HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Lowassa aachiwa kwa dhamana

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa 8.15 na kuelekea nyumbani kwake.
Akizungumza baada ya mahojiano hayo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.
Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
"Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29," amesema.

Lowassa awasili makao makuu ya polisi, Ulinzi Waimarishwa Barabara Zote

Msafara wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ukiwa na magari manne ukisindikizwa na magari mawili ya polisi umewasili makao makuu ya polisi.

Jana Lowassa alipewa taarifa ya kwenda  kuhojiwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Mapema leo, Jumanne asubuhi polisi wameimarisha ulinzi katika barabara zote zinazoingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Mtaa wa Ohio.

Polisi wakiwa na silaha wameegesha magari yao kwenye kila barabara inayoingia makao makuu ya jeshi hilo, huku wengine wakizunguka zunguka maeneo ya jirani.

Wananchi wanaruhusiwa kupita lakini walio kwenye vikundi wanasimamishwa na kuhojiwa, huku wengine wakizuiwa kabisa kukatiza eneo hilo.

Lowassa aitwa ofisini kwa DCI

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz.
Lowassa akizungumza na Mwananchi leo (Jumatatu), amesema ameitwa kwa DCI lakini hajui anachoitiwa.
Hata hivyo, amesema anahisi ni kauli yake kuhusu mashehe wa kikundi cha Uamsho cha Zanzibar wanaoshtakiwa kwa tuhuma ya ugaidi.
“Ni kweli nimetakiwa niripoti kesho saa 4:00 asubuhi katika ofisi ya DCI. Sijui wananiitia nini, lakini nahisi ni kuhusu nilichosema kuhusu mashehe wa Uamsho,” amesema Lowassa.

Jana katika taarifa kwa vyombo vya habari, Lowassa alikaririwa akimtaka Rais John Magufuli kuwaachia huru mashehe hao wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Taarifa hiyo ilisema Lowassa alitoa ombi hilo alipozungumza katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara.

LOWASSA AWALILIA WANAFUNZI WALIOFARIKI KATIKA AJALI, MAITI 32 ZAPELEKWA MOCHWARI KATIKA HOSPITALI YA LUTHERAN KARATU.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.
Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema
Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.
Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.
Tutaendelea kuwapa habari zaidi kuhusu tukio hili.

Lowassa, Maalim wajadili migogoro ya CUF

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amekutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif katika ofisi ya Lowassa iliyopo Mikocheni jijini hapa leo mchana.
Katika mkutano huo Lowassa na Maalim wamejadiliana masuala ya siasa ikiwamo migogoro ya ndani ya CUF na namna ya kuimarisha umoja na mshikamano wa umoja wa vyama vya upinzani.
Maalim Seif, ni Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu wa Zanzibar na Lowassa ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema.

LOWASSA: WALIOFUKUZWA CCM KARIBUNI CHADEMA

Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa amesema anawakaribisha Chadema waliofukuzwa uanachama baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitisha uamuzi wa kuwatimua 12 kati ya 24 walioadhibiwa.
Amesema walioadhibiwa ni mashujaa waliosimama kutetea demokrasia. Lowassa yuko katikati ya tuhuma zilizosababisha wanachama wengi wa CCM kuchukuliwa hatua baada ya uamuzi wake wa kuhamia Chadema kupinga kuenguliwa kugombea urais, kufuatiwa na viongozi kadhaa na wanachama kujiondoa chama tawala na kujiunga na upinzani.
 Katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari jana, Lowassa ambaye pia alikuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM hadi mwaka 2015, amesema viongozi waliotimuliwa na chama hicho tawala walitumia demokrasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria.
“Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki, demokrasia na taratibu na kupinga dhuluma ndani ya chama chao na nchini,” amesema Lowassa, ambaye kabla ya kuenguliwa alikuwa mmoja wa makada waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupitishwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM.

Lowassa, Sumaye Wawasili Mahakamani Kusikiliza kesi ya Lema

Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Vicent Mashinji, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowasa, Waziri Mkuu Msaatafu Sumaye na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro wakiwa mahakamani kusikiliza uamuzi wa Mahakama kuhusu dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema unaotolewa leo
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless  Lema akishuka kwenye gari kuingia mahakamani.

PICHA: VIONGOZI MBALIMBALI WA KISIASA WASHUHUDIA MECHI YA SIMBA NA YANGA

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.(Picha na Francis Dande)
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 
Freeman Mbowe akiwapungia mashabiki wa soka. 
Mbowe.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto), akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.  
 Lowassa akishuhudia pambano la Simba na Yanga. 
 Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya akizungumza na Edward Lowassa.
 Viongozi wakiwa wamesimama kuamboleza kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Yanga na timu ya taifa, Godfrey Bonny.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, akiwasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia pambano la Simba na Yanga.