HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

PICHA: KOREA KASKAZINI YAWACHIMBA MKWARA MAADUI ZAKE KWA KUONESHA SILAHA NZITO



Korea Kaskazini imetoa onyo kwa maadui zake Jumamosi hii kwa kuonesha silaha zake mpya na nzito kwenye gwaride la kijeshi mbele ya kiongozi wake.
Pyongyang imeonesha silaha zake kadhaa kwa mara ya kwanza zikiwemo zile za kutumika chini ya maji.
Hiyo ni ishara kuwa inaweza kuishambulia Marekani au Ulaya bila shida.
Hatua hiyo imekuja katika kipindi ambacho Rais wa Marekani, Donald Trump amekuwa akitweet kuwa kama China haiwezi kukabiliana na mpango wa silaha za nyuklia wa Korea Kusini Marekani itainunua kesi.
Pia utawala wa nchi hiyo umeionya Marekani dhidi ya mashambulio yoyote inayopanga kufanya dhidi yake.
Gwaride hilo limefanyika kusherehekea miaka 105 ya kuzaliwa kwa babu yake Kim. 
Kim anamshutumu Trump kulichokonoa taifa lake kijeshi kwa mfululizo wa nyendo za kibabe ikiwemo kutuma meli kubwa ya USS Carl Vinson kwenye peninsula ya Korea.



  
  

MIILI YA ASKARI NANE WALIOUAWA NA MAJAMBAZI MKOANI PWANI YAAGWA RASMI,WAZIRI MWIGULU ATANGAZA KIAMA KWA WATUHUMIWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa heshima za mwisho Dar es Salaam mbele ya majeneza yenye miili ya askari nane waliouawa na majambazi Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani juzi jioni.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Masauni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa pole kwa wafiwa.
Ndugu,jamaa na marafiki wa wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya wapendwa wao.
Maofisa wa Uhamiaji wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Wananchi wakiwa katika shughuli hiyo ya uagaji wa miili hiyo.
Maofisa wa Polisi wakishiriki kuaga miili ya wenzao hao.
Foleni ya kuaga miili hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu wakati wa kuaga miili hiyo.
Mmoja wa ndugu za askari hao akilia kwa uchungu.






Ni kilio kwa kuwapoteza wapendwa wao.
Ni huzuni.


Na Dotto Mwaibale 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga mkoani 
Pwani.

Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam Mwigulu alisema watu hao watakamatwa  wote na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

"Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata" alisema Mwigulu.

Aliwaomba wananchi wa maeneo husika kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwapata wahusika wa tukio hilo.

Katika hatua nyingine Mwigulu ameitaka wizara husika kuhakikisha inatoa fidia kwa ndugu wa askari hao na majeruhi badala ya kuchukua muda mrefu kuitoa.

"Naomba fidia kwa askari hawa tuliowapoteza wakitumikia taifa itolewa haraka bila kucheleweshwa" aliongeza Mwigulu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu alisema watuhumiwa wote waliohusika kufanya mauaji hayo ni lazima watafikiwa na mkono wa dola.

Alisema wananchi wa eneo hilo wanawafahamu wahusika hivyo amewaomba washirikiane na polisi ili kuwapata vinginevyo nguvu itatumika.

Alisema linapotokea tukio kama hilo kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishabikia kupitia mitandao ya kijamii hivyo akatoa onyo kuwa watakao bainika na wao watakamatwa kwa kutenda kosa.

Askari waliopoteza maisha katika tukio hilo la kinyama wametajwa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub


BUNDUKI KUMI ZIKIWEMO SMG SITA RISASI 59 ZAKAMATWA ARUSHA

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kupata jumla ya bunduki kumi za aina nne tofauti zikiwemo Sub-Machine Gun sita baada ya operesheni ya wiki mbili iliyoanza tarehe 15.02.2017 katika wilaya ya Ngorongoro. 

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema silaha hizo zilipatikana katika vijiji vya Olorieni Magaiduru, Oldonyosambu na Sale vilivyopo katika tarafa za Loliondo na Sale.

Alisema mafanikio hayo yalitokana na taarifa fiche ambazo zilibainisha kwamba kuna baadhi ya watu wanamiliki silaha za kivita hivyo mahojiano makali baina ya askari wa Jeshi la Polisi na Viongozi wa Kimila na kuwataka wasalimishe silaha popote pale ambapo walikuwa wanaamini kwamba silaha hizo zitawafikia Jeshi la Polisi.

Akibainisha vijiji ambavyo silaha hizo zilipatikana kuwa ni Olorieni Magaiduru zilipatikana silaha aina ya Chinese 56 SMG moja yenye namba MT. 70B 1 2730021 na risasi 21 pamoja na silaha aina ya Semi Automatic Rifle (S.A.R) yenye namba KN 250374 ikiwa na risasi nne.

Katika kijiji cha Oldonyasambu ilipatikana silaha aina ya Mark IV yenye namba ZKK 5602 pamoja na silaha nne aina ya Chinese 56 Sub-Machine Gun (SMG) zikiwa na risasi 19. Silaha hizo nne ni Chinese 56 SMG yenye namba RT 7663, bunduki ya pili namba yake ni 563631144 na bunduki mbili nyingine hazikuwa na namba.

Kamanda Mkumbo alisema katika kijiji cha Sale silaha aina ya Chinese 56 SMG yenye namba 89020539 ikiwa na risasi 15 kwenye magazine ilipatikana pamoja na silaha nyingine mbili tofauti ambazo ni S.A.R yenye namba 25032534 na Mark III yenye namba 263126.

Aidha kamanda Mkumbo aliwataka wananchi wanaomiliki silaha za moto kinyume cha sheria wazisalimishe mara moja kwenye ofisi za mitaa, vijiji na hata vituo vya Polisi vyovyote vilichopo karibu huku akitoa onyo kwa wale ambao watakaidi na wakikutwa nazo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Alisema Operesheni hiyo ni endelevu na itakuwa katika maeneo tofauti ya mkoa huu na si wilaya ya Ngorongoro pekee.
 Silaha mbalimbali zikiwemo SMG 6 pamoja na risasi 59 zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika katika wilaya ya Ngorongoro.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo akionyesha silaha mbalimbali zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro iliyofanyika wiki mbili zilizopita.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionesha waandishi wa habari baadhi ya silaha  zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha akiwaonesha waandishi wa habari moja ya silaha ya kivita aina ya Chinese 56 Sub Machine Gun (SMG) iliyopatikana kwenye operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro.

RAIS DKT MAGUFULI AMTEUA MKUU WA MAJESHI

Luteni Jenerali Venance Mabeyo ambaye ameteuliwa na Rais Dkt Magufuli kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO WA JESHI LA PILISI,NSATO MARIJANI AWAFARIJI ASKARI WALIOPOTEZA MALI ZAO KWA TUKIO LA MOTO MJINI MOSHI.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.
Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo..
Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao.
Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.
Kamishna Marijani akita pole kwa PC  Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo.
Kamishna Marijani akimfariji  CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea athari iliyotokana na moto huo.
Kamishna Marinaji akimpa pole SGT Hashim baada ya kupoteza vitu vyote vya ndani pamoja na mavazi kufuatia moto ulioteketeza seheumu ya juu ya jengo hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuongoza Kamishna Marijani kukagua maeneo mengine  ya jengo hilo ambalo linakumbwa na tukio la moto kwa mara ya pili sasa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi ,Nsato Marijani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kutoa pole kwa asakri waliounguliwa vitu katika jengo hilo.
Waliovalia kiraia ni askari Polisi waliofikwa na janga la kuunguliwa moto vitu vya ndani pamoja na mavazi wakionekana wenye huzuni.
Afisa Mnadhimu daraja la kwanza wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani alipotembelea kambi ya polisi mjini Moshi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa juu ya tukio la moto katika jengo la makazi ya askari Polisi.
Baadhi ya wanandugu wa familia zilizounguliwa moto wakionekaa wenye huzuni.
Mkuu wa Shule ya Polisi,Kamandanti Matanga Mbushi akizungumza wakati wa kuzifariji familia za askari waliopoteza vitu vyao katika tukio la moto.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisni nchini ,IGP Ernest Mangu kwa askari waliopoteza vitu vyao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa katika makazi ya askari Polisi mjini Moshi.
Mmoja wa wageni waalikwa akizungumza wakati akitoa salamu za pole kwa jeshi la polisi. 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi nchini limetangaza kuwahamisha askari tisa wa vikosi mbalimbali vya jeshi hilo waliopoteza mali zao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa vya jengo la ghorofa mbili ambalo ni makazi ya askari.

Mbali na hatua hiyo jeshi hilo pia limetoa kiasi cha Sh Milioni tisa kwa familia za askari hao kwa ajili ya kuanza kununua vitu vidogo yakiwemo mavazi baada ya kutoambulia chochote wakati wa tukio hilo zikiwemo sare za jeshi hilo.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani ametoa kauli hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisi ,Inspekta Jenerali,Ernest Mangu wakati akizifariji familia za askari hao pamoja na kutembelea jengo lililoteketea kujionea athari za moto huo uliotokea usiku wa kuamkia juzi.

Akiwasilisha salamu za Pole kwa niaba ya IGP Mangu,Kamishna Marijani alisema jeshi la Polisi litaendelea kutoa msaada kwa askari hao hadi pale maisha yao yatakaporejea huku akivishukuru vikosi vya jeshi la zima moto vya uwanja wa ndege wa KIA,kiwanda cha sukari cha TPC na Halmashauri kwa kazi waliyofanya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa amemwelea kamishna Nsato kuwa thamani ya mali za askari zilizoteketea kwa moto imefikia sh Mil 93.9 huku akiomba wadau kujitokeza kusaidia familia hizo.

Tukio la moto katika jengo hilo lililopo jirani na ofisi za kikosi cha kutuliza ghasia lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 2:30 usiku ,ukianzia katika chumba kimojawapo cha ghorofa ya pili na kuenea katika vyumba vingine nane wakati huo umeme ukiwa umekatika.

Kufuatia moto huo familia tisa za askari hao zenye jumla ya watu 40, ambao 23 ni watu wazima na 17 ni watoto tayari zimepatiwa malazi ya muda katika chuo cha Polisi Moshi wakati taratibu nyingine za kuwasaidia zikiendelea.

Tayari jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limeunda timu ya wataalamu kutoka katika jeshi hilo wakisaidiana na wale wa kikosi cha zimamoto pamoja na shirika la umeme (TANESCO) kufanya uchunguzi wa matukio ya moto katika jengo hilo.