HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

PICHA: FREEMAN MBOWE NA JAMES MBATIA WAWATEMBELEA WALIOATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia jana jumanne Septemba 13, 2016 waliwatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Bukoba. Pia waliambatana na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare, Mbunge  wa Viti Maalum Bi.Savelina Mwijake na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Chadema.Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare akizungumza jambo na wafabiashara mbalimbali walioathiriwa na Tetemeko hilo kubwa Hapa Bukoba na huku kilio chao kikubwa kikiwa ni malimbikizo ya madeni yao kwa serikali ambayo mpaka wanapata hasara kubwa na kwa ujio huu mbaya wa Tetemeko la Ardhi wakidai zaidi ya Milioni 600.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi  James Mbatia(kulia) wakimsikiliza kwa makini mfanyabiashara huyo.
Janga la Tetemeko la Ardhi limewaathiri sehemu kubwa wafanyabiashara
Mhe. James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambae ni Mtaalamu wa Masuala ya Maafa na Mwenyekiti  wa Ukawa amewaunga mkono watu wa Bukoba leo akiambatana na Mwenyekiti mwenza Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe kwenye safari ya kuwatembelea wahanga. Katika Safari hiyo wametoa misaada ya dharura kwa wahanga ikiwemo chakula, sukari, fedha na n.k na leo Jumatano wataendelea na safari hiyo kuwatembelea Wahanga hapa Mkoani  Kagera katika sehemu mbalimbali. Jana Jumanne walitembelea sehemu ya Kibeta, Hamugembe, Kashozi, Nshambya katika shule ya Ihungo iliyoathiriwa zaidi na Tetemeko hilo kubwa la Ardhi na kuwafanya wanafunzi kusimamisha masomo yao kwa wiki mbili kwa kukosa sehemu ya kusomea/Madarasa na Mabweni.
Msafara kuelekea Kata ya Hamugembe
Pia walitembelea Kituo cha Watoto Yatima Hamugembe chenye watoto 36 ambacho kipo chini ya mwangalizi Bi. Saada ambacho kimepata matatizo kwa Nyumba zake kuanguka chini na kuwapa na kuwafariji 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman  Mbowe akisalimiana na Bi. Saada mwangalizi wa Watoto Yatima
Mhe. James Mbatia(wa kwanza kulia) akizungumza na wanakijiji wa Kibeta walipofikakuwajulia hali baada ya tetemeko la ardhi kulikumba eneo hilo.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akipata Ndizi kwenye Soko la Nyakanyasi wakati wa kuwatembelea Wahanga wa Tetemeko la Ardhi Bukoba leo.
Sehemu ya Majengo katika Shule hiyo kwa sasa baada ya kutokea Tetemeko
Tetemeko likiwa limeharibu sana sehemu kubwa ya Kanisa katika Shule hiyo ya Ihungo iliyopo kilometa 8 kutoka Bukoba Mjini
Taswira ya sasa Wanafunzi wa Shule ya Ihungo wakijipanga kuondoka Majumbani mwao baada ya Tetemeko la jumamosi kuwaathiri kiasi kikubwa na kushinikizwa kufunga shule hiyo kwa wiki mbili kupisha kuangaliwa upya kwa Shule hiyo kutokana na kuathiriwa na tetemeko.
Wakiwa Kanisani ndani, Kanisa lililojengwa miaka mingi iliyopita
Akiwa Kanisani hapo alipata muda akafahamu Viongozi mbalimbali katika picha waliopitia katika kanisa Hilo linalotimiza miaka 125 hivi karibuni lililozinduliwa mwaka 1892 likiwa ni kanisa la kwanza likifahamika Kashozi Parish.

Mh. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia pia alitembelea Kanisa la Kashozi


Kanisa la Kashozi kwenye Taswira ambalo pia limepata shida kwenye Tetemeko la Ardhi lililotokea hivi karibuni siku ya Jumamosi sept. 10, 2016.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alipata nafasi akapata picha na Mama mlezi kanisani hapo ambaye alitambulishwa kuwa ana umri mrefu

PICHA NA MDAU WETU FAUSTINE RUTTA

MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI ATOA TAMKO JUU YA MATUMIZI YA ALAMA ZA TAIFA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi hao katika kueleza jamii umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya vielelezo vya Taifa walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 27, 2016 kulia kwake ni Afisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Nyamagory Omary.
Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) muonekano sahihi wa Nembo ya Taifa wakati wa mkutano wake na wanahabari Juali 27, 2016, wa kwanza kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Frank Shijja.
Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo akionesha baadhi ya Vielelezo muhimu vya Taifa wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi yake Julai 27, 2016.


Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Cassian Chibogoyo amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya vielelezo vya Taifa kama njia ya kuheshimu Taifa na kuonesha uzalendo.

Chibogoyo ameyasema hayo hii leo katika kipindi cha pili cha ‘TUJITAMBUE’ ambacho kimewakutanisha waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari Jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa muendelezo wa elimu sahihi ya vielelezo vya taifa kwa jamii.

Akitaja alama tatu muhimu za Taifa ambazo ni Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa na Ngao ya Taifa, Chibogoyo amesema kila kimoja kinasimamiwa na sheria ili kuhakikisha matumizi yake yanaliletea heshima Taifa la Tanzania hivyo, wananchi ni vyema wakawa sehemu ya kutunza tunu hizo na kujiepusha na matumizi yasiyo sahihi.

Katika ufafanuzi wake ameeleza kuwa, Wimbo wa taifa una Tone Maalum na maneno maalum yaliyowekwa hivyo uimbaji unaoongeza vibwagizo kinyume cha uhalisia wake ni kosa kisheria.

Akielezea matumizi ya Bendera ya Taifa amesema ni kinyume cha sheria kubadili rangi zilizoainishwa kisheria kwani kila rangi ina maana yake na kuwa matumizi ya bendera serikalini yana utaratibu maalum kuanzia Ofisi ya Rais hadi kwa viongozi wa ngazi za chini.

“Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pekee ndiye anayeweza kufanya mabadiliko ya Bendera ya Taifa na Ngao ya Taifa kama kinavyoagiza kifungu cha 5 cha sheria ya vielelezo vya Taifa Na. 15 ya mwaka 1971.” Alisema Chibogoyo.

Kuhusu Nembo ya Taifa amesema ziko nembo nyingi feki mtaani ambazo pia zinatumiwa na wananchi katika matangazo au shughuli za kibiashara kinyume na matakwa ya sheria huku akitumia kipindi hicho kuonesha tofauti zilizopo katika alama sahihi na zile ambazo si, sahihi.

Bwana Chibogoyo alihitimisha kikao hicho kwa kuwashukuru wadau wote na kusema kuwa tarehe ya kikao kingine itatolewa kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu.