HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

OTOSIM 2017 BY MAKEKE NI MOTO WA KUOTEA MBALI

 Unapomuongelea MAKEKE si jina geni kwenye Tathnia ya mitindo Tanzania na Afrika kwa ujumla, Mwaka Jana alikuja na collection ya aina yake iliyoitwa TABID - The African Beauty in The darkness, ( uzuri wa afrika gizani) collection hio imefanya vizuri sana 2017/2017 kwan imeoneshwa kwenye Majukwaa mbalimbali makubwa ya Mitindo.

Lakini mwaka huu mwanamitindo huyu asiyeishiwa MAKEKE amekuja na kitu kipya kabisa, kinaitwa OTOSIM2017 - ON THE OTHER SIDE OF MAKEKE, akiwa na maana ya ladha/ubunifu  Wa aina Nyingine, kwa Mara ya kwanza OTOSIM imeonyeshwa kwenye jukwaa kubwa la ZANZIBAR SWAHILI FESTIVAL  mwezi uliopita na kufanya maajabu makubwa jukwaani, nafkiri kwa watu waliokuwepo pale walijionea utamu Wa show hio  ya Ki - MAKEKE, msanii huyu Wa mitindo ameahidi mambo mengi matamu kwa mwaka huu 2017, tuendelee kusubiri.







ASYA IDAROUS ANOGESHA VIP RECEPTION AWARDS GALA FAIRFAX, VIRGINIA


Warembo wakiwa katika picha ya pamoja siku ya Jumamosi March 11, 2017 Fairfax, Virginia kwenye V.I.P. Reception Awards Gala iliyohudhuriwa na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Njeru Githae.
Mwanamitindo nguli wa kimataifa Asya Idarous Khamsin akiwa katika picha ya pamoja na
Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Njeru Githae

 Mrembo akiwa katika vazi la mwanamitindo nguli wa kimataifa Asya Idarous Khamsi.
 Vazi kutoka kwa mama mitindo wa kimataifa Asya Idarous Khamsin.


WAZIRI MWIJAGE AZINDUA AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA WAJASILIAMANI WASICHANA YA TAASISI YA MANJANO

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage  akipokelewa na Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha Nasser mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake ikiwa ni awamu ya pili.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha Nasser  kuhusu darasa linalotumika katika ufundishaji wa wasichana hao leo katika ofisi ya Shear Illusion iliyopo jengo la Millenium Tower jijini Dar
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akizungumza na wanafunzi wa Manjano Academic mara baada ya kufika na kujionea mafunzo hayo leo katika ofisi ya Shear Illusion jijini Dar
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi ijulikanayo kama "Manjano Dream Makers" kwa awamu ya pili iliyozinduliwa leo na waziri huyo katika ukumbi wa LAPF Millenium Towers jijini Dar es Salaam leo.
Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha Nasser akizungumza kuhusu uzinduzi rasmi wa program ya ajira kupitia tasnia ndogo ya urembo pamoja na kufanya utambulisho kwa wageni waalikwa.
Afisa Kutoka TFDA Bi. Grace Shimwela akizungumzia umuhimu wa kupata vibali vya urembo "Cosmetics and Personal Care" kwa wanawake walioko na ambao wamemaliza progamu mbalimbali za mafunzo kutoka kwa Manjano Dream Maker ili kuwasaidia pale wanapoanza kujitegemea
Jokate Mwegelo akizungumza jambo kwenye ufunguzi huo
Mshiriki mmoja aliyenufaika na Taasisi ya Manjano, Josephine Rwetela akizungumzia umuhimu wa kutengeneza ajira kupitia Tasnia ndogo ya Urembo nchini.
Mkurugenzi wa GS1 Tanzania, Fatma Khange akitoa maneno ya shukrani kwa wageni waalikwa pamoja na wanawake wanaoshiri kwenye mafunzo hayo yaliyoziduliwa leo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage.
Baadhi ya washiriki walioudhuria katika uzinduzi huo
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji 8020 Fashion na Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation, Shamim Mwasha
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akimkabidhi cheni Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation, Mboni Masimba
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage  akimkabidhi cheti Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation, Mariam Marion Ndaba
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage  akiwa kwenye picha ya pamoja na Manjano Academic
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akiwa kwenye picha ya pamoja na Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation.
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akiwa kwenye picha ya pamoja na Dream Makers.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,Charles Mwijage amewataka watanzania kuwekeza katika mfumo unaoweza kutoa ajira za moja kwa moja kwa vijana kama ilivyo katika kampuni ya Manjano Foundation.

Mwijage amesema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mafunzo ya wanafunzi 30 juu ya masuala ya urembo yanayoendeshwa ta tasisi ya Manjano Foundation ya hapa hapa nchini.

“huyu ni moja ya wawekezaji ambao wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja kwani ameamua kuwekeza kwa kutengeneza bidhaa ambazo zinatumia malighafi kutoka hapa hapa nchini na kuamua kuwawezesha wanawake wadogo kupata mafunzo hili waweze kuingiza pesa kupitia bidhaa hizo” amesema Waziri Mwijage.

Mwijage ameongeza kuwa mbali na Manjano foundation kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wasichana hao pia ipo katika mpango kabambe wa kujenga kiwanda mjini kibaha ambapo tayari wameshapata ekeri tatu kwa ajili yakujenga Godown ambalo litasaidia kufanya uzalishaji.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser amesema kuwa wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka tasisi hiyo wanaweza kuingiza kiasi cha Milioni mbili mpaka tatu kwa mwezi.

Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka hu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi.