HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MKWASA AAHIRISHA KAMBI TAIFA STARS

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu, imefahamika.

Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.

Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.

Taifa Stars ina mchezo na jijini Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa. Wachezaji ambao Mkwasa aliwaita mapema wiki hii ni: Makipa: Deogratius Munishi, Aishi Manula, Benny Kakolanya, Mebeki: Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Mohamed Husein ‘Tshabalala’, Juma Abdul, Erasto Nyoni, Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Juma Mahadhi, Hassan Kabunda, Washambuliaji: Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib, John Bocco, Jeremia Juma


TAIFA STARS KAMBINI AGOSTI MOSI, 2016

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Jumanne ya Julai 26, 2016 anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). 


Mkwasa maarufu kama Masters amesema lengo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu. 

“Kikosi change kitakuwa na vijana wengi, mimi ni muumini mkubwa soka la vijana ambao baadhi niko nao na ambao nitawaita, lakini pia mara baada ya ligi kuanza, nitaangalia wengine kabla ya kuwa na program ya ratiba ijayo ya michuano mbalimbali ya kimataifa itakayotolewa na CAF na FIFA,” amesema Mkwasa. 

Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili; Taifa Stars ina pointi moja wakati Chad ilijitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.