HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MASAUNI AFUNGUA GEREZA LA WANAWAKE MPWAPWA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akishirikiana na Viongozi wengine kufungua Gereza  la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa  kushirikiana na wafungwa.Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mheshimiwa George Lubeleje , akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,Mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia), akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa (kulia) kuelekea katika eneo lilipo  Gereza la Wanawake Mpwapwa, lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Wananchi wa Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni  askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu, MOHA
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi ya askari  wa jeshi hilo hapanchini.
Akizungumzia changamoto za Makazi ya askari wa Jeshi la  Magereza Nchini, wakati wa uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema Serikali inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.
“Nawaomba  askari wetu nchi nzima  wawe na subira  Serikali inatambua na  inashughulikia changamoto ya makazi ya  askari na tayari tuko katika mazungumzo na wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 9500, lengo ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na familia zao,” alisema Masauni.
Awali akitoa maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu ambao ni askari Magereza kwa  kushirikiana na wafungwa kama sehemu ya utekelezaji wa  amri ya Mh. Rais Dk. John Magufuli ya kutaka wafungwa watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo kilimo,ujenzi na ufundi mbalimbali.
Ujenzi wa Gereza hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia  kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la Kongwa mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa  ndugu wa wafungwa kusafiri mpaka wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.

WAZIRI MKUU AAGIZA MAENEO YA MAGEREZA YAPIMWE

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiongoza  kikao  kati yake na  Maofisa wa Magereza kutoka makao Makuu ya Magereza , pamoja na Makamanda wa Magereza wa Mikoa  yote nchini, ofisini kwake  mjini Dodoma  Februari 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri  MKuu)
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa  Jeshi la Magereza Wanawake  baada ya kikao  chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma   Februari 13,2017.   Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mwigulu Nchemba. 
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watalaamu na Wasimamizi wa Mkiradi ya Jeshi la Mgereza, baada ya kikao  chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza  na Wakuu wa Magereza wa Mikoa kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma   Februari 13,2017.    Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. 
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa  akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Magereza,  Dr Juma Malewa baada ya kikao  chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma   Februari 13,2017.   Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani Meja Jenerali  Projest  Rwegasira. 
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa  akisalimiana na Kamishina Mwandamizi  wa Magereza na Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi, Tusikile Mwaisabira baada ya kikao  chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza  na  Maofisa Magereza wa Mikoa, kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma   Februari 13,2017.

*Ataka karakana za ujenzi, useremala zianzishwe kupunguza gharama
*Asisitiza ufyatuaji matofali kukabili upungufu wa nyumba za askari

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa asimamie zoezi la upimaji wa maeneo yanayomilikiwa na Magereza kote nchini na kuhakikisha yanawekewa mipaka.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatatu, Februari 13, 2017) katika kikao baina ya Kamishna huyo mpya na Maafisa Magereza wa Mikoa yote na maafisa wanaoshughulikia kilimo na viwanda alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma.

“Magereza yetu mengi yako kwenye maeneo ambayo hayajapimwa. Baadhi ya maeneo kuna migogoro kwa sababu wananchi wamejenga karibu kabisa na maeneo ya Magereza. Lazima tupime maeneo yote na kuyawekea alama mipakani ili kubainisha maeneo yetu,” amesisitiza.

Mbali ya maeneo ya Magereza, Waziri Mkuu amesema, jeshi hilo lina mashamba makubwa ambayo pia hayajapimwa hali ambayo amesema imechangia baadhi ya wananchi kulima ndani ya maeneo ya jeshi hilo.

“Natambua kuwa jeshi hili lina mashamba makubwa lakini nayo pia hayajapimwa. Kila RPO ni mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake, tumieni wapima ardhi kutoka kwenye Halmashauri zenu na mhakikishe kuwa maeneo hayo yanapatiwa hati,” amesema.

Amesema umefika wakati sasa kila gereza litambue na kuainisha fursa walizonazo ili waweze kuamua ni kwa kiasi gani wanaweza kujitegemea kwa uzalishaji. “Kama ni kilimo, ufugaji, au uzalishaji wa umeme, tuangalie ni kipi kinaweza kuvutia uwekezaji, lakini cha msingi zaidi ni lazima tuwe na hati za maeneo tuliyonayo,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kuna baadhi ya magereza yalikuwa maarufu kwa kilimo lakini hivi sasa hakuna hata moja lenye trekta na kama yapo ni moja au mawili tu. “Sasa hivi teknolojia ya kilimo imebadilika, ni lazima tutumie zana za kilimo ili kwenda na kilimo cha kisasa.

Akizungumzia kuhusu ufugaji na uvuvi wa samaki, Waziri Mkuu aliagiza jeshi hilo litumie maafisa wake waliobobea kwenye sekta hizo, watumike kuendeleza na kuhamisha ujuzi wao kwa wafungwa wanaotumikia vifungo ili wanapotoka gerezani, wawe na ujuzi ambao utawasaidia kujikimu kimaisha wanaporudi kuishi vijijini.

“Nimetembelea maonesho ya Nanenane na Sabasaba huko nimekuta wamejenga banda la kuku juu ya bwawa la samaki. Hii ina maana kuku wanakula na kinyesi chao kinakuwa ni chakula kwa wale samaki walioko bwawani,” amesema.

Amemtaka Dk. Malewa aangalie uwezekano wa kuanzisha karakana na ujenzi kwenye kila gereza ili maafisa na wafungwa waliopo kule watumike kufanya kazi kwenye karakana hizo. “Nimetembelea gereza la Isanga, nikakuta kuna milango haina komeo. Kwa vile hakuna karakana, inabidi atafutwe fundi kutoka mtaani ili aje kutengeneza kitasa au komeo. Tuanzishe karakana na tuziboreshe,” amesisitiza.

Amesema uwepo wa karakana hizo ziwe ni za umeme, ujenzi au useremala, utasaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwa jeshi la magereza kwa matengenezo madogo madogo yatafanywa na watu wa kwenye karakana badala ya kutumia watu wa nje.

Amesema ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za askari, kila afisa magareza wa mkoa hana budi kuandaa matofali ya kutoka kwani timu za wafyatuaji wanazo na nguvukazi wanayo pia.

“Badala ya kutegemea wazabuni, kule kwenye udongo mzuri, tafuteni vifaa mfyatue matofali ya hydraform. Kule kwenye mchanga, fyatueni ya saruji. Kuweni na matofali ya kutosha kulingana na mahitaji yenu, mtakuwa mmepunguza gharama za ujenzi wa nyumba za askari kwa kiasi kikubwa,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu huyo, Dk. Malewa amesema atafuatilia suala la upimaji wa maeneo ya magereza kwa sababu wanao wapimaji na vifaa wanavyo. Amesema kuna magareza 11 yenye migogoro ya maeneo na wananchi.

“Pia tutafuatilia upimaji wa maeneo ya mashamba ya magereza. Tumeanzisha mashamba makubwa ya kilimo na tutahakikisha maeneo hayo yote yanapimwa na kuwekewa alama za mipaka,” amesema.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mwigulu Nchemba; Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. William Tate Ole Nasha; Kamishna Jenerali wa Magereza, Makatibu Wakuu wa Wizara ya Kilimo wanaoshughulikia Kilimo na Mifugo pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATATU, FEBRUARI 13, 2017.

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA GEREZA LA RUANDA JIJINI MBEYA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Magereza jijini Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida (kulia) wakati alipowasili kukagua shughuli za uzalishaji thamani za ndani na sabuni katika gereza la Ruanda .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Mkuu wa Kiwanda cha Gereza la Ruanda ASP Michael Kuga, akisoma taarifa ya hali ya uzalishaji wa sabuni na thamani za ndani mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo zinazofanyika katika magereza yaliyopo jijini Mbeya.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akipata maelezo juu ya utengenezwaji wa kiti kinachotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kulia waliokaa), akiangalia picha za  thamani za ndani zinazotengenezwa na wafungwa wa Gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wengine waliokaa baada ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Kiwanda hicho,ASP Michael Kuga ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Jesuald Ikonko  na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi. 
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza alipotembelea Kiwanda cha sabuni zinazotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wanaomsikiliza ni Mkuu wa Kiwanda() na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiangalia moja ya sabuni zinazozalishwa na wafungwa wa Gereza la Luanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho().Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWIGULU NCHEMBA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA KIKOSI MAALUM CHA MAGEREZA JIJINI DAR

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb)  akipokea Salaam ya heshima kutoka Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11. Hafla ya hiyo imefanyika leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Dkt. Juma Malewa .
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akikagua Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na Askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kama inavyoonekana katika picha.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimtunuku cheti cha sifa Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 ambapo Mafunzo hayo yamefungwa rasmi leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimvisha nembo ya kijani Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kwa niaba ya wahitimu wenzake. Mafunzo hayo Maalum yamefungwa rasmi leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kabla ya kuyafunga rasmi leo Januari 13, 2017.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo hayo.
 Askari Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 wakiingia uwanjani kwa ajili ya kutoa maonesho mbalimbali ya Ukakamavu na ujasiri.
   Onesho Maalum la Ukakamavu na ujasiri kama inavyoonekana katika picha Askari wa Kikosi Maalum akihimiri kipigo cha nyundo katika mwili wake kwa ujasiri wa hali ya juu.
 Askari Wahitimu wa Mafunzo hayo Maalum wakionesha umahiri wao wa kuvuka vikwazo mbalimbali kwa kutumia kamba kama inavyoonekana katika picha.
Wahitimu wa Mafunzo Maalum wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Jeshi la Magereza).