawala.

CHAMA CHA WAFANYAKAZI COTWU (T) KANDA YA DAR ES SALAAM CHAFANYA MKUTANO WAKE MKUU HOTELI YA VILA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kaimu Mkurugenzi, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Shanes Nungu (katikati), akihutubia wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mussa Mwakalinga na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine.
Wanawake waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanawake wajumbe wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano huo.
Vigogo wa chama hicho wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine, Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam wakiimba wimbo wa mshikamano katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.
Wajumbe wakionesha mshikamano wao wakati wakiimba wimbo maalumu wa mshikamano.
Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo akizungumza katika mkutano huo.
Makatibu wa matawi wa chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Tanzania (CMA), Shanes Nungu (wa tatu kushoto).
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)