HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MASAUNI ATANGAZA MAJINA YA WATUHUMIWA 16 WA MAUAJI YANAYOENDELEA KIBITI, MKURANGA NA IKWIRIRI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha baadhi ya picha za watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP),Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.

MASAUNI AZINDUA MPANGO WA KUWASAIDIA WAKIMBIZI NA NCHI ZINAZOHIFADHI WAKIMBIZI, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke. 
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi  Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
 Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini  pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MASAUNI AFUNGUA GEREZA LA WANAWAKE MPWAPWA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akishirikiana na Viongozi wengine kufungua Gereza  la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa  kushirikiana na wafungwa.Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mheshimiwa George Lubeleje , akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,Mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia), akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa (kulia) kuelekea katika eneo lilipo  Gereza la Wanawake Mpwapwa, lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Wananchi wa Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni  askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu, MOHA
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi ya askari  wa jeshi hilo hapanchini.
Akizungumzia changamoto za Makazi ya askari wa Jeshi la  Magereza Nchini, wakati wa uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema Serikali inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.
“Nawaomba  askari wetu nchi nzima  wawe na subira  Serikali inatambua na  inashughulikia changamoto ya makazi ya  askari na tayari tuko katika mazungumzo na wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 9500, lengo ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na familia zao,” alisema Masauni.
Awali akitoa maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu ambao ni askari Magereza kwa  kushirikiana na wafungwa kama sehemu ya utekelezaji wa  amri ya Mh. Rais Dk. John Magufuli ya kutaka wafungwa watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo kilimo,ujenzi na ufundi mbalimbali.
Ujenzi wa Gereza hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia  kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la Kongwa mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa  ndugu wa wafungwa kusafiri mpaka wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.

WAZIRI NCHEMBA AWASILI ENEO YALIPOTOKEA MAUAJI YA POLISI WANANE

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewasili eneo yalipotokea mauaji ya askari wanane katika kijiji cha Jaribu, Wilayani Kibiti.
Waziri Nchemba ameambatana na naibu wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.
Nchemba atatembelea kambi za askari polisi wa kanda ya Pwani na katika kata ya Bungu wilayani Kibiti.

MASAUNI AHITIMISHA ZIARA YAKE MIKOA YA KUSINI KWA KUTEMBELEA GEREZA LA KILIMO NA MIFUGO LAMAJANI, WILAYANI MASASI, MKOA WA MTWARA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Seleman Mzee, wakati alipokuwa anawasili wilayani humo, Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia), kuingia Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasikwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anamfafanulia jambo mara baada ya kutoka ndani ya Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anatoa maelezo kuhusu Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi. Gereza hilo lina wafungwa zaidi ya 60 ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. Kikao hicho kilifanyika ofisi ya Mkuu wa Gereza hilona kuhudhuriwa na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo vilivyo chini ya wizara yake pamoja na viongozi wa wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiiangalia moja ya nyumba za askari magereza zilizopo jirani na Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa huo (RPO), Ismail Mlawa. Kushoto ni Ahmed Bakari, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo. Masauni alimaliza ziara yake ya mikoa ya kusini kwa kutembelea Gereza hilo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MASAUNI ALIAGIZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUANZISHA KITUO CHA ZIMAMOTO WILAYANI RUANGWA MWEZI UJAO, MAANDALIZI UJENZI WA KITUO KIPYA CHA POLISI

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi pamoja na Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya Wizara yake mkoani humo.  Katika mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuanzisha Kituo cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu pamoja maandilizi ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauniakimpa maelekezo Fundi Mkuu wa ujenzi wa Gereza Ruangwa (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo unaoendelea mjini Ruangwa. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Tusekile Mwaisabila.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ruangwa, Joseph Kiyengi wakati alipokuwa akionyesha eneo litakalojengwa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo. Maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho yameshaanza. Katika ziara yake Masauni pia aliagiza uanzishwaji wa Kituo cha Zimamoto wilayani humo haraka iwezekanavyo. Katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Twaha Mpembenwe. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ruangwa, Joseph Kiyengialipokuwa anatoa taarifa yake katika Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa ambacho kilijumuisha Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya Wizara hiyo mkoani Lindi.  Katika mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuanzisha Kituo cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu pamoja maandilizi ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MASAUNI AVIAGIZA VYOMBO ULINZI KUONGEZA KASI ZAIDI KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU, WAUZA DAWA ZA KULEVYA MKOANI LINDI, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa na Askari wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake, katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza, mjini Kilwa mkoani Lindi. Masauni aliwataka maafisa na askari hao kuongeza nguvu zaidi katika ukamataji wa wahamiaji haramu pamoja na wauza dawa za kulevya.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anakagua Makazi ya askari Polisi, Mitwero mkoani humo ambapo nyumba za askari hao zimechangaa na chache kutokana na wingi wa askari hao. Hata hivyo, Serikali hivi karibuni inatarajia kujenga nyumba mpya katika eneo hilo.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni eneo la Mitwero mkoani humo ambalo nyumba za makazi ya askari polisi zitakapojengwa. Masauni alikagua nyumba wanazoishi askari hao kwasasa pamoja na kukagua eneo hilo makazi mapya yatakapojengwa.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akilikagua Jengo jipya la ghorofa la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi ambalo linajengwa mjini humo. Kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, George Kombe, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga. Masauni aliongozana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anaangalia ramani ya ujenzi wa makazi ya askari polisi eneo la Mitwero mkoani humo. Masauni yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi. 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kulia) akimkaribishaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ofisini kwake kwa ajili ya kupewa taarifa ya mkoa huo, wakati Naibu Waziri Masauni alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NAIBU WAZIRI MASAUNI AFUNGUA MKUTANO WA SADC WA KUJADILI MASUALA YA USALAMA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akizungumza na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) (hawapo pichani), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto meza kuu) akizungumza na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga, na kulia ni Afisa wa kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Rokhayatou Diarra.
 Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wapili kulia meza kuu) akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia meza kuu ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye pia alifungua mkutano huo. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisindikizwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez  (kushoto), pamoja na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (kulia), mara baada ya Masauni kufungua Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo ambapo Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo walijadili masuala mbalimbali ya usalama. Warsha hiyo  ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wanne kulia), Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na  Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo mara baada ya Masauni kuufungua Warsha hiyo iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo. Warsha hiyo ilifanyika katika  Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.