Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Inmi Patterson, pale alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Inmi Patterson, pale alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale alipotembelewa na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania, wakiongozwa na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa Sarah Cooke(kulia kwake) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Sarah Cooke (wa pili kushoto) pale Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi kutoka Norway, Mheshimiwa Hanne Kaarstad (katikati) na Balozi kutoka Finland Mheshimiwa, Pekka Hukka (kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Ghasia (wa pili kulia) akiongoza kikao cha pamoja cha mashauriano kati ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja na Wadau wa Mashirika ya Maendeleo Duniani, kutoka Benki ya Dunia (World Bank) na Shirika la fedha la kimataifa (IMF) kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti na Wadau kutoka Mashirika ya Maendeleo Duniani wakiwa katika kikao cha Mashauriano ya pamoja kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASALIMIANA NA MABALOZI WA UINGEREZA NA MAREKANI LEO BUNGENI
By: VIJIMAMBO on June 08, 2017 / comment : 0 Kassim Majaliwa, Mabalozi, Matukio, waziri mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini, Mheshimiwa Inmi Patterson kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa, Sarah Cooke kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WATEULE
By: VIJIMAMBO on April 23, 2017 / comment : 0 Mabalozi, Matukio
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazunguzo na Mabalozi Wateule wanaoenda kuiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani.Mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma, yalijikita katika kujadili namna bora ya kuiwakilisha Tanzania ughaibuni kwa kuzingatia sera ya nchi ya mambo ya nje, kwa lengo la kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo, na kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi ya nchi yetu ikiwemo kutangaza shughuli za utalii zinazopatikana nchini.
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisisitiza jambo
Balozi Mteule Baraka H. Luvanda akichangia jambo wakati wa mazungumzo. Punde baada ya mazungumzo na Mhe. Naibu Waziri, Mabalozi walikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Katibu Mkuu Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Aziz P Mlima akiongea na Mabalozi ofisini kwake mjini Dodoma
Mazunguzo yakiendelea
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEWATAKA MABALOZI WA TANZANIA KUTANGAZA FURUSA ZA UWEKEZAJI TANZANIA
By: VIJIMAMBO on April 23, 2017 / comment : 0 Kassim Majaliwa, Mabalozi, Matukio, waziri mkuu
BALOZI SEIF AKUTANA NA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA NCHI ZA NJE
By: VIJIMAMBO on April 12, 2017 / comment : 0 Balozi Seif Ali Iddi, Mabalozi, Matukio
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mabalozi wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani hapo Ofisini kwa Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif wa kwanza kutoka Kushoto akibadilishana mawazo na Mabalozi hao ambao wa kwanza kushoto mwa Balozi Seif ni Balozi Dr. Abdulla Possi anayekwenda Shirikisho la Ujerumani na Balozi Sylvester Ambukile anayeelekea Nchini Afrka Kusini.
Balozi Seif wa Tatu kutoka Kulia akiwa katika Picha ya pamoja na Mabalozi Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani mara baada ya kufanya nao mazungumzo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Balozi Sylvester Mabumba Comoro, Balozi Sylvester Ambukile Afrika Kusini na Balozi Omar Yussuf Mzee Algeria, na kushoto ya Balozi Seif ni Balozi Baraka Luvanda India na Balozi Dr. Abdulla Possi Shirikisho la Ujerumani. Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mabalozi wanayoiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mataifa rafiki Duniani wana kazi ngumu na nzito ya kuinadi Tanzania katika Nchi hizo ili ipate kuungwa mkono katika harakati za kuimarisha Uchumi wake.
Alisema yapo maeneo na sekta kadhaa ambazo zimeshajengewa miundombinu imara kama Utalii, Mawasiliano, Kilimo, Biashara na Afya zinazohitajika kupata msukumo kwa mataifa rafiki na washirika wa maendeleo katika njia ya kustawisha maisha ya Wananchi na kuongeza pato la Taifa.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Mabalozi Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kuliwakilisha Taifa kwenye Mataifa mbali mbali Duniani walipofika kuaga rasmi wakijiandaa kuelekea kwenye vituo vyao vya Kazi.
Mabalozi hao aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar ni Balozi Sylvester Mabumba anayekwenda Visiwa vya Comoro, Balozi Baraka Luvanda anaelekea Nchini India, Balozi Omar Yussuf Mzee anakwenda kuanzisha Ubalozi Mpya waTanzania Nchini Algeria, Balozi Dr. Abdulla Posi anakwenda Shirikisho la Ujerumani na Balozi Sylvester Ambukile anayekwenda Nchini Afrika Kusini.
Balozi Seif Ali Iddi alisema kumalizika kwa vita Baridi Vikuu vya Pili vya Dunia ndani ya Karne ya 20 vilivyokumbwa na wimbi la Mataifa Makubwa kutaka kuendelea kutawala dhidi ya yale yaliyokuwa yakipigania Kujitawala kumeipeperusha Dunia hiyo kuelekea kwenye uchumi zaidi.
Alisema nafasi yao ya Kidiplomasia ni vyema wakaitumia katika ushiriki wao kwenye vikundi mbali mbali vya ushirikiano vinavyowapa fursa Wanadiplomasia hao kubadilishana mawazo na Taaluma ya jinsi ya kustawisha Uchumi na Maendeleo ya Mataifa yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Mabalozi hao Wapya wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi waliyoipata ambapo Rais wa Tanzania hakufanya makosa kutokana na vigezo tofauti alivyovitumia katika kuwapata kushika wadhifa huo.
Balozi Seif alitaja Nchi wanazokwenda Mabalozi hao za Shirikisho la Ujerumani, Comoro, Algeria, India, Afrika Kusini na Israel kwamba zimekuwa na uhusiano mzuri wa Kihistoria na Tanzania kiasi kwamba jukumu lao linapaswa kuzingatia udumishaji wa ushirikiano huo.
Alisema zipo nafasi za mafunzo ya Elimu ya Juu, Taaluma katika Sekta za Kilimo, Afya, Biashara na Utalii zinazopatikana katika Mataifa hayo kiasi kwamba Mabalozi hao watapaswa kuzifuatilia ili zilete tija kwa Vijana watakaopata Taaluma ya Kujenga Taifa lao.
Akitoa Shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake Balozi Sylvester Luvanda anayeiwakilisha Tanzania Nchini India alisema wamethamini fursa ya uteuzi waliyopewa na Taifa na kuahidi kwamba watawajibika kwa nguvu zao zote.
Balozi Sylvester alifahamisha wazi kuwa inatia moyo na faraja kuona kwamba Nchi wanazokwenda kufanya kazi bado zina mafungamano mazuri ya ushirikiano wa Kidiplomasia na Tanzania.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
12/4/2017.
RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI PAMOJA NA MABALOZI WANNE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
By: VIJIMAMBO on February 26, 2017 / comment : 0 Mabalozi, Magufuli, Matukio, Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba(Wakwanza kulia) , Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni (Wakwanza kushoto) pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(Watatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma) na Mabalozi Pindi Chana(Wakwanza kulia walisimama mstari wa nyuma ) , Balozi Matilda Masuka(Wapili kutoka kulia waliosimama mstari wa nyuma), Balozi Abdallah Kilima(Wapili kutoka kushoto mstari wa nyuma) na Balozi Silima Kombo Haji (Wakwanza kushoto waliosimama) mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
By: VIJIMAMBO on February 13, 2017 / comment : 0 Mabalozi, Magufuli, Matukio, Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke aliyefika Ikulu kwa ajili ya Mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel Fred Kidega mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel Fred Kidega mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amemshika mkono Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga wakati akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akifurahia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga mara baada ya kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais Magufuli Awapangia Vituo vya Kazi Mabalozi Watatu
By: VIJIMAMBO on February 12, 2017 / comment : 0 Habari, Mabalozi, Magufuli, Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wapya watatu ambao aliwateua tarehe 03 Desemba 2016.
Mabalozi hao waliopangiwa vituo ni Joseph Sokoine anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Omar Yussuf Mzee anayekuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Algeria na Grace Mgavano anayekwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ladis Komba nchini Uganda ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Aidha, Balozi Sokoine ambaye anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Deodorus Kamala ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Mzee kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alishawahi kushika nafasi mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na nafasi ya mwisho alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya kwanza ya Rais Dkt. Ali Mohammed Shein.
Kwa upande wa Balozi Mgavano kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Ubalozi alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
Mabalozi wote waliopangiwa vituo vya kazi wataapishwa na Rais Ikulu jijini Dar Es Salaam leo Jumapili tarehe 12 Februari 2017 saa tano asubuhi.
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA
By: VIJIMAMBO on February 11, 2017 / comment : 0 Dkt. Augustine Mahiga, Mabalozi, Magufuli, Matukio, Rais, WAZIRI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mabalozi wanaziwakilisha nchi mbalimbali nchi Tanzania na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuanza mwaka mpya iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara Balozi Dkt.Aziz P. Mlima wakifuatilia hotuba ya Mhe. Rais Magufuli
Sehemu ya Waheshimiwa Mabalozi wakifuatilia hotuba
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi wakifuatilia hotuba
Hotuba ikiendelea
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Lu Youqing
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maaendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo nchini Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Joseph Sokoine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Celestine Mushy
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Baraka Luvanda
Mkuu wa Kitengo cha Mawaliano Serikalini na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga akizungumza katika hafla hiyo
Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mhiga wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi
Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga wakiwa katika picha ya pamoja Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa nchini Tanzania
Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
|
Rais Magufuli akutana na Mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewashukuru Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kwa ushirikiano na mchango wao kwa Serikali ya Tanzania ambao umesaidia kufikia malengo ya Serikali kwa mwaka uliopita wa 2016. Rais Magufuli aliwasihi Waheshimiwa Mabalozi waendelee kuisaidia Serikali ili kufikia malengo iliyojiwekea kwa mwaka 2017.
Mhe. Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam kati yake, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo nchini.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli alisema kuwa mwaka 2016 ambao ulikuwa mwaka wake wa kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Awamu ya Tano umekuwa wa mafanikio makubwa ambapo nchi imendelea kudumisha amani, mshikamano, umoja na Muungano umeimarika. Aidha katika mwaka huo, Serikali imeongeza jitihada za kuimarisha demokrasia, kupiga vita rushwa, ujangili na ufisadi.
Mhe. Rais Magufuli aliongeza kusema kuwa, Serikali ya Tanzania imefanikiwa kiuchumi na kuwa nchi ya pili yenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika ikitanguliwa na Ivory Coast. Uchumi wa Tanzania ulitarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka jana kutoka asilimia 7.0 mwaka uliotangulia. Pia kiwango cha mfumuko wa bei kilipungua kutoka asilimia 6.5 mwezi Januari 2016 hadi kufikia asilimia 2.5 mwezi Oktoba mwaka huohuo.
Akizungumzia suala la ukusanyaji mapato, Mhe. Rais Magufuli alisema kwamba Serikali inasimamia kikamilifu suala hilo ambapo kwa sasa kiwango cha ukusanyaji wa mapato kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 850 hadi kufikia shilingi trilioni 1.2 kwa mwezi.
Kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2021, Rais Magufuli aliwaeleza Mabalozi hao kuwa, mpango huu unalenga kujenga Uchumi wa Viwanda ili kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inavyoelekeza.
Alieleza kuwa katika kutekeleza Mpango huo kiasi cha shilingi Trilioni 107 kinahitajika na kati ya hizo Serikali itatoa shilingi trilioni 59 ambazo ni wastani wa shilingi trilioni 11.8 kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Utekelezaji wa mpango huo umeshaanza ambapo Serikali katika Bajeti yake ya mwaka 2016 imetenga kiasi cha shilingi trilioni 29.5 ambazo ni sawa na asilimia 40 ya Bajeti ya Serikali kwa ajili ya Bajeti ya Maendeleo. Kiwango hicho ni cha juu zaidi kuwahi kutengwa kwenye bajeti ya maendeleo katika historia ya Tanzania.
Fedha hizo zimeelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda kama vile nishati, barabara, reli na maji. Aliongeza kusema kuwa Kati ya fedha hizo shilingi trilioni 5.5 zimetengwa kwa ajili ya miundombinu ya usafirishaji na shilingi trilioni 1.2 zimetengwa kwa ajili ya nishati ya umeme. “Hii imetuwezesha kuendelea au kuanza utekelezaji wa miradi mikubwa ya usafiri ikiwemo reli, barabara, anga, maji pamoja na miradi ya umeme. Tuliweza pia kununua ndege mpya sita ambazo bila shaka zitasaidia kukuza sekta ya utalii nchini”
Kwa muktadha huo, Rais Magufuli aliwaomba Mabalozi kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza katika ujenzi wa Reli wa kiwango cha kimataifa kutoka Dar Es Salaam hadi Mwanza na Kigoma na kuunganisha hadi nchi za Burundi, DRC na Rwanda. Serikali kwa kutumia fedha zake za ndani itaanza kujenga kilomita 300 kuanzia Dar Es Salaam hadi Morogoro.
Vile vile, Serikali imeweka kipaumbele kwenye kuboresha huduma za jamii ikiwemo sekta ya elimu iliyotengewa trilioni 4.8 na sekta ya afya kiasi cha trilioni 1.9. Kupitia mpango huu wa kuboresha sekta ya elimu, kiwango cha udahili kwa watoto wanaojiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza na wale wanaopokea ufadhili wa masomo ya juu kimeongezeka mara dufu ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Akizungumzia masuala ya Diplomasia, Mhe. Rais Magufuli aliwaeleza Mabalozi na Wawakilishi hao wa Mashirika ya Kimatifa kuwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi ningine yameimarika ambapo Viongozi Wakuu kutoka nchi mbalimbali wamefanya ziara nchini Tanzania. Aidha, yeye binafsi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Viongozi wengine Serikalini wamefanya ziara za kuimarisha ushirikiano kwenye nchi mbalimbali. Katika ziara hizo, Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano. Mhe. Rais aliahidi kuwa Tanzania itaendelea kuwa mwanachama mwaminifu kwenye Mashirika ya Kimataifa na Kikanda ikiwemo Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN), Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki na mengine.
“Tunawashukuru sana Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na Kikanda kwa kazi nzuri mnayoifanya hapa nchini kwetu. Mafanikio yote haya niliyoainisha yamewezeshwa na ushirikiano wenu na naahidi Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwenu ili muweze kufanya kazi zenu vizuri” alisema Rais Magufuli.
Vilevile aliwaomba Mabalozi hao kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kuiwezesha kufikia malengo yake na aliwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini na kutumia fursa za malighafi, nguvukazi na soko kubwa lililopo nchini.
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli alianisha changamoto zinazochangia kukwamisha jitihada mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na Mabadiliko ya Tabianchi na kuiomba Jumuiya ya Kimataifa kushirikiana katika kukabiliana na changamoto hii ili kuziwezesha jamii zetu kufikia maendeleo na ustawi. Pia kupitia Mabalozi hao alizipongeza nchi zilizoridhia Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na kueleza kuwa Tanzania imeanza mchakato wa kuridhia Mkataba huo tangu mwezi Aprili, 2016.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais aliwaeleza rasmi Mabalozi hao azma ya Serikali ya kuhamishia Makao Makuu mjini Dodoma katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake na kuwaomba Mabalozi hao nao waanze mchakato wa kuhamia Dodoma.
“Mwaka jana wakati nakabidhiwa uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi niliahidi ndani ya miaka mitano Serikali itahamia Dodoma. Tayari Waziri Mkuu na baadhi ya Wizara zipo Dodoma. Nawaomba Mabalozi nanyi muanze kufikiria kuhamia Dodoma kwani Serikali imekwishatenga viwanja kwa ajili yenu, alisisitiza Rais Magufuli.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe hapa nchini, Mhe. Edzai Chimonyo alisema kuwa anaipongeza Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Magufuli kwa hatua kubwa ya maendeleo iliyopiga katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wake. Alisema kuwa katika kipindi hiki wameshuhudia uchumi ukikua, nidhamu katika utumishi wa umma, ukusanyaji wa mapato kuongezeka, na kiwango cha mfumuko wa bei kupungua.
Aidha, aliongeza kuwa wanaunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga miundombinu wezeshi ikiwemo Reli kwa vile kutawezesha kukuza biashara na nchi jirani na mataifa mengine kwa ujumla. Pia alipongeza jitihada za Serikali katika kukuza ushirikiano na Sekta Binafsi ambayo ina mchango mkubwa kwenye maendeleo na kupongeza juhudi za Tanzania kwenye usuluhishi wa migogoro kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu na kuitaja Tanzania kuwa ni Kisiwa cha Amani.
Kuhusu Mabalozi kuhamia Dodoma, Balozi Chimonyo alisema Jumuiya ya Mabalozi inaunga mkono wazo hilo na wapo tayari kuhamia Dodoma kama ilivyopangwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 10 Februari, 2017
|
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi kwa kushiriki Maonesho ya...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
WAZIRI DKT. BASHIRU AIAGIZA BODI MPYA YA TAFICO KUIGEUZA TAFICO KUWA INJINI YA UCHUMI SEKTA YA UVUVIWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameitaka Bodi mpya ya pili ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kuhakikis...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu na mafunzo kwa vyuo vikuu pamoja na shule za sekondar...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014






























