HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

DMF YATOA MKONO WA EID EL FITR KWA WAKAZI WA MAGOMENI KAGERA JIJINI DAR

Mratibu wa Matukio ya Kijamii wa Taasisi ya Doris Mollel, Alice Mwakatika akikabidhi sehemu ya vyakula kwa mmoja wa wakazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, iliyofanyika Juni 24, 2017. 
Mratibu wa Matukio ya Kijamii wa Taasisi ya Doris Mollel, Alice Mwakatika (kulia) pamoja na Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa taasisi hiyo, Rahma Amoud (wa pili kulia) wakikabidhi sehemu ya vyakula kwa Bi. Aisha Mohamed (kushoto) mkazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, iliyofanyika Juni 24, 2017. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani, Saleh Kawambwa.
Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amoud akikabidhi sehemu ya vyakula kwa wakazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, iliyofanyika Juni 24, 2017. 
Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amoud akikabidhi sehemu ya vyakula kwa Bi. Ashura Nassor mkazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, iliyofanyika Juni 24, 2017. Katikati ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani, Shaban Kawambwa.
Mratibu wa Matukio ya Kijamii wa Taasisi ya Doris Mollel, Alice Mwakatika akimkabidhi mfuko wa sandarusi wenye vyakula mbalimbali Mtoto Biatha Shembilu (14)  ambaye ni mgonjwa wa moyo mkazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, Juni 24, 2017.
Rahma Amoud wa DMF akikabidhi sehemu ya vyakula kwa Mzee Abdul Mkwanda na Mkewe Bi. Moshi Mlango wakazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, Juni 24, 2017.

DK. SHEIN ATOA MSAADA KWA WANANCHI WA PEMBA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO

  MAGODORO 80 yaliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, yakiwa kwenye uwanja wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, kabla ya kugawiwa kwa waathirika wa mvua wa mkoa huo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, akitoa neno la shukuran, mara baada ya kukabidhiwa magodoro 40 na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, kutoka kwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali Mohamed Shein kwa ajili ya waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

UNGA wa ngano polo 112, uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein pmoja na Mchele na Sukari idadi kama hiyo, kwa ajili ya wananchi wa Pemba, wanaoishi kwenye mazingira magumu, ambapo chakula hicho ni sadaka, inayotolewa kila mwezi wa ramadhan na rais wa Zanzibar kwa ajili ya futari, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MJUMBE wa kamati ya zaka na sadaka ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ndgu Haji Nassib Nyanya, akimkabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, mchele, sukari na unga wa ngano, chakuka chenye thamani ya shilingi milioni 40, ikiwa ni sadaka iliotolewa na Rais Zanzibar, kwa ajili ya futari ya wnananchi wanaoishi kwenye mazingira magumu kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza kabla ya kuwakabidhi wakuu wa wilaya ya Mkoani na Chakechake, saruji paketi 150 kila wilaya, zilizotolewa na Rais wa Zanzibar, kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mvua ilionyesha hivi karibuni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, na Mkuu wa wilaya Chakechake, Salama Mbarouk Khatib, saruji paketi 150 kila wilaya, iliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

JTFE YAMWAGA VYANDARUA KITUO CHA WATOTO ALBINO SHINYANGA

Katika kukabiliana na ugonjwa wa Malaria, Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) inayojishughulisha na masuala ya watu wenye Ualbino yenye makao makuu yake nchini Uholanzi imetoa msaada wa vyandarua 50 kwa ajili ya watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga. 



Msaada huo umetolewa na mwenyekiti wa JTFE, Pieter Staadegaard siku moja tu baada ya kutembelea kituo hicho na kuelezwa kuhusu upungufu wa vyandarua katika kituo hicho ambapo sasa kina watoto 228 kati yao wenye ualbino ni 142. 
Akikabidhi vyandarua hivyo leo Jumamosi May 27,2017 Staadegaard alisema vitasaidia kupiga vita ugonjwa wa malaria na kwamba miongoni mwa malengo ya taasisi hiyo ni kuongeza elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ualbino na kuwawezesha kiuchumi watu wenye ualbino. 
"Nilifikika katika kituo hiki jana May 26,2017 kisha kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa watoto ikiwemo midoli,miwani ya kuzuia mionzi ya jua lakini pia viatu,nilipomaliza kugawa zawadi hizo viongozi wa kituo hiki wakaniambia pia kuna upungufu wa vyandarua,ndiyo nimeamua kuleta vyandarua ili watoto hawa wasije kupata ugonjwa wa malaria kwa kukosa vyandarua",alieleza Staadegaard.
“Taasisi hii yenye makao makuu yake nchini Uholanzi imeanzishwa mwezi Januari mwaka 2017 baada ya mimi kukutana na bwana Josephat Torner mkoani Geita kisha kujadili namna ya kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu watu wenye ualbino”,aliongeza Staadegaard. 
Katika hatua nyingine alisema taasisi hiyo ina mpango kwa kuanza kununua Kahawa inayozalishwa nchini Tanzania na kuipeleka nje ya nchi kwa lengo la kuwainua kiuchumi watu wenye ualbino. 
Naye Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner alisema katika kuadhimisha siku ya Albino duniani June 13 mwaka huu,TAS inaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ualbino.
Kwa Upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Buhangija na msimamizi wa kituo hicho,Seleman Kipanya alishukuru kupokea msaada huo na kuwaomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia watoto hao.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Pieter Staadegaard akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner akizungumza katika kituo cha Buhangija
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner  akizungumza kabla ya kuanza kugawa vyandarua
Vyandarua vilivyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Pieter Staadegaard akigawa vyandarua kwa watoto
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner akiwaelekeza watoto wakati wa kugawa vyandarua
Zoezi la kugawa vyandarua linaendelea
Afisa Habari na Uhusiano kutoka Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner akigawa vyandarua
Msimamizi wa kituo cha Buhangija/Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa vyandarua
Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Buhangija Kuluthum  Ally akitoa shukrani kwa taasisi ya JTFE kutoa misaada katika kituo cha Buhangija.


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MOROGORO

Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba. Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo.
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF. Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro. Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga akitoa ufafanuzi mchache jinsi alivyokuwa anaufahamu Mfuko wa Pensheni PPF. Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wakielekea wodini.
Wagonjwa wakitumia mashuka na vitanda vilivyotolewa na PPF. --- Serikali imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini. Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini. Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha. Naye meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' ambapo aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.

WANAWAKE WA MSIKITI WA KHOJA SHIA ITHNA ASHERI WATOA MISAADA HOSPITALI YA BUTIMBA

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
WANAWAKE wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri jijini Mwanza wametoa  msaada wa vitu mbalimbali  vyenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa Hospitali ya Butimba ya Wilaya ya Nyamagana ili kusaidia kupunguza changamoto zinazoikabili.
Mwenyekiti wa kina mama hao Radhida Ahmed akimkabidhi msaada huo Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk. Kajiru Mhando alisema utasaidia kupunguza kero kwa wagonjwa na kuzitaka taasisi zingine zijitokeze kutatua changamoto za hospitali hiyo hasa  ujenzi wa wodi ya wazazi.
Alisema msaada huo umelenga kuonyesha mshikamano wao kwenye jamii katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume, Imam Mahdi (A.T.F.S) ambayo hudhimishwa  Mei 7, kila mwaka.
“ Tuliguswa na changamoto zinazoikabili hospitali yetu hii ya wilaya lakini pia kuonyesha mshikamano wetu na jamii tukaona tuje kutoa msaada huu kwa ajili ya kuwapunguzia wagonjwa kero na changamoto,Wapo wenye utajiri waone na kuguswa na matatizo ya wenzao na kuwasaidia hasa wagonjwa” alisema Rashida.
Aliutaja msaada huo walioukabidhi kuwa ni magodoro 10, mashuka pea 25 na foronya zake, mablanketi 50 na vyandarua 50, vifaa vya usafi (mifagio 10, brashi 10 na Squizers 10) pamoja na sabuni ya maji (Detol) lita 10 na ya unga kg 15.
Vingine ni vifaa tiba ambavyo ni mashine mbili za kupima mapigo ya moyo,Stethescope mbili na, Heavy duty Gloves(pea 5),Sterile Gloves (boksi 4) makasha ya kuhifadhia uchafu makubwa na madogo (12) na zawadi kwa watoto.
Awali Mwenyekiti mstaafu wa Msikiti huo Alhaji Sibtain Meghjee alisema jamii ya Waasia na Waislamu shughuli wanazozifanya kwenye jamii  hazipewi fursa ya kutangazwa kwenye vyombo  vya habari.
“Kwetu sisi Waislamu, hasa Asian Community ( jamii ya Waasia) shughuli nyingi za kijamii tunazofanya hazipewi nafasi kwenye vyombo vingi vya habari.Vyombo vingi viko mstari wa mbele kutangaza zaidi migogoro kuliko misaada inayolenga kusaidia jamii, kujenga umoja na mshikamano  kwenye jamii,” alisema Meghjee.
Akipokea msaada huo Dk. Mhando aliwapongeza akina mama hao kwa moyo wao wa huruma na kujitoa  kuisaidia hospitali hiyo na kwamba utawasaidia kupunguza changamoto lukuki zilizopo  .
“Ingawa bado tuna changamoto ya ukosefu wa wodi ya wanaume lakini vifaa hivi vimetusaidia sana na vitaanza kutumika leo hii hasa katika wodi ya wazazi ya akina mama wanaojifungua ambao wengi ndio waathirika,”alisema.
Dk. Mhando alieleza kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa madawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na miundombinu ya majengo pia haina kitanda cha kutolea damu, mashine ya kupima mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni ili kutambua kama yu hai ama la.
“Wodi zilizopo kwenye hospitali yetu ya wilaya hazitoshi na hatuna  wodi ya wanaume na wanaokuja kutibiwa hapa na kutakiwa kulazwa, tunalazimika kuwapa rufaa ya kwenda Hospotali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,”alisema Dk. Mhando.
  Msaada iliyotolewa katika hospiali ya Butimba jijini Mwanza kutoka kwa wanawake wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza.
Wanawake wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza wakabidhi Blanketi
 Dk Kajiru akipokea moja ya godoro kati ya 10 yalitolewa msaada wa akinamama wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna    Asheri Mwanza
 Mwenyekiti wa Wanawake wa   msikiti wa Khoja Shia Ithan Ashaeri Rashida Ahmed pamoja na Mrs karimu wakimfurahia mtoto Hajida walipotelea wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Butimba.

RAIS DKT MAGUFULI ATOA MSAADA WA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA (AMBULANCE) KWA WABUNGE WA NKASI, TABORA NA SHINYANGA

 Wabunge wa Nkasi, Tabora na Shinyanga wakiwasili tayari kukabidhiwa magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwakaribisha  Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (Nkasi Kaskazini)  Mhe. Munde tambwe (viti maalumu - Mkoa wa Tabora) na Mhe Lucy Mayenga (viti maalumu-mkoa wa Shinyanga) kupokea magari ya kubebea wagonjwa waliyopewa saada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Nkasi Mhe Ali Mohamed Kessy baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Lucy Mayenga baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Munde baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kati) akiwa na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Alphayo Kidata (Kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu  Bw. Charles Mwankupili (kulia) na  Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (mbunge wa Nkasi Kaskazini)  Mhe. Munde tambwe na Mhe Lucy Mayenga (wabunge viti maalumu)  baada ya kuwakabidhi magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017.


PICHA NA IKULU

MKE WA ROMA MKATOLIKI AFUNGUKA KUHUSU TUKIO LA MUME WAKE KUTEKWA

Mke wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu.
Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.

“(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki.

Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu.

“Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy.

Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

KINYEREZI FAMILY YAWAKUMBUKA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA NEW HOPE SIKUKUU YA PASAKA


Wadau wa Kinyerezi Family kiwa sambamba na Watoto wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu, New Hope kilichopo Tabata,wakisali kwa pamoja mara baada ya kuwakabidhi Msaada wa vitu mbalimbali,ikiwemo mchele, nyama, sukari, mayai, nguo na vinginevyo, ili  watoto hao nao wapate kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka
  Kinyerezi Family wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watoto wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu cha New Hope kilichopo Tabata,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali,ikiwemo mchele, nyama, sukari, mayai, nguo na vinginevyo, ili na watoto hao wapate kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka