HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MBOWE AFUTURISHA MISIKITI MINNEJIMBONI KWAKE,WAISLAMU WILAYA YA HAI WAMTUNUKU CHETI.

Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Helga Mchomvu wakati wa Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakipata Futari katika msikiti wa Kibaoni wilayani Hai.
Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Omar Mohamoud akizungumza wakati wa hafla ya kupata Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki ,Fahad Lema akisoma Risala kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe mara baada ya kumalizika hafa ya kupaa futari kwa pamoja katika msikit wa Kibaoni wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimiana na Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki Fahad Lema mara baada ya kuwasilisha ombi la kusaidiwa ujenzi wa vyumba vya madrasa ambapo Mh Mbowe alichangia kiasi cha Sh Mil,2 kwa ajili ya kununua mbao za kuezekea Paa.  
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimana na Waumini katika Msikiti wa Kibaoni uliopo Bomang'ombe wilayani Hai ,mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akipata Futari na waumini wengine katika Msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai baada ya kushiriki pia katika miskiti mingine mitatu .
Mmoja wa viongozi wa Dini ya Kiislamu Mwl Mohamed Mbowe akizungumza wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe katika Msikiti wa Lambo .
Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji ,Habib Nasiwa akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe kwa jitihada zake za kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali katika wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akionesha zawadi ya Cheti alichokabidhiwa na Waislamu katika wilaya ya Hai.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi zawadi ya Cheti kwa Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu ili afungue na kusoma kilichoandikwa ndani.
Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu (Mwenye suti) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Cheti kilichotolewa na Waislamu wa wilaya ya Hai,kwa Mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe. 
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akishiriki Dua mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliyoandaliwa katika misikiti minne tofauti ukiwemo msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai.
Baadhi ya wauimini wa Dini ya Kiislamu wakiwasiliza viongozi mara bada ya kushiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Msikiti wa Lambo uliopo Machame ambao Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe amechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wake.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni,Mh ,Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali.
“Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
Mh Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo katika misikiti minne tofauti ya Modio ,Rundugai,Kibaoni na Lambo.
Cheti hicho kilichosainiwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Sheakh ,Omary Mahmoud ambaye pia ni katibu wa msikiti wa Kibaboni Bomangombe kimetolewa ikiwa ni ni ishara ya kutambua mchango mkubwa unatolewa na Mbunge huo kwa Waislamu.
AkIzinunguza mara baada ya kukabidi cheti hMjumbe wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa alitoa shukrani kwa niaba ya waislamu wa jimbo la Hai kwa namna ambavyo ameendelea kujitoa pamoja na kuchangia ujenzi wa msikiti wa Lambo.
“Nimehemewa sana ,sidhani kama naweza kusema kiasi cha kutoshereza ,nimehemewa na kujaaa furaha ya kufikiwa na Mh Mbowe,halikua jambo rahisi la kumpata leo ,kwanza tukijua Bunge linaendelea kadharika tukijua kwamba ana majukumu mengine mengi lakini akaona ashiriki na sisi wilaya ya Hai.”alisema Nasiwa.
“Jambo fupi la kukushirikisha jioni ya leo,mheshimwa tunakupongeza kwa kujua umuhimu wa ramadhan kwa kuacha shughuli zako na kuja kushiriki nasi katika kutufuturisha,tunakupa asante sana na mungu akubariki sana,”aliongeza Alhaji Nasiwa.
Katika hafla hiyo ya kufuturisha ,Mh Mbwe alishiriki katika misikiti yote minne ambapokatika msikiti wa Mudio alitoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi inayomilikiwa na msikiti huo na pia alikabidhi kiasi cha sh Mil moja kwa msikiti wa Rundugai kwa ajili ya mwalimu anayefundisha masomo ya dini katika shule ya Msingi na Sekondari za Rundugai .

PICHA: YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson akiongoza kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 06, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
 Mbunge wa Temeke (CUF) Mhe.Abdallah Mtolea katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma June 6, 2017.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Southern Highland kutoka Iringa wakiwa Bungeni kujifunza Shughuli mbalimbali katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Jaquiline Ngonyani akiuliza swali katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Rose Tweve akiuliza swali katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba  akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Mhe.January Makamba  katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.


MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 42, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 06, 2017.

 Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Tulia Ackson akijibu miongozo mbalimbali ya wabunge mara baada ya kumaliza kipindi cha Maswali ya Kawaida katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 01, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 aziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussein Mwinyi akizungumza jambo na Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Catherine Ruge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma June 1, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Anna Mollel akiuliza swali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kantui kutoka Kilosa wakiwa Bungeni kujifunza Shughuli mbalimbali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.

Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO, DODOMA.

PICHA: YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa Kaliua(CUF) Mhe.Magdalena Sakaya katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
  Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe,Prof.Joyce Ndalichako akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angelina Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk.Susan Kolimba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Philip Mpango akisoma Hotuba ya Makadirio  ya Mapato na Matumizi ya Wizara  ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Faida Bakar akiuliza swali katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Amina Mollel akiuliza swali katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe  akizungumza jambo na Naibu wake Mhe.Anastazia Wambura katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijadili  jambo na Mbunge wa Iringa Mjini(CHADEMA) Mhe.Peter Msigwa katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe.George Masaju akifafanua jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.Kushoto kwake ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani.

Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.