HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Wake Wanyimwa Dhamana na Kurudishwa Rumande

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana kwa kesi inayowakabili, wamerudishwa rumande mpaka Julai 17 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria dhidi ya mawakili wa utetezi na mawakili upande wa jamhuri (serikali).

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti

MCHEZAJI WAZAMANI WATIMU YA TANZANIA ‘TAIFA STARS’, MOHAMMED MSOMALI AFARIKI JAMAL MALINZI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro (MRFA), Paschal Kihanga kutokana na kifo cha Kocha na mchezaji mahiri wa zamani wa Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mohammed Msomali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka MRFA, Kocha Mohammed Msomali ambaye anaweza kuelezwa kuwa ‘gwiji’ la kandanda la Tanzania, alifikwa na umauti Septemba 08, 2016 saa saba mchana akiwa nyumbani kwake akisubiri kupata mlo wa mchana. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74.
Taarifa za awali zinaeleza siku mbili zilizopita, Kocha Msomali alilalamika kuugua kifua na kwamba baada ya kupata tiba mchana, alijipumzisha akisubiri kupata mlo wa mchana, lakini walipokwenda kumwamsha, alikutwa amefariki dunia. 
Anatarajiwa kuzikwa kesho Septemba 09, 2016 saa 7 mchana mara baada ya swala Ijumaa.
Mbali ya salamu hizo kwenda MRFA, Rais Malinzi pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Msomali, ndugu, jamaa na marafiki huku akiwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wao.

Katika nafasi za uchezaji, historia inaonesha kuwa Msomali nyota yake ilianza kuonekana kwenye timu mahiri ya Cosmopolitan ya Dar es Salaam kabla ya kuchezea klabu nyingine za Young Africans pia ya Dar es Salaam, Mseto ya Morogoro, Timu ya Mkoa wa Morogoro ‘Moro Stars’ na Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kadhalika timu ya Bara ambayo ni maarufu kwa jina la Kilimanjaro Stars.
Wakati wa uhai wake, Msomali amepata kuzifundisha Mseto na Tumbaku za Morogoro ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (Klabu Bingwa Tanzania) mwaka 1975. Pia alizinoa Young Africans, Timu ya Mkoa wa Morogoro ‘Moro Stars’ na kwa muda mrefu timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ sambamba na ile ya Bara ambayo ni maarufu kwa jina la Kilimanjaro Stars.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee Mohammed Msomali mahala pema peponi.
Innalillah Wainnailaihi Raajiuun – Hakika sisi ni wa Mungu, na kwake tutarejea.

JAMAL MALINZI AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS MPYA WA (EFA) HANI ABOU-REIDA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Hani Abou-Reida kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri (EFA) katika uchaguzu mkuu uliofanyika juzi Jumanne Agosti 30, 2016 jijini Cairo.

Katika salamu zake, Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa Hani Abou-Reida katika wadhifa huo ni kilelelezo cha familia ya mpira wa miguu ya Misri kuona umuhimu wake katika kutumikia shirikishi hilo sambamba na kuwa mwakilishi FIFA.
Rais Malinzi amesema ana imani na Abou-Reida kuwa ataweza kutumikia vema nafasi hiyo sambamba na kutumikia wadhifa wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Abou-Reida (63) ni mjumbe wa FIFA kutoka Kanda ya Afrika Kaskazini tangu mwaka 2009 na sasa ataongoza shirikisho la EFA kwa awamu ya kwanza kwa miaka minne ijayo akichukua nafasi ya Galam Allam aliyeongoza EFA tangu mwaka 2012.

Katika uchaguzi huo, wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa EFA waliochaguliwa ni pamoja na wale wenye majina maarufu kama vile Hazem Emam ambaye alikuwa nyota mahiri wa klabu ya Zamalek sambamba na kiungo mkabaji mahiri wa zamani wa klabu ya Al- Ahly. Nyota hao pia walipata kuchezea timu ya taifa maarufu kwa jina la Pharaohs.
Pia wamo Sahar El-Hawary, Hazem El-Hawary, Karam Kordi, Khaled Latif, Seif Zaher, Mohammed Aboud El-Wafa, Ahmed Megahed a

MALINZI AWEKWA KATI NA BMT

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Rais wa TFF Jamal Malinzi

Baraza la Michezo Tanzania (BMT) lipo katika mchakato wa kutaka kujiridhisha juu ya tukio la Rais wa TFF Jamal Malinzi kuamua kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera wakati akiwa bado ni kiongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF).

Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amethibitisha taarifa hiyo: “Tunaangalia katiba zao zinasemaje kwanza, kwasababu sasahivi bado tunaangalia historia kwakua viongozi waliopita hawakufanya hivi. Sijaiona katiba ya chama alichogombea kule (Kagera) nikijiridhisha nitatoa majibu.”

Kama BMT itajiridhisha kwamba Malinzi amegombea kwa mujibu wakanuni na taratibu, basi atakuwa salama, lakini kama atakuwa nje ya katiba basi BMT itajua nini cha kufanya.