HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

SPIKA NDUGAI ATEMBELEWA NA BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI TANZANIA LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Inmi Patterson, pale alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Inmi Patterson, pale alipomtembelea  leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale alipotembelewa na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania, wakiongozwa na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa Sarah Cooke(kulia kwake) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Sarah Cooke (wa pili kushoto) pale Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi kutoka Norway, Mheshimiwa Hanne Kaarstad (katikati) na Balozi kutoka Finland Mheshimiwa, Pekka Hukka (kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Ghasia (wa pili kulia) akiongoza kikao cha pamoja cha mashauriano kati ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja na Wadau wa Mashirika ya Maendeleo Duniani, kutoka Benki ya Dunia (World Bank) na Shirika la fedha la kimataifa (IMF) kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti na Wadau kutoka Mashirika ya Maendeleo Duniani wakiwa katika kikao cha Mashauriano ya pamoja kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASALIMIANA NA MABALOZI WA UINGEREZA NA MAREKANI LEO BUNGENI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini, Mheshimiwa Inmi Patterson kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa, Sarah Cooke kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WATEULE

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazunguzo na Mabalozi Wateule wanaoenda kuiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani.Mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma, yalijikita katika kujadili namna bora ya kuiwakilisha Tanzania ughaibuni kwa kuzingatia sera ya nchi ya mambo ya nje, kwa lengo la kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo, na kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi ya nchi yetu ikiwemo kutangaza shughuli za utalii zinazopatikana nchini. 
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisisitiza jambo 
Balozi Mteule Baraka H. Luvanda akichangia jambo wakati wa mazungumzo. Punde baada ya mazungumzo na Mhe. Naibu Waziri, Mabalozi walikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
Katibu Mkuu Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Aziz P Mlima akiongea na Mabalozi ofisini kwake mjini Dodoma 
Mazunguzo yakiendelea 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEWATAKA MABALOZI WA TANZANIA KUTANGAZA FURUSA ZA UWEKEZAJI TANZANIA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Mabalozi Wanane waTanzania Walioteuliwa hivi karibuni, Ambao Walifika Ofisini kwake Mjini Dodoma 21/April/2017 kumuaga kwa ajili ya kwenda Kuanza Kazi ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizo pangiwa Picha na PMO

BALOZI SEIF AKUTANA NA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA NCHI ZA NJE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mabalozi wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani hapo Ofisini kwa Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif wa kwanza kutoka Kushoto akibadilishana mawazo na Mabalozi hao ambao wa kwanza kushoto mwa Balozi Seif  ni Balozi Dr. Abdulla Possi anayekwenda Shirikisho la Ujerumani na Balozi Sylvester Ambukile anayeelekea Nchini Afrka Kusini.
Balozi Seif wa Tatu kutoka Kulia akiwa katika Picha ya pamoja na Mabalozi Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani mara baada ya kufanya nao mazungumzo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Balozi Sylvester Mabumba Comoro, Balozi Sylvester Ambukile Afrika Kusini na Balozi Omar Yussuf Mzee Algeria, na kushoto ya Balozi Seif ni Balozi Baraka Luvanda India na Balozi Dr. Abdulla Possi Shirikisho la Ujerumani. Picha na – OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mabalozi wanayoiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mataifa rafiki Duniani wana kazi ngumu na nzito ya kuinadi Tanzania katika Nchi hizo ili ipate kuungwa mkono katika harakati za kuimarisha Uchumi wake.


Alisema yapo maeneo na sekta kadhaa ambazo zimeshajengewa miundombinu imara kama Utalii, Mawasiliano, Kilimo, Biashara na Afya zinazohitajika kupata msukumo kwa mataifa rafiki na washirika wa maendeleo katika njia ya kustawisha maisha ya Wananchi na kuongeza pato la Taifa.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Mabalozi Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kuliwakilisha Taifa kwenye Mataifa mbali mbali Duniani walipofika kuaga rasmi wakijiandaa kuelekea kwenye vituo vyao vya Kazi.

Mabalozi hao aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar ni Balozi Sylvester Mabumba anayekwenda Visiwa vya Comoro, Balozi Baraka Luvanda anaelekea Nchini India, Balozi Omar Yussuf Mzee anakwenda kuanzisha Ubalozi Mpya waTanzania Nchini Algeria, Balozi Dr. Abdulla Posi anakwenda Shirikisho la Ujerumani na Balozi Sylvester Ambukile anayekwenda Nchini Afrika Kusini.

Balozi Seif Ali Iddi alisema kumalizika kwa vita Baridi Vikuu vya Pili vya Dunia ndani ya Karne ya 20 vilivyokumbwa na wimbi la Mataifa Makubwa kutaka kuendelea kutawala dhidi ya yale yaliyokuwa yakipigania Kujitawala kumeipeperusha Dunia hiyo kuelekea kwenye uchumi zaidi.

Alisema nafasi yao ya Kidiplomasia ni vyema wakaitumia katika ushiriki wao kwenye vikundi mbali mbali vya ushirikiano vinavyowapa fursa Wanadiplomasia hao kubadilishana mawazo na Taaluma ya jinsi ya kustawisha Uchumi na Maendeleo ya Mataifa yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Mabalozi hao Wapya wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi waliyoipata ambapo Rais wa Tanzania hakufanya makosa kutokana na vigezo tofauti alivyovitumia katika kuwapata kushika wadhifa huo.

Balozi Seif alitaja Nchi wanazokwenda Mabalozi hao za Shirikisho la Ujerumani, Comoro, Algeria, India, Afrika Kusini na Israel kwamba zimekuwa na uhusiano mzuri wa Kihistoria na Tanzania kiasi kwamba jukumu lao linapaswa kuzingatia udumishaji wa ushirikiano huo.

Alisema zipo nafasi za mafunzo ya Elimu ya Juu, Taaluma katika Sekta za Kilimo, Afya, Biashara na Utalii zinazopatikana katika Mataifa hayo kiasi kwamba Mabalozi hao watapaswa kuzifuatilia ili zilete tija kwa Vijana watakaopata Taaluma ya Kujenga Taifa lao.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Mabalozi wenzake Balozi Sylvester Luvanda anayeiwakilisha Tanzania Nchini India alisema wamethamini fursa ya uteuzi waliyopewa na Taifa na kuahidi kwamba watawajibika kwa nguvu zao zote.

Balozi Sylvester alifahamisha wazi kuwa inatia moyo na faraja kuona kwamba Nchi wanazokwenda kufanya kazi bado zina mafungamano mazuri ya ushirikiano wa Kidiplomasia na Tanzania.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

12/4/2017.


RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI PAMOJA NA MABALOZI WANNE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba(Wakwanza kulia) , Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni (Wakwanza kushoto) pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(Watatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma) na Mabalozi Pindi Chana(Wakwanza kulia walisimama mstari wa nyuma ) , Balozi Matilda Masuka(Wapili kutoka kulia waliosimama mstari wa nyuma), Balozi Abdallah Kilima(Wapili kutoka kushoto mstari wa nyuma) na Balozi Silima Kombo Haji (Wakwanza kushoto waliosimama) mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke aliyefika Ikulu kwa ajili ya Mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel Fred Kidega mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel Fred Kidega mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko  aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko  Ikulu 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao   Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amemshika mkono Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga  wakati akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao   Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akifurahia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga mara baada ya kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Rais Magufuli Awapangia Vituo vya Kazi Mabalozi Watatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wapya watatu ambao aliwateua tarehe 03  Desemba 2016.
 
Mabalozi hao waliopangiwa vituo ni Joseph Sokoine anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Omar Yussuf Mzee anayekuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Algeria na Grace Mgavano anayekwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ladis Komba nchini Uganda ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
 
Aidha, Balozi Sokoine ambaye anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Deodorus Kamala ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Balozi Mzee kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alishawahi kushika nafasi mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na nafasi ya mwisho alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya kwanza ya Rais Dkt. Ali Mohammed Shein.
 
Kwa upande wa Balozi Mgavano kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Ubalozi alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
 
Mabalozi wote waliopangiwa vituo vya kazi wataapishwa na Rais Ikulu jijini Dar Es Salaam leo  Jumapili tarehe 12 Februari 2017 saa tano asubuhi.