HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

KLINIKI YA AFYA YA AKILI KUTOLEWA KUPITIA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA NCHINI- DK.KIGWANGALLA

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni mjini Dodoma.

Kliniki ya Afya ya Akili kutolewa kupitia Hospitali zote za Rufaa nchini- Dk.Kigwangalla Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla amekutana na viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni Dodoma. 
Viongozi hao walikaribishwa na Wabunge wawakilishi wa Watu wenye changamoto mbali mbali za ulemavu nchini, Mhe. Amina Mollel (Mb.) na Mhe. Stella Ikupa (Mb.). Katika kikao hicho Dkt. Kigwangalla ameweza kujadiliana nao mambo mbalimbali viongozi hao wa TUSPO ikiwemo uanzishwaji wa Kliniki ya Afya ya Akili kupitia Hospitali zote za Rufaa za Mkoa hapa nchini. 

“Nimekutana na Viongozi wa TUSPO ambao wanashughulika na masuala ya Afya ya Akili. Tulijadili mambo mengi na niliwaelezea mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwenye eneo hili, ikiwemo Uanzishwaji wa Kliniki za Afya ya Akili kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mkoa nchini nzima. Lakini pia Uanzishwaji wa Rehabilitation Centers kwenye kila kanda na usambazaji wa Madaktari bingwa wa Afya ya Akili na wataalamu wote wanaohitajika kutoa huduma hizi kwenye Hospitali na vituo hivi” 

Ameeleza Dkt. Kigwangalla. Aidha, ameongeza kuwa, amewaahidi uongozi huo wa TUSPO, kuwa atafuatilia juu ya hatua ambayo mchakato wa kukamilisha muundo wa kisheria (legal framework) ulipofikia na sababu za kukwama kwake toka sheria ya afya ya akili ilipotungwa mwaka 2008. “Serikali ya awamu ya tano ni sikivu kwa wananchi wake bila kubagua. 

Nina aahidi kulifuatilia sualala uanzishwaji wa Baraza la Afya ya Akili, kwani tayari sheria ilishatungwa muda mrefu. Na kwamba ni kwa nini Baraza la Afya ya akili halijaanzishwa toka sheria itungwe mpaka leo na kwa nini mpaka leo hakujawa na kanuni za Afya ya akili kuelekeza juu ya mambo mbalimbali” alieleza Dkt. Kigwangalla ambapo amewaahidi kuwapa taarifa ya utekelezaji wa masuala hayo kwenye Bunge la Mwezi November 2017.

Kuhusu Magonjwa ya Akili: Magonjwa ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na tabia au mwenendo uliotofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine za kijamii. 

Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi na shughuli za mtu husika (mgonjwa) au huathiri jamii nzima inayomzunguka endapo mgonjwa huyo hatopatiwa matibabu stahiki na kwa wakati muafaka. Kwa Tanzania imeeelezwa kuwa baadhi ya wagonjwa wengi wa akili hawafiki katika vituo vya kutolea huduma za afya na badala yake kuishia kwenye tiba za jadi au kutelekezwa na kunyanyapaliwa huku takwimu za zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu takriban milioni 45 na kutokana na taarifa ya afya ya akili kwa mwaka 2014/15 inaonyesha kuwa idadi ya watu 817,532 wanaugua magonjwa mbalimbali ya akili nchini, hii ni karibu asilimia 2 ya watanzania wote.

 Pia idadi hii ni ongezeko la wagonjwa 367,532 ukilinganisha na takwimu za mwaka 2013/14 walikuwa ni 450,000. Kati ya wagonjwa wote wa akili kwa mwaka 2014/15 wanawake ni ni 332,000 na wanaume ni 485,532. Mkoa wa Dar-Es-Salaam unaongoza kwa kuwa n awagonjwa wengi nchini ukifuatiwa na mkoa wa Dodoma na mkoa wa mwisho ni Lindi. Idadi hiyo ya wagonjwa ni wale walioweza kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla (mwenye koti nyeusi kulia) akifanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni mjini Dodoma.

“HALI YA DAWA NCHINI IMEIMARIKA”-MHE.KIGWANGALLA

  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya upatikanaji wa Dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja mbalimbali za Wabunge leo Mjini Dodoma.

“Moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma nchini”Alisema Mhe.Kigwangalla.

Amesema kuwa katika kutekeleza azma hii Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia bilioni 251,500,000,000 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Aidha hadi kufikia Mwezi April 2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.

Kufuatia Ongezeko ilo la fedha kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika sana.

“Hadi kufikia tarehe 15 Januari 2017,Mkoa wa Kagera pekee umepokea kiasi cha bilioni 4,150,767,216 kupitia fungu 52 kwa ajili ya kununulia dawa,vifaa,vifaa tiba na vitendanishi.”Aliongeza Mhe.Kingwangalla.

NAIBU WAZIRI WA AFYA KUWEKA HADHARANI MAJINA YA MASHOGA DAR ES SALAAM

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa atawaweka hadharani wanaume wote wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja (mashoga) ambao hufanya biashara hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
 
Naibu Waziri aliyasema hao jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alieleza kuwa yupo katika ziara jimboni kwake na mara atakaporejea jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma rasmi ataiweka orodha hiyo hadharani.
 
Aidha, amesema kuwa wale wote wanaodhani kuwa vita dhidi ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni mzaha, wataona hali itakavyokuwa kwani vita hiyo ni kubwa sana na wataishinda.
 
Kigwangalla ambaye pia ni mtaalamu wa afya alisema kuwa suala la mtu kuwa shoga si suala la kibaolojia (asili) bali ni watu tu kujiendekeza na hivyo watakahikikisha wanalikomesha.
 
Sheria ya ndoa ya Tanzania inapinga watu wa jinsia moja kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, lakini pia ni kitu kilichozuiliwa katika vitabu vitakatifu vya dini.

KIGWANGALLA AAGIZA KUKAMATWA KWA KIJANA MAARUFU MITANDAONI KWA USHOGA, JAMES DELICIOUS

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla, akijibu hoja za wabunge ameviagiza vyombo vya usalama kumtafuta mtu anayejulikana kwenye mitandao ya kijamii kama "James Delicious" kwa kujitangaza kama shoga kinyume cha sheria na kumfikisha mbele ya sheria kujibu tuhuma za kuendesha biashara ya kuuza ngono ya kinyume cha maumbile.

Chanzo: Jamii Forums

'Oktoba 14 kwangu ina maana zaidi ya moja' Dk. Kigwangalla

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mtoto Sheila akimlisha keki baba yake Dk. Kigwangalla

Na Dk. Hamisi Kigwangalla.

Tarehe ya leo, miaka minane iliyopita alizaliwa binti yangu Sheila. Ni Mtoto wangu wa kwanza. Unaweza kukadiria mshawasha na mcheche niliokuwa nao siku hiyo. 

Kila mwaka tunapomkumbuka baba wa Taifa letu, basi mimi hukumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa mwanangu pia. Mwaka juzi niliandika makala. Nimeitafuta siioni. Nitajaribu hapa leo kurejea, Kwa ufupi, maudhui ya makala ile. 

Wakati naandika makala ile nilikuwa nimetoka kutangaza nia ya kuchukua fomu ya kuwania Urais. Nilitafakari sana mustakabali wa maisha yangu. Nilipotoka na nilipofikia. Nikahusianisha Tanzania ile na Tanzania ya akina Sheila. Mustakabali umebadilika kabisa! 

Mwanangu Sheila amezaliwa kwenye zama za utandawazi, elimu yake, Kwa mimi mzazi mwenye kuelewa dunia ya sasa na ushindani atakaopaswa kuukabili, naliona jukumu langu la kumuandaa vema. 

Mimi, hadithi yangu, ni tofauti sana na hadithi ya mwanangu. Siyo lazima na yeye apitie madhila yangu. Yeye ninamuandaa. Namuandaa ajue wajibu wake wa kujiandaa kupambana na ushindani. Mimi niliandaliwa na nchi. Hii ni tofauti kubwa ya kwanza. 

Mimi na Ndg. Bashe tulipoingia shule mwaka 1984, pale Shule ya Msingi Kitongo, na kufundishwa kusoma na kuandika na Mwl. Malunde, tulipelekwa kutimiza majukumu ya wazazi kama ambavyo Serikali ilikuwa ikielekeza. Watoto tulikuwa ni hazina nyeti ya Taifa, mali ya jamii nzima. Leo kila mtu na wanaye. Kila mtu na wa kwao. 

Darasa letu lilikuwa na watoto wa kila mtu, bila tofauti ya kipato ama cheo. Tulisoma na watoto wa Mkuu wa Wilaya, Watoto wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wilaya, Bwana Tawala, Meneja wa Benki, matajiri wa kiarabu na kihindi nk. Shule zilikuwa ndiyo hizo tu. Sote tulipata fursa sawa na kwa maana hiyo tulikuwa na mustakabali sawa wa maisha yetu ya baadaye. 

Mimi nilipelekwa shule na mama yangu mzazi, bi Bagaile Lumola. Hii ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kipekee kwenye maisha yangu. Nilifurahia sana shule, japokuwa mara nyingi nilienda shule bila kula, na sare zangu za wasiwasi, miguu peku, lakini sikuwahi kuona tofauti yoyote ile kati yangu na watoto wa Mkuu wa Wilaya. Hata wao mara nyingine walikuja shuleni bila viatu. Sote tuliona sawa tu, kwamba ni 'kawaida' tu. Pengine hayo yalikuwa ndiyo maisha ya nyakati zile. 

Utandawazi umeibadilisha kabisa jamii yetu. Udugu wetu mpana unaanza kupotea. Zamani tatizo la mmoja wetu mtaani lilikuwa letu sote. Furaha yake ilikuwa yetu sote. Nakumbuka jirani na nyumbani kwa bibi yangu Mama Bagaile, aliyenilea, kulikuwa na familia ya Mzee mmoja mkatoliki mwenye kushika dini yake sana, Mzee Kidola, kila akitaka kuchinja, iwe kuku iwe mbuzi, atanoa kisu chake vizuri, atamfuata babu yangu, ambaye alikuwa muislamu. Na kila akichinja sisi ni lazima tuchekelee maana lazima agawe nyama kwa babu yangu. Hivyo hivyo, siku za Eid, ni lazima tuwapelekee sufuria la pilau na nyama. 

Mzee Kidola alipenda kufuturu nasi uji wa pilipili manga na chai ya viungo, enzi hizo tukifuturu nje ya nyumba barazani, na wapita njia wakikaribishwa! 

Upendo na mshkamano uko hatarini kupotea. Leo Ndg. Saidi anatolewa macho mchana kweupe, hadharani, anafanyiwa unyama watu wanatazama tu. Udugu wetu, upendo na mshkamano wetu umeenda wapi? 

Hii ni tofauti ya pili ya maisha ya makuzi yangu na makuzi ya mwanangu Sheila. 

Tanzania yangu mimi ni Tanzania iliyojengwa na baba wa Taifa, Mwl. Nyerere. Ni Tanzania iliyotoa fursa kwa mtoto aliyelelewa na mama ntilie kuota ndoto ya kuwa Daktari na kuitimiza. Ni Tanzania iliyotoa fursa sawa kwa mtoto wa  mama ntilie na mtoto wa Mkuu wa Wilaya kuwa Mbunge. 

Tanzania ya Sheila, mwanangu, ni Tanzania ninayowajibika kuijenga. Kila kukicha natafakari, Je ni Taifa gani ninaloandaa kwa ajili ya mwanangu na wajukuu zangu? 

Kila nikiangalia nyuma ninakotoka. Najiuliza nimefikaje hapa. Ni muujiza. Nikitazama tulipo na nikitafakari tunapokwenda, nabaki na maswali magumu sana kichwani! 

Hivi, Tanzania ninayoijenga mimi leo, itatoa fursa Sawa Kwa Sheila, mtoto wa Mbunge, na kwa mtoto mwingine wa mama ntilie kama mimi? 

Ninapokukumbuka baba wa Taifa moyo wangu unavuja damu kwa uchungu; machozi ya furaha na upendo yananitoka, ndoto zako zimegusa maisha yangu. Naahidi kufanya kila niwezalo kuishi falsafa yako, siyo kwa kutembea na 'kifimbo' tu na kuvaa suti za Mao, bali kwa kutoa uongozi madhubuti wakati wa kutunga sera ili kulinda misingi ya taifa tulilorithi kutoka kwa babu zetu. 

Viongozi wa zama zetu tuna kazi ya ziada ya kufanya. Ni lazima tuweke ubunifu kwenye malengo ya mbali ya Taifa letu, sera zetu na mikakati yetu. Zama zimebadilika, utandawazi umetamalaki, lakini kuna mambo ya msingi tuna wajibu wa kuyalinda kwa nguvu zetu zote kwa kuwa ni tunu za Taifa letu. 

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA KONGAMANO LA 30 LA NIMR JIJINI DAR LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu  Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali ndani nje ya nchi wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela akizungumza mapema leo, alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Katika kongamano hilo kauli mbiu yake ni “Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.”. 


Dkt Mwele alieleza pia Mada zitakazojadiliwa ndani ya kongamano hilo kuwa zitajikita zaid kwenye maeneo kama vile 1. Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake,3. Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria,4. Usalama wa Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5. Mkakati wa afya moja katika kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6. Magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele.

BOFYA HAPA KUSOMA HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS KUHUSU KONGOMANO HILO, KUSOMA HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU WA NIMR DKT MWELE MALECELA BOFYA HAPA

Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo kufungua Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kati ni Naibu Waziri wa Afya,  Dkt.Hamis Kigwangala.

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. HAMISI KIGWANGALLA AMKANA DR MWAKA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kuna baadhi ya magazeti na mitandao imekuwa ikiandika kuwa Dkt. Kigwangalla amesoma high school na aliyekuwa 'Tabibu', Ndg. Juma Mwaka, shule ya Kigoma Sekondari na kwamba walikuwa marafiki; hizi ni habari za uongo, za kupika zenye kupotosha ukweli ili kuwaaminisha watu kuwa 'wanajuana' na pengine wana ugomvi 'binafsi'.

Nimekuwa nikimpuuza kwa sababu sikuwa na haitotokea nikawa na nia mbaya dhidi ya mtanzania mwenzangu yeyote kwa sababu tu mimi nina dhamana ya uongozi. Sinaga tabia hiyo.

Uongo ukirudiwa rudiwa hubadilika na kuwa ukweli. Leo nimeamua, hapa chini, kukanusha ili watanzania pia mumpuuze, tuendelee kuimarisha huduma za tiba asili na tiba mbadala kutoka kwa matabibu wa kweli wanaofuata taratibu na siyo wasanii kama huyu. Uongo ama uzushi dhidi yangu mimi binafsi kamwe hautonirudisha nyuma mimi kama mtumishi wa umma. Lazima ifike mahali tujenge nchi ya watu 'serious' wanaofuata Sheria, Kanuni na Taratibu. Wanaoheshimu Serikali. Kwenye Afya za watanzania hatuwezi kuvumilia usanii, lazima tuwalinde walaji. Hili ni jukumu tulilopewa na Mhe. Rais. Tutasimamia Sheria ipasavyo. Hatutolegeza hata kidogo.

1. Sikusoma 'high school' Kigoma Sekondari. Nimesoma O'level (form I - IV) Kigoma Sekondari. High School nilisoma Shinyanga Sekondari. Sikumbuki kusoma katika shule zote hizi mbili na mtu mwenye Jina Hilo. Kama alisoma Kigoma Sekondari labda mbele yangu ama nyuma yangu. Pia kipindi nasoma Kigoma Sekondari, hakukuwa na 'high school'.

2. Ndg. Juma Mwaka hajawahi kuwa rafiki wala adui yangu. Sina ugomvi binafsi. Nafanya kazi ya kusimamia Sheria ya tiba asili na tiba mbadala ipasavyo.

3. Naithamini tiba asili na tiba mbadala na Ndiyo maana nimeongoza Wizara ya Afya kufanya Mapinduzi makubwa kwenye eneo hili, ikiwemo kuweka utaratibu mzuri na rahisi zaidi wa kusajili watoa huduma, dawa zao, mazingira wanapotunzia dawa, wasaidizi wao, viwanda vyao, na pia kuweka mikakati ya uanzishwaji wa viwanda vya dawa za tiba asili na tiba mbadala sambamba na kufanyia utafiti dawa zao na kudhibiti ubora wa dawa zenyewe na dozi wanazowapa wateja.

4. Muulizeni Ndg. Juma Mwaka anaposema ana ugomvi 'binafsi' na mimi, anamaanisha nini, ugomvi upi? Juu ya nini? Awape taarifa kamili. Mimi Sina ugomvi naye. Kwanza sikuwahi kumjua kabla ya ziara yangu ya kikazi pale Foreplan, ntakuwaje na ugomvi na mtu nisiyemjua? Si utakuwa ujuha huo?

5. Mnaofuatilia suala hili mtakeni Ndg. Juma Mwaka awape majibu ya Msingi ya hoja za wakaguzi kutoka Wizara ya Afya. Mimi nilikuwa msimamizi nikiwapa nguvu wataalam wafanye kazi yao. Wataalamu walikuwepo, nao ana ugomvi nao 'binafsi'? Mwambieni awajibu kama dawa za tiba ya kisasa kukutwa kwenye eneo lake la kazi ilikuwa halali? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya maboksi 200 ya dawa? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya magunia 10 ya dawa za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa usajili? Alikuwa na uhalali wa kuendelea kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wateja wake wafuate dawa pale ili wasikatishe dozi? Tena kinyume na katazo la Baraza la tiba asili na tiba mbadala! Yeye yuko juu ya Serikali? Yuko juu ya Sheria? Ama anadhani anaweza kuidhihaki na kuiogofya Serikali?

6. Baada ya ziara yangu ya December 2015, ambapo sikutoa maelekezo ya kumfungia wala kumfutia kibali, niliwaelekeza Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala kuwa wawaite wawaelekeze matabibu wote wafuate Sheria, kanuni na taratibu. Waliitwa. Wakaelekezwa. Waungwana wakatii. Yeye hakutii, wakamfuta. Baada ya kufutiwa usajili, akaendelea kujitangaza na kutoa huduma, yeye ni nani?

7. Kufanya haya ni kuvunja sheria za nchi. Na makosa haya yana adhabu zake. Sisi kama Serikali tumeagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Serikali ina mkono mrefu, itamkamata. Itamtia nguvuni na atafikishwa mahakamani. Ataenda kujitetea huko kuwa ana 'ugomvi binafsi' na Naibu Waziri Kigwangalla!

Mwisho, aende akafuatilie kisa cha mfanyabiashara wa kigiriki aliyesema ameiweka Serikali mfukoni - Mwalimu Nyerere alimfanya nini!

Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.