HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

EKA 17 ZA MASHAMBA YA BANGI ZAFYEKWA

Polisi Mkoa wa Arusha wameteketeza eka 17 za mashamba ya bangi katika Kata ya Kisimiri, wilayani Arumeru.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema mashamba hayo yalitekelezwa wakati wa msako maalumu.
 
Mkumbo alitoa onyo kwa wananchi wanauzunguka Mlima Meru ambao wamekuwa wakilima bangi kwa kisingizio kuwa, polisi hawawezi kufika.
 
“Kuna mtindo wa kulima bangi milimani hasa Mlima Meru, tunasema tutaendelea na msako kubaini wote wanaohusika,” alisema.
 
Aliwataka viongozi wa mitaa na madiwani kuwa makini na kudhibiti kilimo hicho haramu kwenye maeneo yao. Kamanda Mkumbo alisema kwa sasa umeanzishwa mtindo wa baadhi ya wananchi kuchanganya bangi na mazao mengine ili kupoteza ushahidi.
 
“Wanachokifanya sasa wanachanganya miche ya mazao na bangi, kwa hiyo inakua pamoja tutaendelea na msako huo kila kona lengo ni kuhakikisha kunakuwa na ukomo wa kilimo hicho cha dawa za kulevya mkoani hapa,” alisema Mkumbo.

DC DANIEL CHONGOLO AONGOZA OPARESHENI YA KUTEKETEZA MASHAMBA YA BHANGI EKARI 5 WILAYANI LONGIDO

Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Longido ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Godfrey Daniel Chongolo imeendelea na oparesheni ya kuteketeza madawa ya kulevya katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.

Sehemu ya Bhangi ikichomwa moto,kuhakikisha haichuliwi tena kwa matumizi mengine ya ulevi.

Mkuu wa wilaya ya Longido, Godfrey Daniel Chongolo akijiandaa kuanza kuongoza oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya Bhangi akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya pamoja na DC wa wilaya ya Longido, Mh Daniel Chongol ( pichani kulia) wakiendelea na oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya bhangi katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo mkoani Arusha

POLISI KILIMANJARO YANASA SILAHA,DAWA ZA KULEVYA NA VIROBA VILIVYOPIGWA MARUFUKU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandaizi wa Jeshi la Polisi ,Wilbroad Mutafngwa akionyesha silaha zilizomakamatwa pamoja na Dawa za Kulevya aina ya Mirungi na Bhangi.
Misokoto ya Bhangi iliyokamatwa.
Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa.
Silaha aina ya Bastola zilizokamatwa na jeshi hilo.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Kamanda wa Polisi,(hayupo pichani.)
Mfanyabiashara wa vinywaji kwa jumla ,Gerald Kimario akiwa amebeba boksi la Pombe iliyofungwa katika vifungashio vya Plastiki baada ya jeshi la Polisi kukuta bidhaa hizo katika ghala lake  la kuuzia bidhaa zake.
Mkaguzi wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Chakula na Dawa,William Mhifadhi akitizama Pombe iliyopigwa marufuku ikiwa katika vifungshio vya plastiki.
Sehemu ya Vifungashio vya Plastiki vya Pombe viivyoppigwa marufuku hivi karibuni.
Watuhumiwa wa matukio ya usafirishaji wa Dawa za kulevya pamoja na Unyang'anyi wakiwa mikononi mwa jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutfungwa akionesha gari lililokamatwa likiwa na mizigo ya Dawa za kulevya aina ya Milungi ,wahusika wakijaribu kuisafirisha.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

Vanessa Mdee Kaachiwa Kwa Dhamana

Mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu Vee Money ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kuwa ameshikiliwa kwa takribani wiki moja kufuatia tuhuma ya dawa za kulevya inayomkabili.

Mdee aliachiwa jana jioni ambapo anatuhumiwa kutumia na kusambaza dawa za kulevya. Alishikiliwa na Polisi tangu juma lililopita baada ya kwenda kuripoti kufuatia kutajwa kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa hizo iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam, Paul Makonda.

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA, JIJINI DAR

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga, wakati Kamishna huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya dawa za kulenya nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimuaga Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Madawa ya Kulevya: Vanessa Mdee ajisalimisha Polisi

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita.

Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.

Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa chini ya Lebo B'hitts.

VIGOGO WATANO WAHOJIWA KWA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA

 
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumkabidhi orodha ya majina 97 Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, sasa orodha hiyo imeanza kufanyiwa kazi kwakuwa vigogo watano waliopo kwenye orodha hiyo wameanza kuhojiwa.

Kamishna wa Intelijensia wa Mamlaka hiyo, Fredrick Kibula alisema Jumatatu hii kuwa wanawahoji na wanafanya uchunguzi dhidi ya watuhumiwa hao kabla ya kuwafikisha katika Mahakama.
Alisema, “Tuna watu muhimu watano wanaotoka katika orodha ile ya mkuu wa mkoa. Tunao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na muda ukifika tutawatajia mtawafahamu. “Hatukamati ovyo ovyo ni lazima tujiridhishe bila shaka kwamba wahusika wana sifa ya kukamatwa. Pia hatutangazi ingawa tunafanya operesheni za kiuchunguzi ambazo zinafanyika mara kwa mara.”
Tarehe 13, Februari wwaka huu,RC Makonda alimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rogers Sianga orodha ya majina 97 awamu ya tatu ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya.

AUDIO: Watuhumiwa 11,503 wa dawa za kulevya watiwa mbaroni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema jumla ya watuhumiwa  11,503 wa uzalishaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya wamekamatwa kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu nchini.


Akizungumza leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha kwanza tangu Serikali kuhamia mjini Dodoma, Majaliwa amesema katika kipindi hicho kesi za kujibu zilikuwa ni 9,811 ambapo watuhumiwa 941 walikutwa na kesi za kujibu huku 238 wakiachiwa huru na kesi 478 bado zinaendelea mahakamani.

Kuhusu pombe za viroba, Majaliwa  amesema oparesheni inaendelea katika mikoa mbalimbali baada ya kupigwa marufuku March Mosi mwaka huu na kwamba kupitia oparesheni hiyo wamegundua mambo mengine ikiwemo uwepo wa makampuni yaliyokuwa hayalipi kodi.

Kwa upande wa ajenda za kikao hicho cha mawaziri, Majaliwa amesema wizara zitatoa takwimu za watumishi wangapi waliohamia, idadi ya watumishi wote,  wamepanga awamu ngapi za kuhamia Dodoma .

==>Msikilize hapo chiniakiongea