HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI WATOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPTALI YA RUFAA YA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Maawenzi wakiwa  wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo
Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ,Boniface Lyimo akizungumza mara baada ya kuwapokea Madiwani hao na kutoa maelekezo ya namna ya kutoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,wakielekea katika wodi walimolazwa wagonjwa kwa ajili ya kutoa zawadi.
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema na Diwani wa kata ya Kiusa,Stephen Ngasa akikabidhi zawadi ya sabuni ya unga kwa wagonjwa waliolazwa katika Hopstali ya Mawenzi.
Diwani wa kata ya Mawenzi,Hawa Mushi akitoa zawadi kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Diwani wa kata Pasua ,Charles Mkalakala akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wagonjwa katika Hospitali hiyo.
Madiwani wakiongojea kuingia katika wodi nyingine kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali hiyo.
Madiwani wakitoa zawadi katika wodi ya wanawake Hospitali ya Mawenzi
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema,Stephen Ngasa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,awenzi mara baada ya kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi kwa wagonjwa pamoja na kusafisha mazingira katika Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema,Stephen Ngasa akiagana na katibu wa Hosptali ya Mawenzi ,Boniface Lyimo mara baada ya kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi na kusafisha mazingira ya hosptali hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

SAKATA LA POSHO ZA MADIWANI ARUSHA LAIBUKIA BUNGENI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Sakata la posho za madiwani wa Jiji la Arusha bado halijapoa, baada ya Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini kuliibulia katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), akisema linakwamisha ukusanyaji wa mapato. 

Sakata hilo liliibuka jana wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipitia na kuhoji hesabu za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/2015. 

Mbunge huyo alisema halmashauri hiyo imekata posho kwa madiwani na watendaji na kuzipeleka fedha hizo kwa walimu, jambo ambalo linawavunja moyo wawakilishi hao wa wananchi kutimiza majukumu yao. 

“Madiwani ndiyo wanawasaidia kuwahamasisha wananchi katika ukusanyaji wa mapato na hao mnawavunja moyo. Mkurugenzi hamuwezi kufikia malengo kama mtakuwa watendaji peke yenu,” alisema Selasini. 

Alisema halmashauri hiyo ikimaliza mvutano huo inaweza kuongeza mapato kutoka Sh12 bilioni hadi Sh18 bilioni na kujiendesha bila kutegemea ruzuku. 

Mbunge huyo alisema katika halmashauri zote nchini hakuna diwani anayelipwa posho ya Sh10,000, kwa nini madiwani wa jiji hilo pekee walipwe kiasi hicho. 

Akijibu hoja hiyo, mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Athuman Kihamia alisema hakuna diwani anayelipwa kiasi hicho cha fedha na kwamba, madiwani wote wanalipwa posho ya Sh40,000 kwa mwezi na nauli Sh10,000 kulingana na kanuni walizokubaliana mwaka 2003. 

Alisema madiwani hao walikuwa na posho zipatazo tano ambazo ni nauli, kujikimu, vikao, madaraka na mawasiliano.

Pia, Kihamia alisema walikuwa wakilipwa Sh150,000 za mafuta kinyume na kanuni walizokubali kuzitumia za mwaka huo. 

“Siwezi kurudia makosa kwa kulipa fedha zisizofuata kanuni na utaratibu, maana mtakuja kunihoji hapa kwa nini nimezilipa,” alisema. 

Mbunge wa Kwela (CCM), Ignas Malocha alimpongeza mkurugenzi huyo kwa kufuata misingi na utaratibu wa kanuni na sheria katika uendeshaji wa jiji hilo.

 Akizungumza nje ya kamati hiyo, Meya wa jiji hilo, Calist Lazaro alitaka liachwe lijiendeshe lenyewe bila kuingiliwa.

CHADEMA YALAANI DIWANI KUSWEKWA RUMANDE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Katibu wa CHADEMA jimbo la Arumeru Mashariki Elisa Stephen Mungure (Kulia) akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Embaseny Gadieli Mwanda (kushoto) nje ya Mahakama ya Mwanzo ya Enaboishu jana mara baada ya kuwekwa rumande kwa saa 48 na mkuu wa wilaya ya Arumeru ambapo jana alifikishwa mahakamani na kupewa dhamana


      Na Woinde Shizza, Arusha 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Wilaya ya Arumeru Mashariki kimelaani vikali kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexender Mnyiti kumuweka rumande Diwani wa Kata ya Embaseny Gadieli Mwanda kwa saa 48 na kudai kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya madaraka. 

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru Elisa Stephen Mungure amesema kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji dhidi ya viongozi wa upinzani ambao wamekua wakikamatwa mara kwa mara na kuwekwa rumande . 

Mungure alisema kuwa mbinu hiyo imekua ikitumika kwa hila ili kudhoofisha na kuua upinzani hivyo chama chake kimejipanga kukabiliana na hila hizo za kisiasa. 

“Diwani wa Kata ya Embaseny alitakiwa kuripoti katika kituo cha polisi cha Usariver septemba 20 mwaka huu ndipo alipokutana na Amri ya Mkuu wa Wilaya ya kuwekwa ndani kwa masaa 48 bila kuhojiwa ,jana alifikishwa mahakama ya Mwanzo ya Enaboishu na kutuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mradi wa Kuku Kukua ambao Diwani huyo siyo muhusika ,tunamshukuru Mungu amepata Dhamana” Alisema Mungure 

Akizungumza baada ya kupata Dhamana katika mahakama hiyo Diwani huyo Gadiel Mwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Arumeru Mashariki alisema kuwa Mkuu wa Wilaya alifanya ziara katika kata yake na kuzungumza na Wananchi ,baadhi ya watu ambao wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM walimshutumu kuwa anahusika na mradi huo alipotaka kujitetea alinyimwa nafasi hiyo na kuamriwa kufika kituo cha polisi asubuhi na mapema ndipo alipokutwa na masaibu hayo. 

Mwanda alisema kuwa misigano ya kisiasa inayotekea inalenga kuzorotesha juhudi za maendeleo ambazo amekua akizifanya kwa kushirikiana na wananchi jambo ambalo litawaathiri wananchi wengi hivyo amewataka wananchi kuendelea na juhudi hizo ikiwemo ujenzi wa zahanati ya kisasa. 

Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo Ester Swai na Agnes Elia wamesema kuwa kukamatwa kwa viongozi kila mara kunazua hali ya taharuki miongoni mwa wananchi hivyo wamezitaka mamlaka husika kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa.

DIWANI ASWEKWA NDANI KWA KUKIUKA MAADHIMIO YA BARAZA LA MADIWANI WILAYANI IKUNGI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kutoka Kushoto ni Eng Sadick Chakka Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.


Na Mathias Canal, Singida
Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke  Emmanuely Njingu (CHADEMA) kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati hiyo kutokana na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo ambalo limepelekea kuhamishiwa katika kamati nyingine.

Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa Diwani huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.

Mwanga amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.

Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya kuwa mjumbe wa kamati husika. Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada ya maridhiano ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine ya huduma za uchumi.

“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao vya kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu wote hazichagui upande mmoja” Alisema Mwanga

Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo kabisa tangu alipochaguliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa changemoto ya uhaba wa maabara, afya duni na miundombinu pia alizungumzia kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo ambalo linairudisha nyuma Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014 ilikuwa na Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.

Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi 631,455,000 lakini makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka ulimalizika kwa kukusanya 173,899,828.

Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri iliyopangwa ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000 hivyo kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji.

Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo kumesababishwa na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato hii ikiwa ni kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.

Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa, taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo ya kuifanya Ikungi kukua kiuchumi .


MADIWANI WA UKAWA WASUSIA KIKAO CHA PAUL MAKONDA KWA MADAI KWAMBA ANAWADHARAU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Madiwani wa Ukawa wa Manispaa ya Kinondoni wamesusa kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kiongozi huyo hana uhusiano mzuri na viongozi wa upinzani. 

Jana, Makonda aliitisha kikao cha wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara za manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na madiwani wote, wakiwamo wabunge wanaounda halmashauri hizo.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Arnaoutoglou kililenga kuzungumzia masuala mbalimbali, kama maeneo yaliyovamiwa na uboreshaji wa elimu mkoani Dar es Salaam. 

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema Makonda amekuwa na tabia ya kudharau na kutoheshimu viongozi wenzake, hasa wa upinzani akiwaona hawatendi kazi vizuri. 

Pia, Jacob alidai kuwa Makonda amekuwa na tabia ya kuingilia kazi zinazofanywa na viongozi wengine kwa kutumia cheo cha ukuu wa mkoa, jambo ambalo meya huyo alisema ni kinyume cha sheria. 

“Akitaka tumpe ushirikiano, Makonda abadilike la sivyo mtindo utakuwa huuhuu, mambo yatakuwa hivi. Huu ni mwanzo na ndiyo maana leo (jana) Ukawa Kinondoni tumekuwa na msimamo mmoja,” alisema Jacob. 

Jacob, ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chadema), alisema hawakuona umuhimu wa kwenda katika kikao hicho kwa sababu kiongozi wa mkutano huo anawadharau. 

Akijibu tuhuma hizo, Makonda alisema madiwani waliohudhuria kikao hicho maeneo yao yalikuwa na shida na yanahitaji kushughulikiwa, hivyo si kazi yake kuhesabu watu na kubaini nani hakufika mkutanoni. 

Alisema ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kuvirudisha viwanja vilivyochukuliwa na kuvirejesha kwa matumizi yaliyokusudiwa. 

“Huyo anayelalamika mwambie huo anaoufanya ni utoto akikua ataacha. Narudia tena siyo kazi yangu kuangalia nani hajaja kwenye kikao,” alisema.

Kwenye kikao hicho, meya wa Ilala (Chadema), Charles Kuyeko alikuwapo kwenye mkutano huo pamoja na madiwani wenzake, sambamba na wale wa Temeke. 

Makonda si mgeni wa tuhuma .Aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kionondoni katika kipindi ambacho alikuwa akituhumiwa kuhusika kwenye sakata la kupigwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba kwenye mdahalo wa Katiba uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl. 

Katika kipindi hicho, Makonda pia alikuwa akituhumiwa kumrushia tuhuma za ufisadi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiahidi kuwa CCM isingempitisha kugombea urais. 

Akitoa majumuhisho ya kikao cha jana kilichoanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi, Makonda aliwataka watu waliovamiwa na kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, kuanza kubomoa majengo yao kabla ya Serikali kuwafikia. 

Kabla ya kutoa majumuisho hayo, Makonda alitoa nafasi kwa madiwani wa manispaa hizo kueleza kero zinazowakabili, hususan zinazohusu ardhi. 

“Najua mchakato huu utawagusa hadi vigogo, lakini mimi siogopi vita kwa sababu ndani yangu ninaongozwa na Mungu pekee,” alisema Makonda. 

Mbali na hilo, Makonda alisema endapo mtendaji wa ardhi atayebainika kuhusika katika kuchezea michoro na ramani ili aachie ardhi na kujipatia fedha, atashughulikiwa kwa mujibu sheria. 

Katika hatua nyingine, Makonda amemwagiza kamishna msaidizi wa ardhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mathew Nhange kumwambia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi awaondoe maofisa ardhi na mipango miji wa Kinondoni na Ilala baada ya kushindwa kutoa taarifa za kuridhisha katika mkutano huo. 

Huku akiwataja maofisa hao wanaotoka Kinondoni na Ilala, Makonda alisema alishakutana na wakuu wa idara kwenye vikao vilivyopita, hivyo alitegemea kuwa watumishi hao wangetoa taarifa zilizokamilika. 

Kamishna naomba umwambie katibu mkuu mimi siwataki watumishi hawa katika manispaa hizi. Mwambie awatoe na kuwapangia kazi nyingine,” alisema Makonda. 

Kamishna Nhange alisema agizo hilo analifanyia kazi na kwamba atampa katibu mkuu taarifa za watumishi hao jana.

MBUNGE NASSARI NA MADIWANI 28 WA CHADEMA WAFUTIWA KESI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


SERIKALI kupitia Ofisi ya Mwendesha Mashitaka (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imetakiwa kufanya utafiti wa kina katika mashauri inayoyafungua mahakamani.

Kauli hiyo ilitolewa mjini Arusha jana na Wakili wa Kujitegemea, Charles Abraham, aliyekuwa akiwawakilisha watuhumiwa 29 katika kesi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) na madiwani 28 wa chama hicho wakituhumiwa kuvunja uzio wa thamani ya Sh milioni saba.

Akizungumza nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya Hakimu Mkazi, Desder Kamugisha kuifuta kesi hiyo, Wakili Abraham alisema uamuzi huo ulitolewa baada ya Serikali kukosa ushahidi.

“Ni rai yangu kwa Serikali  kwamba iwe inafanya utafiti katika mashauri inayoletewa kabla haijapeleka kesi mahakamani. Hii itasaidia kuondoa gharama zisizo za lazima na usumbufu kwa watu na jamii wakiwamo viongozi,” alisema Wakili Abraham.

Awali, mahakamani hapo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Blandina Msawa, uliwasilisha ombi la kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo, hivyo ulimuomba hakimu huyo kuiondoa  hoja ambayo ilikubaliwa na upande wa utetezi.

Akitoa uamuzi wa kuifuta kesi hiyo, Hakimu Kamugisha alisema kwa vile upande wa mashitaka umeamua kuiondoa kesi hiyo, mahakama haitakuwa na kipingamizi.

Mbunge Nassari akizungumzia kufutwa kwa kesi hiyo, alisema ilifunguliwa kisiasa badala ya kuangalia maslahi ya mali za Serikali.

Naye Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Yona Nnko ambaye mwaka jana alihamia Chadema, alimpongeza Nassari na madiwani kwa kufanikiwa kupigania haki ya wananchi wa Arumeru Mashariki.

Nassari na madiwani hao walifunguliwa kesi hiyo na Jamhuri wakidaiwa kuharibu mali ya Itandumi Makere katika eneo la Usa River.

MADIWANI WA KYERWA NA BIHARAMULO MKOANI KAGERA WAPEWA SOMO LA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA FEDHA ZA SERIKALI ZA MITAA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwezeshaji kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Magdalena Katunzi akiwasilisha mada ya uzimamizina Udhibiti wa fedha katika Mamlaka za serikali za mitaa. Mada hiyo ilitolewa kwa madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Kyerwa na Biharamuo Mkoani Kagera leo.
Lengo kuu la mada hiyo kwa Madiwani ahao ambao halmashauri zao zimechaguiwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma ni pamoja na kumuwezesha Diwani kupata taarifa na uweewa juu ya taratibu za usimamizi na udhibitiwa fedha katika Mamlaka za Serikali za mitaa.

Aidha Katunzi alianisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya mapato vya Mamlaka za serikali za Mitaa, ikiwa ni mapato ya ndani, ruzuku kutoka serikali kuu na Mikopo. 

Madiwani walifundishwa mbinu za kuongeza mapato ya Hamashauri ambapo walifundishwa namna ya kubuni na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato, kuboresha viwango vya tozo, kuboresha mbinu za ukusanyaji mapato, kusimamia matumizi ya fedha za serikali ya mitaa na udhibiti wa fedha za Halmashauri.
 Madiwani kutoka Hamashauri za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo wakifuatilia mada hiyo ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha za Mamlaka ya Serikali za mitaa.
 Wakuu wa Wiaya za Kyerwa na Biharamulo mkoani Kagera, Kanali Mstaafu, Shaabn Lissu (kushoto) wa Kyerwa na Saada Malunde wa Biharamulo wakiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Wende Ng'ahala (kulia) wakifuatilia mada hiyo.
Madiwani kutoka Hamashauri za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo wakifuatilia mada hiyo ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha za Mamlaka ya Serikali za mitaa.

 Ofisa Mipango wa Wilaya ya Biharamulo, Andambike Kyomo akifafanua jambo kuhusu namna ya ugawaji wa fedha za Halmashauri kwa makundi ya Vijana, Wanawake na matumizi mengine.
 Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akifafanua jambo kuhusu mada hiyo na maswali yaliyoulizwa na washiriki.
Madiwani kutoka Hamashauri za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo wakifuatilia mada hiyo ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha za Mamlaka ya Serikali za mitaa.
 Ili kuondoa uchovu kwa washiriki kunakosababisha kusinzia wakati wa mafunzo, washiriki walifanya mazoezi kuchangamsha mwili na kuimarisha usikuvu.
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde (kulia) akifurahia kuonana na Mkurugenzi Mpya wa Hlamashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Wende Israel Ng'ahala. Watendaji hao ndio walioonana kwa mara ya kwanza na wote ni wapya katika Wilaya hiyo.  Source:Father Kidevu Blog, Kagera

MADIWANI WA HALMASHAURI ZA KYERWA NA BIHARAMULO WAANZA MAFUNZO YA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deusdedith Kinawiro akifungua mafunzo ya siku nne ya Madiwani kutoka Hlamashauri mbii za Kyerwa na Biharamuo juu ya namna ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma (PS3) chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekali kupitia shirika ake la misaada la Kimataifa (USAID) ikishirikiana na serikali kuu.

Mradi huo ulizinduliwa Julai 12 mwaka huu ambapo Halmashauri hizo mbii ndio zitatekeeza mradi huo mkoani Kagera kwa awamu ya kwanza.

Kinawiro alisema anatarajio kuona mafunzo haya elekezi yanatumika kama ilivyokusudiwa, na waheshimiwa madiwani wanapata uelewa na maarifa kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu na majukumu yao katika kusimamia uendeshaji wa Mamlaka hizi.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali (Mstaafu), Shabaan Lissu akiwa na Mkuu wa Wiaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya madiwani yaliyofanyika mjini Bukoba leo.
 Mwenyekiti wa Hlamashauri ya Kyerwa, Kashunju Runyogote (kushoto) akiwa na madiwani wenzake wa Kyerwa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
 Baadhi ya Madiwani na Watendaji wa Hamashauri za Kyerwa na Biharamuo mkoani Kagera wakifuatilia ufunguzi huo.
 Kiongozi wa timu ya Uzinduzi ya PS3 Mkoani Kagera na Mtaalam wa Fedha wa Mradi huo wa PS3, Abdul Kitula akizungumza juu ya mafunzi hayo kwa madiwani.

Kitua aliwataka watendaji hao kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ambayo ndio utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za  Umma ambao nchini unatekelezwa katika mikoa 13 na kuzinufaisha Halamashauri 93.
 Madiwani kutoka Hamashauri za Kyerwa na Biharamuo wakimsikiiza Kitula wa PS3.
 Mwenyekiti wa mafunzo hayo, Ernest Kausa akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake.
 Wawezeshaji kutoka Mradi wa PS3 wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
 Magdaena Katunzi kutoka PS3 akitoa maelekezo ya namna mafunzo hayo yatakavyofanyika pamoja na mada zitakazo tolewa.
Maofisa wa Halamashsuri wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
 Madiwani kutoka Halmashauri mbaimbali wakielezea Matarajio yao baada ya mafunzo hayo jinsi yatakavyo badilisha utendaji wao wa kazi.
 Mtaalam wa Masuala ya Tafiti Tendaji kutoka PS3 Aloyce Maziku akiendesha mafunzo kwa madiwani.
 Wajumbe wa kamati ya Utendaji ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT) kutoka kushoto, Mstahiki Meya wa Jiji a Tanga na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya ALAT Taifa, Seleboss Mustafa, Mstahiki Meya Manispaa ya Tabora,Leopold Ulaya na Mwenyekiti wa Halamashauri ya Bariadi na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya ALAT, Robert Mgata
Mtaalam wa Masuala ya Utawaa Bora wa Mradi wa PS3, Pau Chikira akiwasiisha mada ya Utawaa bora na Ushirikishwaji wa wananchi wakati wa mafunzo hayo.


 Madiwani wakifuatilia mada kwa umakini.

Mwezeshaji kutoka PS3, Lazaro Kisumbe  akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
 
Washiriki wakifuatilia mada hiyo.
 Maofisa wa PS3 wakijadiliana jambo.
Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka TAMISEMI, Bertha Swai akifafanua jambo.
 Picha ya pamoja kati ya Mgeni rasi na madiwani wa halmashauri zote mbili.
Picha ya pamoja kati ya Mgeni rasmi na maofisa wa PS3.