Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu akizungumza jambo na mmoja wa marubani wa shirika la Samaritan's Purse kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya wanafunzi watatu hawajaelekea Marekani kwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea wilayani Karatu wiki iliyopita.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akifurahia jambo na mmoja wa marubani wa kampuni ya Samaritan's Purse kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya wanafunzi watatu hawajaelekea Marekani kwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea wilayani Karatu wiki iliyopita.
Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro.
Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo wamjulia hali Doreen Elibarick
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akimsalimia Doreen Elibarick kabla ya kupanda ndege kwenda Marekani kwa matibabu.
Utaratibu wa kuwaingiza kwenye gari kisha kwenye ndege ukiendelea na maafisa wa uwanja wa ndege wa KIA.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akifurahia Kadi zilizoandaliwa na wanafunzi wa shule ya ISM kwaajili ya wanafunzi wenzao.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA KAMATI YA MGOGORO WA LOLIONDO
By: VIJIMAMBO on April 20, 2017 / comment : 0 Kassim Majaliwa, Matukio, Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo, waziri mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori Ttengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupoke taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuhusu ramani ya pori Tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumishi ya ardhi kwenye pori hilo. Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo Taarifa ya Kamati Shirikishi (Teule) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori Tengefu la Loliondo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea Taarifa ya Kamati Shirikishi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo mkoani Arusha, ambapo atatoa maelekezo baada ya kuisoma.
Amepokea taarifa hiyo leo (Alhamisi, Aprili 20, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Spika, Bungeni mjini Dodoma. Aliiunda Kamati hiyo, Desemba mwaka jana, mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Kiini cha mgogoro huo ni eneo la pori tengefu la Loliondo ambalo linagombewa na wawekezaji, wakulima, wawindaji kwa sababu ni mapitio ya wanyama, chanzo cha maji, mazalia ya wanyama, malisho ya mifugo na makazi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Tate William Ole-Nasha, viongozi wa mkoa wa Arusha, wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bw. Rashid Taka, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Arusha na wilaya ya Ngorongoro, wawakilishi wa wananchi, wawekezaji na asasi za kiraia ambao wote walishiriki katika uandaaji wa taarifa hiyo.
Waziri Mkuu amesema lengo la kamati hiyo ni kutaka kupata muafaka wa matumizi ya rasilimali zilizoko katika eneo hilo ili kila upande uweze kutekeleza majukumu yake bila ya kuathiri mwingine na kuwezesha wananchi wote kunufaika na rasilimali zilizoko katika eneo hilo.
“Serikali inataka watu wote tuwe kitu kimoja katika kutunza maeneo yetu, lakini pia shughuli za wananchi nazo ziweze kuendelea ili Watanzania wote tuweze kunufaika na rasilimali zilizoko kwenye maeneo yetu,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali inapenda kuona maeneo yote nchini yakiwa katika hali ya utulivu bila ya kuwepo kwa migogoro ya aina yoyote na ikitokea ni vema ikawa inapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika kwa ufasaha.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, APRILI 20, 2017.
WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA KAMATI INAYOSGHULIKIA MGOGORO WA LOLIONDO
By: VIJIMAMBO on March 02, 2017 / comment : 0 Kassim Majaliwa, Matukio, Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo, waziri mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akipokea Taarifa ya Kamati inayoshughulikia Mgogoro wa Loliondo Kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati amabye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo, Wanao shuhudia Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Uhifadhi Tanzania Martine Loiboki, Mkuu wa Wilaya ya Loliondo Rashid Taka, Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Wanyama Pori Prof Alexander Songorwa, Mkurugenzi Mkuu wa Thomson Safari s John Bearcroft , Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Milian Ole Nasha (MB) ,Mwenyekiti wa CCM Arusha Lekule Laiser , Mkurugenzi wa Baraza la Wafugaji Wanawake Bibi Maanda Ngoitika , Kikao hicho cha Kukabidhi Tarifa kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma leo tarehe 2 Februari 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionyesha Kitabu cha Taarifa ya Kamati inayoshughulikia Mgogoro wa Loliondo Kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati amabye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo, Wanao shuhudia Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Uhifadhi Tanzania Martine Loiboki, Mkuu wa Wilaya ya Loliondo Rashid Taka, Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Wanyama Pori Prof Alexander Songorwa, Mkurugenzi Mkuu wa Thomson Safari s John Bearcroft , Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Milian Ole Nasha (MB), Mwenyekiti wa CCM Arusha Lekule Laiser , Mkurugenzi wa Baraza la Wafugaji Wanawake Bibi Maanda Ngoitika, Kikao hicho cha Kukabidhi Tarifa kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma leo tarehe 2 Februari 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza Tarifa ya Mgogoro wa Loliondo kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati na Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Bwana Mrisho Gambo.
(Picha na PMO)
RC GAMBO: SERIKALI ITAYAPA KIPAUMBELE MAMBO YA MSINGI ILI KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII
By: VIJIMAMBO on January 31, 2017 / comment : 0 Matukio, Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo akiingia ukumbini tayari kwa kuanza rasmi kwa kongamano na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Arusha. Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa maendeleo katika komgamano hilo.
Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa AICC Elishilia Kaaya akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo na yeye kama mwenyeji wa eneo hilo akiwakaribisha katika kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano ambalo aliwaahidi waandishi kuwa ataliiitisha kwaajili ya kujadili na kupata taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha pamoja na wadaumbalimbali.
Mwenyekiti wa Arusha press club (APC) Akizungumza na katika kongamano hilo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza katika kongamano hilo.
Wa kwanza kushoto ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,akiwa kwenye kongamano katika kituo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.
Wadau wa Utalii kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.
Wa kwanza kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Mussa Juma ,akifuatiwa na Omary Moyo wakiwa katika kongamano hilo.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo.
Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha chanel Ten Jamillah Omary akiwa na mkurugenzi mwenza wa Me Production ambaye pia ni mpiga picha wa kituo cha luninga cha ITV Anold Rweyemamu.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia,aliyeko kushoto kwake ni nyekiti wa ccm mkoa ndugu Laizer
Na.Vero Ignatus, Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua Kongamana kutoa taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha ambapo kongamano hilo limewashirikisha wadau wa habari katika kuangalia na kutafakari na kupitia pamoja na kuangalia mpango mkakati wa maendeleo katika mkoa.
Gambo amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kutoa mrejesho kwa Watanzania kupitia waandishi kwa kipindi cha miezi sita ,na kuangalia mambo gani serikali ikiyapa kipaumbele itaondoa changamoto mbalimbali katika jamii kwa ujumla.
Aidha amesema kuwa utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia desemba 2016 umekuwa na mafanikio makubwa ,ambapo amesema kuwa hii ni kutokana na utamaduni wa kufanya na kutekeleza majukumu ya kazi kwa vitendo.
Amesema utekelezaji huo umechangia katika kuboreka kwa maeneo mbalimbali ya sekta muhimu katika kukuza uchumi katika mkoa hasa pato la mkoa na wananchi moja kwa moja.
“Katika kipindi hiki,miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kupewa kipaumbele cha kutosha hivyo kwa namna moja kutekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (MKUKUTA II)katika mkoa na taifa kwa ujumla”alisema Gambo.
Amesema kuwa Mkoa umesimamia utekelezwaji wa shughuli za serikali na kushuhudia mafanikio katika sekta za kilimo,afya,maji,barabara,mofugo,maliasili na nyinginezo kama takwimu zilivyowasilishwa .
Amesema kuwa serikali imejipanga kuhangaika na wale wote ambao wanachochea migogoro kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hatutawafumbia macho.
Kwa upande wamafanikio utekelezaji wa mkoa kuanzia mwaka 2005 mkoa ulikuwa na shilingi 723,809 milioni kwa mwaka huo mkoa ulikuwa wa (9) katika kuchangia patao la Taifa,ambapo pato la mkazi lilikadiriwa kuwa shilingi 506,902 kwa mwaka sawa na shilingi 1,389 kwa siku.
Kwa mwaka 2010 pato la mkoa wa Arusha lilikuwa shilingi 2,136,514milioni kwa kuchangia pato la taifa Arusha ilikuwa ya 7.mwaka huo pato la mkazi wa Arusha lilikuwa shilingi 1,283,361 kwa mwaka sawa na shilingi 3,516 kwa siku.
Hadi mwaka 2015 pato la mkoa linakadiriwa kuwa shilingi 4,271,447milioni.
kwa takwimu hizo pato la mkazi wa Arusha lilikuwashilingi 2,322,031 milioni kwa mwaka ni sawa na shilingi 6,361 kwa siku.
MKURUGENZI MKUU WA UNEP AFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA
By: VIJIMAMBO on January 25, 2017 / comment : 0 Matukio, Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo, UN Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo(kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim katika ziara yake mkoani Arusha,Gambo ameiomba UNEP kusaidia fedha mradi wa kulinda chanzo cha maji cha Olgilai kilichopo wilayani Arumeru kinachotumika kusambaza maji jijini Arusha ambacho kimesongwa na shughuli za binadamu kikiwemo kilimo na upandaji miti ambayo sio rafiki na vyanzo vya maji.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim akiwa na ujumbe wake wakifatilia mada iliyowasilishwa na Meneja wa Baraza la Mazingira Kanda ya Kaskazini(NEMC) Novatus Mushi.
Mratibu wa kitaifa wa UNEP nchini, Clara Makenya akizungumza jambo kwenye ziara hiyo,kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim(kushoto kwake) naa maafisa wengine wa UN pamoja na ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim (mwenye tai) akiangalia chanzo cha maji cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiri jijini Arusha (AUWSA) eneo la Olgilai Kata ya Kiutu alikofika kuangalia uharibifu wa chanzo hicho.
SAKATA LA MWANDISHI HALFANI LIHUNDI , MKUU WA MKOA WA ARUSHA AINGILIA KATI
By: VIJIMAMBO on December 26, 2016 / comment : 0 Habari, Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo
Sakata la mwandishi wa habari wa ITV Halfan Lihundi kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 24 kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Arumeru baada ya kuandika habari ambayo haikumfurahisha mkuu huyo, limechukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuingilia kati na kusema waandishi wa habari wanao uhuru wa kuandika habari mahali popote katika mkoa huo ili mradi wazingatie weledi katika taaluma.
Gambo ambaye wakati sakata hilo linatokea alikuwa safarini analazimika kukutana na wanahabari wote wa jiji la Arusha baada ya tukio hilo lililogoga vichwa vya waandishi mkoa wa huo na kusababisha kusimamisha shughuli zao ikiwemo kuweka kalamu chini kumnusuru mwenzao lakini pia wadau mbalimbali tasnia ya habari kukerwa na kitendo hicho.
Gambo amesema anatambua umuhimu wa kazi za waandishi wa habari na kuongeza kuwa kabla ya kiongozi huyo hajafanya maamuzi hayo pamoja na mamlaka aliyonayo busara ilitakiwa itumike.
Claud Gwandu ni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa arusha na baadhi ya waandishi arusha anapaza sauti zao kuonyesha hisia zao juu ya sakata hili.
Lakini busara ya Gambo inatuliza munkari ya waandishi hawa na kumaliza mzozo huo ambao ulionekana kwenda mbali zaidi.
Na je nini kauli ya mkuu huyo kuhusiana na usalama wa waandishi hawa wakiwa katika kutekeleza majukumu yao?
Akiwa mkoani arusha katika majumuisho ya ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita waziri mkuu aliwapongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya kwani huamsha au hutoa mrejesho wa mambo muhimu ambayo huwasaidia viongozi kufanya maamuzi sahihi.
MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA UMMA ARUSHA
By: VIJIMAMBO on December 02, 2016 / comment : 0 Kassim Majaliwa, Matukio, Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo, waziri mkuu
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa serikali na halmashauri wa mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha, Desemba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya mkoa wa Arusha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo baada ya kusomewa taarifa hiyo katika mkutano wake na watumishi wa serikali na halmashari kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Desemba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bahasha yenye nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ubadhirifu unaofanyika katika halmashauri ya Wilaya ya Arusha kutoka kwa Benard Mtei wa Idara ya Afya katika halmashauri hiyo wakati alipozungumza na watumishi wa serikali na halmashauri mjini Arusha Desemba 2, 2016.
Baadhi ya watumishi wa serikali na halmashauri wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Desemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MHE. GAMBO AWATAKA WAFADHILI KUTOA CHAKULA MASHULENI
By: VIJIMAMBO on November 16, 2016 / comment : 0 Jamii, Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkurugenzi wa WEI-TANZANIA Bi. Lilian Badi (aliyesimama) akielezea mafanikio ya Mradi wakati wa Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkurugenzi Mkuu wa World Education Inc Bi.Gill Garb akitoa taaria ya utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee kupitia WEI-Bantwana.
Tumebadilisha maisha ya watoto na kuhakikisha usalama wao katika Jamii wanazoishi, tumewatambua wazazi wenye watoto walioathirika na kuwapa elimu ya jinsi ya kuwafahamisha watoto wenye hali hiyo na namna ya kuishi nao ili waweze kukua katika malezi bora na afya njema sanjari na kupata Elimu alisema Bi. Hindu.
Na Nteghenjwa Hosseah - Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amewataka wafadhili na wadau wa watoto kubuni miradi inayoendana na kusaidia Mpango wa Serikali wa Elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari ili kupunguza changamoto zinazojitokeza kwa sasa na kuuwezesha mpango huu kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Mhe. Gambo ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa kushirikishana tuliojifunza wakati wa utekelezaji wa mpango wa pamoja tuwalee uliotekelezwa kwa miaka sita kwenye Kanda ya Kaskazini na ambao kwa sasa umemaliza muda wake ulifanyika kwenye Hotel ya Mt Meru Jijini hapa.
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa amesema kazi kubwa imefanyika wakati utekelezaji wote wa mradi na mafanikio yake tumeonekana kwani watoto wamefikiwa na kusaidiwa kutoka katika mazingira hatarishi yaliyokuwa yanawakabili na wengine kupatiwa kadi za msamaha wa matibabu na zaidi mradi huu umekabidhiwa kwa Halmashauri husika ambazo zitaendelea kusimamia na kutekeleza mipango iliyowekwa chini ya mradi wa Pamoja Tuwalee.
Aliendelea kusema kuwa kukamilika kwa mradi huu katika awamu ya kwanza ni wazi kabisa kwamba ni maandalizi ya mradi mwingine ambao utakua na malengo yanayoshabihiana na programu ya awali hivyo ni vyema kwa kuwa walengwa bado ni watoto niwatake wadau kubuni miradi utakaolenga kusaidia Elimu bure na kwa kuwa watoto wote wanapata Elimu bure kupitia mpango huu basi ni vyema mkaelekeza nguvu kwenye utoaji wa Chakula kwa wananfunzi suala ambalo tumeona ni changamoto kwa watoto wetu.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la WEI – Bantwana “World Education Inc” Bi. Gill Gap alisema wanajivunia kuwa Taasisi iliyofanikisha utekelezaji wa mradi wa pamoja kwa ushirkiano wa Serikali ya Tanzania katia utekelezaji wa mradi pamoja na Serikali ya Marekani kwa ufadhili mradi huu. Pamoja Tuwalee ilikuwa maalumu kuwalinda watoto walio katika mazingira hatarishi na kutoa Elimu kwa wazazi walioathirika namna ya kuishi na watoto hao pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa Halmashauri kuendeleleza jitahada za mradi huu.
Jacklin Badi ni Mkurugenzi wa WEI – Tanzania anasema “Bantwana ni kitengo ndani ya Shirika la WEI kinachohudumia watoto na hapa Tanzania tulianza utekelezaji mwaka 2010 na mpaka sasa tumefanikiwa kuwafikia watoto 1,470,445 pamoja na wazazi wao na wameweza kupatiwa huduma jumuishi za kuwasaidia na kuwalinda watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana “Center for women, Children and Youth Development (CWCD) Bi. Hindu Ally Mbwego ambao ni watekelezaji wa mradi huu wa Pamoja Tuwalee kupitia mwamvuli wa WEI-Bantwana amesema wamefanikiwa kuwafika katika maeneo yote ya Jiji la Arusha, Halmashauri ya Karatu na Moshi na wanajivunia mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi huu.
Mradi wa pamoja Tuwalee ni mpango wa Kitaifa wa miaka mitano uliotekelezwa na fedha za mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupunguza makali ya virusi vya ukimwi kwa waathirka kupitia Shirika la Misaada la Marekani la USAID na kutekelezwa na WEI-Bantwana pamoja na Kituo cha maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana kilichopo Jijini Arusha.
Mwakilishi wa US-AID Tanzania Bi. Maria Busquets akielezea namna ambavyo Shirika lake limefanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akizungumza na wadau wa Mkutano
Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana (CWCD) Bi. Hindu Ally Mbwego akielezea mafanikio ya mradi kupitia Kituo chake ambao ndio watekelezaji katika Halmashauri za Jiji la Arusha, Karatu na Moshi.
Picha ya pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha (katikati mbele), Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi waliotekeleza mradi huu, viongozi wa WEI, US AID, CWCD pamoja na Wadau wa watoto walioshirki katika Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(mbele kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa CWCD Bi. Hindu Ally Mbwego (kulia mbele) pamoja na baadhi ya watoto wa Pamoja Tuwalee.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Pili kushito) kwenye picha ya pamoja na wadau waliotekeleza mradi wa Pamoja Tuwalee
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati)
akiwa na wataalam kutoka Halmashauri ya
Korogwe waliofanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee.
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi kwa kushiriki Maonesho ya...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
WAZIRI DKT. BASHIRU AIAGIZA BODI MPYA YA TAFICO KUIGEUZA TAFICO KUWA INJINI YA UCHUMI SEKTA YA UVUVIWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameitaka Bodi mpya ya pili ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kuhakikis...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu na mafunzo kwa vyuo vikuu pamoja na shule za sekondar...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014


















