HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA HAI ASHIKILIWA NA POLISI KWA SAA TANO BAADA YA KUMALIZA KIKAO CHA BARAZA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Helga Mchomvu akieleka kito cha Polisi huku  akisindikizwa ana askari Polisi.
Mwenyekiti wa Halmahauri ya wilaya ya Hai ,Helga Mchomvu akiingia kituo cha Polisi Bomang'ombe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Hela Mchomvu (Kulia) akiingia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kwa ajili kuongoza kikao cha baraza hilo.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yahana Sintoo.
Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Hai,Hela Mchomvu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,Yahana Sintoo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Baadhi ya Madiwani wanaounda baraza la Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo.
Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao cha baraza hilo.
Diwani Harry Masakia akisoma kanuni za kudumu za Halmashauri wakati wa kikao cha baraza hilo.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akitoka nje ya ukumbi wa mikutno baada a kuhairisha kikao cha baraza hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,akizungumza na askari Polisi waliokuwa nje ya ukumbi wakimsubiri kwa ajili ya kumfikisha kituo cha Polisi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akiongozana na askari Polisi wakati akilekea ofisini kwake.
Askari Polisi wakiomngojea Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu nje ya ofisi yake .


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Meya wa Ubungo achukuliwa na polisi

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hata hivyo sababu za kuchukuliwa kwake bado hazijawekwa wazi.
Tukio limetokea leo Jumatatu saa sita mchana katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Kibamba.
Askari wapatao wanne wakiwa katika gari aina ya Land Cruise walifika katika eneo hilo kisha kuzuia msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa tayari kuanza ziara ya kutembelea manispaa hiyo.
Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.
Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.
"Tunakuomba uongozane na sisi hadi kituoni tuna maongezi na wewe yasiyozidi dakika 10 tukiridhika tunakuachia uendelee na shughuli zako,"
Baada ya kumweleza hayo, ofisa huyo alikwenda moja kwa moja katika gari la Sumaye na kumweleza kuwa wanamuhitaji meya kwa dakika 10 kisha watamuachia.

Meya wa jiji amtembelea Mjane wa Bob Makani nyumbani leo

Inline image 1
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akimfariji Mjane wa aliyekuwa mhasisi na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bob Makani (Mama Makani)
Inline image 2
Mjane wa aliyekuwa mhasisi na Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kaboga Makani akimueleza jambo Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mara baada ya kumtembelea Nyumbani kwake mapema leo asubuhi.
Inline image 3
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwa kwenye picha ya pamoja na familia ya Mahasisi na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chadema Bob Makani, wa kwanza kulia ni mtoto wa mzee Makani , Mohamed Mkani, na katikati ni mke wa Bob Makani Kaboga Makani.
Inline image 4
Inline image 1
Inline image 2


Meya wa jiji la Dar es Salaam akiwa na familia ya Mjane wa aliyekuwa muwasisi na Katibu mkuu wa kwanza wa Chadema.
Inline image 3
Inline image 4

Picha zote na Christina  Mwagala, OMJ.



NA CHRISTINA MWAGALA, OMJ
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amemtembele mjane wa aliyekuwa Mhasisi na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bob Makani , Mama Kaboga Makani ikiwa ni moja ya ziara zake za kutembelea wazee pamoja na viongozi ambao waliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Meya ambaye amerejea Nchini jana kutoka Nchini Iran ambapo alikuwa kwa ziara ya kikazi ya siku 10, amesema kwamba hatua ya kutembelea viongozi pamoja na wazee ambao ni waasisi inalenga kutambua michango yao katika nafasi ambazo waliwahi kutumikia na kwamba busara zao pia ndio zimeweza kulifikia Taifa sehemu ilipo hivi sasa.

Alifafanua kuwa Bob Makani enzi za uhai wake alikuwa ni mmoja na mwasisi wa Chadema na kwamba anatambua mchango wake kutokana na juhudi alizozionyesha ikiwemo kukipigania chama hadi kufikia kilipo hivi sasa.

Alisema Bob Makani pamoja na wenzake ndio waliokianzisha Chama Cha Chadema na kufika mbali zaidi kwamba bila wao hata yeye asingekuwa Meya wajiji hili kupitia chama hicho na kwamba mchango wao ndani ya chama bado utaendelea kukumbukwa na kila mmoja wakiwemo wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla.

Alisema Bob Makani mbali na kuwa mwanachama na mwasisi wa Chadema lakini pia aliwahi kuwa Gavana wa Benki kuu ambapo alitumikia nafasi hiyo kwa na hivyo baada ya kustaafu nafasi hiyo aliamua kuanzisha chama na hivyo kuwepo hadi hivi sasa.

“ Haya sio mambo ya kisaisa , lakini unaweza kuona kwamba ni alikuwa mtu muhimu , lakini pia kama kijana wao lazima nipate basara kutoka kwao, ingawaje hatunaye tena hapa duniani, lakini huko alipo anaona jambo gani ambalo tunafanya kama vijana ambao alituacha ndani ya chama” alisema.

Alifafanua kwamba jambo la kutembelea viongozi ama waasisi wa nafasi chama sio jambo la kisiasa bali ni kutokana na kutambua mchango wakazi ambazo waliwahi kuzifanya wakati huo.

“ Ziara hii sio ya kwa Mzee Makani tu, ila ni kwa waasisi , na wale ambao waliwahi kuwa viongozi wa jiji, wapo nitawatembelea, ikiwa ni sehemu yangu pia ya kutambua mchango wao, sambamba na kupata baraka , busara zao ambazo walizitumia katika uongozi wao, ukizungumza vizuri na wazee hawa unapata baraka na kuona kwamba namna gani unaweza kuwaongoza wananchi” alisema Meya Mwita.

“ Nimekuja leo kumuona Mama yetu, naweza kusema ni mama yetu kwa sababu kila mmoja anamfahamu mzee Makani , alikipigania chama, na ndio katibu mkuu wa wa kwanza ndani ya Chadema, kama vijana hatuna sababu ya kuwasahau wasisi wetu, wazee wetu, watu ambao tunawatambua kabisa waliitumikia nchi yetu” alisema Meya Isaya.

MD KAYOMBO: YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Aliyesimama) Boniface Jacob akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya
Wenyeviti wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichoendeshwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Boniface Jacob ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Picha zote na Nassir Bakari)

Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa kikao

kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na Afisa Utumishi wa manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma akishauri jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo

Usikivu ni jambo la busara kikaoni
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa ya Ubungo.

Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewataka wenyeviti wa Mitaa iliyopo katika Manispaa hiyo kutumia vyema nafasi zao za uongozi kwa kuwatumikia wananchi kwa haki huku akiwasihi kuishauri serikali katika majukumu yake ili kuwa na maendeleo chanya katika maeneo yao sawia na kupunguza lawama za mambo yaliyopita ili kuwa na Manispaa imara yenye ukusanyaji mzuri wa mapato.

MD Kayombo amewasihi wenyeviti hao kuwa na mahusiano mazuri baina yao na maafisa watendaji wa Mitaa kwani kufanya kazi kwa Ushirikiano na Upendo ndio silaha pekee ya kuimarisha utendaji na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Mitaa.

MD Kayombo ameyasema hayo Wakati wa kikao cha kazi pamoja na wenyeviti wa Mitaa kilichokuwa na dhamira ya kushauriana namna bora ya kuimarisha mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuwa na uchumi imara, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Mtaa wa Kibamba CCM na kuhudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa atazuru kata hadi Kata ili kubaini wapi kumwepwaya na kipi kipaombele katika maeneo husika ili kuanza nayo katika kuimarisha maendeleo ya wananchi.

Hata hivyo wenyeviti wote wamekabidhiwa Bendera, Rejista, Vitini vyenye miongozo ya kisheria sambamba na vitini vinavyobainisha majukumu ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ili kutoingiliana katika utendaji na viongozi wengine wakiwemo watendaji wa Mitaa na Kata.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa wenyeviti wanapaswa kuwasimamia vyema wananchi kulipa kodi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya Manispaa kujisimamia yenyewe na kujiendesha kirahisi.

Mstahiki Meya ametumia Kikao hicho kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg John Lipesi Kayombo kwa uongozi wake imara na uliothubutu kwani umewafanya wananchi katika Manispaa hiyo kuwa walipaji wazuri wa kodi.

Jacob amesema kuwa mipango ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni kuifanya Manispaa hiyo kuwa ya mfano na kuzishinda Manispaa zingine katika Jiji la Dar es salaam.

Kuhusu Posho za wenyeviti wa Mitaa, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo amewasihi wenyeviti kuwa na subira kwani wanaandaa mpango imara kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ili kuwalipa malimbikizo ya posho zao zote wanazodai.

Pia amewasihi wenyeviti hao kutumia Uhuru wao kikatiba kuwafungulia kesi wale wote wanaowaonea, kuwazalilisha na kuwakejeli kwa kuwafungulia kesi katika mahakama kwa mujibu wa sheria.

MEYA ILALA AFUNGUA RASMI DARAJA LA BONYOKWA-KINYEREZI

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akihutubia wananchi baada ya kufungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.

Mwandishi wetu
MSTAHIKI MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko jana alifungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku alisema  daraja hili limejengwa kwa takribani mwaka mmoja na kugharimu Tsh.million  478 hadi kukamilika kwake leo hii. Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku nyingi kutokana na sababu mbali mbali lakini kutokana na usimamizi imara wa Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Charles Kuyeko sasa historia imebadilika.

Meya Kuyeko akizungumza na umati wa wananchi waliokusanyika kushuhudia ufunguzi huo amewasitiza kulilinda na kulitunza vyema daraja hilo kwani limejengwa kwa kodi zao.

Awali, Meya akitoa historia ya daraja hilo amesema kuwa, waliokuwa wanatakiwa kujenga daraja hilo ni wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) lakini kutokana na kusuasua kwao, Mimi (Meya)  niamua kuingilia kati kwa Manispaa kutenga Fedha kujenga daraja la muda ili kuwasaidia wananchi wa Bonyokwa kuondokana na atha ya kuwa Kisiwa hususani wakati wa Mvua.

Kuyeko ambaye pia ni Diwani wa kata ya bonyokwa amewaambia wananchi hao waliofurika kwenye uzifunguzi huo kuwa huo ni mwanzo tu wa utekelezaji wa ahadi zake katika kutatua kero za wananchi na wapiga kura wake. "Nawahakikishia kuwa hamtajutia kunipa kura zenu kwani daraja hili imekuwa kero ya miaka nenda rudi lakini Mimi nimeimaliza kwa muda mfupi kwa kushirikiana na watendaji wangu hivyo mtarajie mengi kabla mwaka huu kuisha hata daladala zitakuwa zinafika hadi kisiwani".

Mbali na hayo,Meya amewaahidi wananchi hao muda mfupi ujao atatatua kero ya maji na barabara kama ambavyo aliahidi kutekeleza wakati wa kampeni.

Ufunguzi huo ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali na kisiasa akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest, madiwani wa kata mbalimbali na viongozi wa vyama vya siasa.

Akitoa salam kwa niaba ya viongozi wa vyama vya siasa, Dk.Makongoro Milton Mahanga mbunge wa zamani jimbo la Segerea ambaye kwa sasa ni, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Ilala alisema, "Tangu niwe kiongozi sijawahi kuona kiongozi mahiri kama Meya Kuyeko. 

Ameweza kuwaunganisha viongozi wa Manispaa yake na kuwa kitu kimoja, na hadi sasa ameshafanya vitu vingi ambavyo awali vilishindikana nakupongeza sana Meya Kuyeko.

Dkt. Mahanga  aliwasisitiza wananchi kuwaamini viongozi wanaotokana na UKAWA kwani ni wazuri jifunzeni kwa Kuyeko mambo makubwa anayoyafanya. Kwa niaba ya Chadema nampongeza sana Meya Kuyeko kwa kukiwakirisha vyema  chama kwa wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Segerea ndugu Gango Kidera aliwataka wananchi wa Bonyokwa  waendelee kumwamini na kumuunga mkono Meya Kuyeko, Baraza lake la Madiwani kwani amekuwa mfano bora kwa kutekeleza ahadi zake zinazotokana na ilani na Sera za Chadema/UKAWA. 

Chadema imemtuma Kuyeko kuwatumikia wananchi wa Bonyokwa na Manispaa nzima ya Ilala kwa kuhakikisha anatatua kero zao kwa spidi ya mwendokasi na leo tumeona anatenda kwa maslahi ya wananchi. Nakupongeza sana Meya Kuyeko, alisema Kidera

Viongozi wengine waliozungumza katika ufunguzi huo ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest ambaye aliwapongeza wananchi wa Bonyokwa kwa kumchagua Kuyeko, wananchi wa Bonyokwa mlifanya maamuzi sahihi kuchagua Chadema kwa sababu bila Chadema Meya Kuyeko tusingempata. 

Anatropia pia alimpongeza Meya Kuyeko kwa kuendelea kutatua kero za wapiga kura wa Bonyokwa siku hadi siku na Ilala kwa ujumla. UKAWA kwa Manispaa ya Ilala chini ya Meya Kuyeko imeleta matumaini makubwa kwani wakazi wa Manispaa wapatao 1,415,443 walikuwa wamekata tamaa kabisa kwani viongozi waliopita walishindwa kutatua kero za wananchi, hivyo UKAWA chini ya Meya Kuyeko ni mfariji mkuu wa wananchi, alisema Anatropia.

Diwani wa Buguruni Mhe. Penza wa CUF akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Ilala alisema ilani ya UKAWA imeweka vipaumbele kwenye Barabara, maji, afya, elimu, na masoko na mitaji hivi vyote vinafanyika.

Meya Kuyeko aliwashukuru wananchi kwa kuendelea kumwamini na kumpa ushirikiano wa karibu hali ambayo inampa ari ya kuwatumikia kwa nguvu zake zote. Pia amekishukuru chama chake Chadema, viongozi, Madiwani na watendaji wote wa Manispaa ya Ilala wakiongozwa na Mkurugenzi kwa kumpa ushirikiano wa hali na Mali katika kuwatumikia wananchi.

MAABARA YA KISASA YA KOMPYUTA YA SHULE YA SEKONDARI MIKOCHENI YAZINDULIWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meya Mstaafu wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda.

 Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya intaneti ya Raha Broadband, Aashiq Shariff na Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta.
 Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akimuuliza jambo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikocheni aliyekuwa akitumia kompyuta baada ya ufunguzi rasmi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule hiyo, Dar es Salaam juzi. Kushoto kwake ni Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta na Meya Mstaafu wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda (kushoto) wakimtazama mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Jamila Msami akitumia kompyuta baada ya ufunguzi rasmi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya shule hiyo kwa ufadhili wa Kampuni ya intaneti ya Raha Broadband, Dar es Salaam juzi.
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta (wa pili kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Raha Broadband, Aashiq Shariff (wa pili kushoto) na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Bethel Kimei (Mama Langa).

Saw Na Mwandishi Wetu, 
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda ameitaka jamii kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kuboresha Sekta ya elimu kwa kuchangia maendeleo ya elimu ili kuleta mabadiliko ya elimu nchini.

Meya huyo Mstaafu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam kwa udhamini wa kampuni ya intaneti ya Raha Broadband kwa kushirikiana na yeye mwenyewe hivi karibuni.
Hiyo inakuwa ni miongoni mwa Maabara chache bora za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini kwa shule za Umma.
Mwenda aliutaka uongozi wa shule hiyo kuitunza maabara hiyo na kuitumia vizuri ili faida yake ionekane kwenye matokeo ya mitihani ya shule hiyo.
"Tukubaliane kuwa mtaitunza maabara hii vizuri ili umuhimu wake uonekane katika matokeo ya mitihani ya wanafunzi". Alisema Mwenda.
Aidha aliishukuru kampuni ya Raha Broadband kwa kuchangia kompyuta na vifaa pamoja na huduma ya intaneti kwa kila mwezi vyenye thamani ya shilingi milioni 18 na kuwataka viongozi wa Manispaa hiyo kuwashawishi wananchi nao kuchangia maendeleo ya elimu kwa shule za Manispaa hiyo.
Kwa upande wake Meya huyo Mstaafu alichangia shilingi milioni 3.9 ikiwa ni ukarabati wa Chumba cha maabara, madirisha, milango pamoja na meza za kompyuta.
Naye Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta alimshukuru Meya huyo Mstaafu pamoja na kampuni ya Raha kwa mchango wao na kuomba waendelee kumsaidia kwa shule nyingine za Manispaa hiyo.

UKAWA YASHINDA UMEYA UBUNGO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akizungumza baada ya kichaguliwa nafasi hiyo kushoto ni Naibu Meya wa manispaa hiyo Ramadhani Kwangaya na kulia ni mkurugenzi wa manispaa hiyo John Kayombo. (Picha na Loveness Bernard)

Diwani wa Kata ya Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Boniface Jacob ameshinda nafasi ya Umeya Manispaa ya Ubungo katika uchaguzi uliofanyika leo baada ya ule wa awali kuhairishwa. Amepata jumla ya kura 16 za UKAWA na Mgombea Wa CCM kura 2 huku Naibu Meya wa UKAWA akishinda kwa kura 15 dhidi ya kura 3 za CCM.

MANISPAA YA KINONDONI YAVUNJWA RASMI, MEYA BONIFACE KAPOTEZA NAFASI YAKE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amevunja Baraza la Madiwani rasmi baada ya serikali kuigawa manispaa hiyo kuwa mbili. Kagurumjuli alilivunja juzi saa 11:00 baada ya kumalizika kwa Baraza la Madiwani la kawaida.

Alipokuwa akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo.
“Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema.
Aliongeza kuwa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi wa meya katika manispaa hizo.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni alikuwepo kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo ni Boniface Yakob ambaye amebaki nafasi yake ya udiwani.

Kuvunjwa kwa baraza hilo kulikuwa kunatarajiwa baada ya serikali kugawanya manispaa ya Kinondoni kuwa mbili.