HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

USIKOSE KUTAZAMA FILAMU YA KESHO YANGU NDANI YA STARTIME

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ijumaa ya tarehe 2 September 2016 kupitia chaneli ya Sibuka Maisha inayopatikana kwenye king'amuzi cha Startimes Tanzania itaanza kuonyesha filamu mpya ambayo inaitwa Kesho yangu. Filamu hiyo ni moja ya filamu mpya zitakazokuwa zikionyeshwa kabla ya kuingizwa sokoni kwenye mfumo wa DVDs. Filamu hiyo ya Kesho yangu Itaonekana kwa mara ya kwanza kupitia chaneli ya Sibuka Maisha kupitia king'amuzi cha Startimes Tanzania.

VIDEO: MADUKA KIBAO YA FILAMU KARIAKOO YAFUNGWA, TRA YATAKA MIKATABA YA USAMBAZAJI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Maduka mengi yanayouza filamu katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, yamefungwa baada ya mamlaka ya mapato Tanzania, TRA kuwataka wamiliki waoneshe mikataba ya usambazaji wa filamu hizo za nje.

Filamu hizo zinadaiwa kutolipiwa ushuru. Kwa mujibu taarifa ya Channel 10, baadhi ya maduka yamefunguliwa nusu huku wamiliki wakifanya biashara kwa kuibia.

Wafanyabiashara hao wamejitetea kuwa hawana mikataba ya usambazaji na kwamba filamu hizo zinapoingia nchini zinakuwa zimeshalipiwa ushuru.
Wakiongea kwenye mkutano na maafisa wa serikali, wafanyabiashara hao wamedai kuwa takriban maduka 40 yamefungwa. Wamesema kuwa suala la kuwa na mikataba na wamiliki wa filamu hizo ni kitu kisichotekelezeka.

SERIKALI YAFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MASHIRIKISHO YA FILAMU NCHINI.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kaimu Mkurgenzi, Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akiongea na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya sekta ya sanaa nchini wakati alipokutana nao hivi karibuni Wizarani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo. 
Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akisistiza jambo mbele ya baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya sekta ya sanaa nchini wakati wa kikao hicho Wizarani hapo jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Bw. Simon Mwakifwamba akieleza jambo mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu masuala ya sanaa nchini wakati wa kikao hicho Wizarani hapo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania wakichangia mada kuhusu maendeleo ya sekya ta Sanaa nchini wakati wa Kikao na Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa upande wa Sekta ya Sanaa kilichofanyika hivi karibuni Wizarani hapo. 

(Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu nchini ikiwa ni sehemu ya kubaini changamoto mbalimbali zinazoyakabili Mashirikisho hayo.

Akiongea hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi alisema kwamba, Mashirikisho yanayounda Shirikisho la Filamu nchini hayanabudi kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kubaini changamoto na namna ya kuzitatua kwa manufaa ya Wasanii na Taifa kwa ujumla.

Alieeleza kuwa, Wasanii wanapaswa kuzingatia maadili wakati wanapofanya kazi zao za sanaa ili waweze kujijengea heshima kwao, kwa jamii ambayo ndio mlaji wa kazi zao za kisanaa na kwa Taifa kwa ujumla.

“Mnapofanya kazi zenu za sanaa, jitahidini kufuata miiko ya kazi zenu, tumieni vipaji vyenu vizuri kwa kufuata maadili ya Kitanzania, lakini pia jitahidini kuwainua wale wasanii wanaochipukia ama wale wadogo ili waweze kuwa na hamasa ya kuendeleza kazi zao za sanaa”, alisema, Bi. Kihimbi.

Bi. Kihimbi aligusia suala la fursa ya kazi za sanaa inayodhaminiwa na Taasisi ya British Council Tanzania na kuwataka wasanii kuchangamkia fursa hiyo kwa kuhakikisha kuwa kila msanii au kikundi kinaandika Pendekezo (Proposal) kuhusu fursa hiyo ili kujiwekea nafasi kubwa kwa wasanii wa Tanzania kushinda fursa hiyo na kuweza kupata fedha za kuendesha kazi za sanaa kulingana na wazo lililobuniwa.

“Kuweni wabunifu katika hii fursa ili mje na wazo zuri ambalo litawawezesha kushinda hii fursa hasa hii ya nAnA (new Arts new Audiences) kwani inamhusu msanii mmoja mmoja au kikundi”, alisema, Bi. Kihimbi.

Aliongeza kuwa, Serikali itajitahidi kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaonekana kuwa kero kwa wasanii nchini ikiwemo suala la wizi wa kazi za sanaa (Piracy) ambalo kwa sasa tayari Waziri mwenye dhamana katika Wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye ameonyesha mfano kwa kukamata DVDs feki pamoja na mitambo ikiyotumika kudurufu kazi hizo za sanaa nchini.

Kwa upande wake, Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alisema kwamba Bodi yake inashirikiana vema na wasanii nchini kwa kuzingatia Sheria za nchi pasipo kumuonea msanii yeyote na kuwataka wasanii kote kuendeleza uhusiano huo mzuri uliopo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Aidha, aliwataka viongozi wa Shirikisho hilo la Sanaa kuendelea na utaratibu wa kupeana taarifa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sanaa na kuwahimiza wasanii kupenda kujiendeleza kielimu ili waweze kumudu soko huku akiwasisitiza kuhakikisha kuwa kazi zao wanazotengeneza zinapata kibali cha Bodi kwa kuwekewa madaraja na zinakuwa na stika halali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuepusha uharamia wa kazi zao.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Bw. Simon Mwakifwamba ameiomba Serikali kuendelea kushirikiana na Wasanii kwa karibu kwa kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo na ikiwemo suala la uharakishaji wa Sera ya Filamu kwani ndiyo kipaumbele chao cha kwanza, elimu ya namna ya kutengeneza filamu bora, usambazaji wa kazi zao pamoja na adui yao mkubwa ambaye ni uharamia wa kazi za sanaa.

Ameishukuru Serikali kwa kuunda Sekta mpya ya Sanaa na kusema kuwa, Sekta hiyo itakuwa Mkombozi kwao kwani wanajisikia fahari kutambuliwa na kuwa na kitengo chao cha masuala ya kazi zao huku akiaahidi ushirikiano mzuri kwa sekta hiyo.

MSAMA AFICHUA MTANDAO WA WIZI WA STIKA ZA TRA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi wa Msama Action Mart, Alex Msama akionesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, stika za TRA pamoja na CD feki ya mwimbaji wa nyimbo za injili Boniphace Mwaitege wakati wa mkutano na wambayo ni 'feki' lakini imewekwa stika ya TRA. (Na Mpigapicha Wetu)

NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI wa Msama Action Mart ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama amewalaumu baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhujumu mapato halali ya waimbaji, wasanii na Serikali.

Msama alisema jijini Dar es Salaam jana kwamba, baadhi ya maofisa hao wa TRA, wamekuwa wakiuza ‘stika’ kwa wezi wa kazi wa waimbaji na wasanii ili ‘kutakatisha’ kazi za wizi.

“Unakamata CD feki, lakini unakuta ina ‘stika’ ya TRA. Unajiuliza inakuweje?  Yote hii ni kutokana na baadhi ya maofisa wa TRA kuuza ‘stika’ hizi isivyohalali kwa wezi,” alisema huku akionesha mfano wa stika halali na CD feki.
Msama, mmoja wa wadau wa vita dhidi ya wizi wa kazi za waimbaji injili na wasanii, alisema wanachofanya wezi  ni kubandika ‘stika’ halali katika kazi feki  na kuziuza.

“Hawa jamaa wamebuni mbinu mpya ya kutumia stika halali za TRA katika kazi feki, jambo ambalo linahitaji uzoefu kubaini kwamba ni feki,” alisema Msama.

Alisema hujuma hiyo dhidi ya jasho la waimbaji na wasanii, imekuwa ikiwanyima wahusika kufaidi jasho la kazi zao kwani huishia kwa wajanja hao wachache.
“Kama si dili ya baadhi ya maofisa wasio waaminifu wa TRA, wezi hawa wangepata wapi stika hizo? alihoji Msama huku akionyesha stika halali
za TRA na CD feki.

Alisema kibaya zaidi ni kwamba, stika hizo feki hazitumiki kwa kazi hizo feki za waimbaji na wasanii, pia hata kwa bidhaa nyingine ili kuzihalalisha.

Msama anatoa wito kwa jamii kusaidia vita hiyo ngumu kwa kuacha kununua kazi feki ili kuinua uchumi wa wasanii na nchi kwa ujumla.

Alisema vitendo hivyo vya baadhi ya maofisa wasio na uadilifu, vinarudisha nyuma harakati za Serikali kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Msama ametoa wito kwa uongozi wa TRA kufanya kila uwezalo kuwabaini maofisa hao wenye kukiuka maadili ya kazi yao kwani wanakipaka matope chombo hicho.

BODI YA FILAMU YATOA MSAADA KWA WAKONTA ALIYEPOOZA MWILI MZIMA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Wakonta Kapunda akimshukuru Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo kwa msaada wa shilingi laki 5 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akikabidhi msaada wa shillingi laki 5 kwa Wakonta Kapunda Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM).