HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Wachoraji wapata msiba wa Mwenzao Theresia Kaiza


BALOZI SEIF ASHIRIKI MAZIKO YA MZEE KHAMIS JUMA MKADARA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu kutoka Kulia akijumuika pamoja na Viongozi na Wananchi katika kumsalia Mwanasiasa Mkongwe wa Kisiwani Pemba Mzee Khamis Juma Mkadara kwenye Msikiti wa Ijumaa Wawi Chake chake Pemba.  Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Juma Abdulla Juma {Mabodi } na kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Kilimo, Mali Asili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mtaa wa Wawi Chake chake wakiwa miongoni mwa wananchi waliomsalia Kiongozi huyo nguli wa Kisiasa Kisiwani Pemba Mzee Mkadara.
Balozi Seif akimimina mchanga katika Kaburi la Mzee Khamis Juma Mkadara aliyezikwa katika Mavani ya Familia yake yaliyopo Mashariki ya Msiku wa Ijumaa wa Wawi Chake chake.
Balozi Seif wa Pili kutoka Kulia akiwa sambamba na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Juma Abdulla Juma { Mabodi } wakiwafariji wanafamilia ya Mwanasiasa Mkadara Nyumbani kwake Wawi Chake chake.
Baadhi ya Wanafamilia ya Mzee Khamis Juma Mkadara wakionyesha sura za majonzi na huzuni kufuatia kuondokewa na mpendwa wao aliyekuwa kiungo katika familia hiyo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Juma Abdulla Mabodi wa Pili kutoka Kulia akiwataka kuwa na moyo wa subra Wajukuu wa Mzee Mkadara. Picha na – OMPR – ZNZ.                                                                                                    


Mwanasiasa Mkongwe wa Zanzibar Mzee Khamis Mkadara aliyefariki Dunia mapemba jana asubuhi amezikwa Kijijini kwake Wawi Mkoa wa Kusini Pemba maziko yaliyohudhuriwa na Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislamu, Wananchi pamoja na Viongozi wa Kiserikali na Kisiasa. 


Mzee Khamis Mkadara alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya kawaida pamoja na uzee alifariki nyumbani kwake Mtaa wa Wawi Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika mazishi hayo aliiwakilisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Chama cha Mapinduzi akijumuika na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Juma Abdulla Mabodi na baadhi ya watendaji wa Serikali.

Marehemu Mzee Khamis Juma Mkadara alizaliwa Mwaka 1927 na kuanza elimu ya Quran katika Madrasa mbali mbali za Wilaya ya Chake chake ambapo baadaye katika ujana wake akajishughulisha na masuala ya Kisiasa katika dhana nzima ya kudai Uhuru wa Visiwa vya Zanzibar.

Katika kipindi hicho ya kutaka kujikomboa Mzee Mkadara alikuwa muanzilishi wa Chama cha Shirazy Association na baadaye kukiunganisha na chama cha African Association na Kuzaliwa kwa Chama cha Afro Shirazy Party.

Katika utumishi wa Chama Mzee Khamis Juma Mkadara aliwahi kuwa Mwenyekiti wa ASP wa Wilaya ya Chake chake mwaka 1973 na baada ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi mwaka 1977 aliendelea na wadhifa huo hadi mwaka 1997.

Mbali ya wadhifa huo wa Kichama Mzee Mkadara pia aliwahi kuwa Diwani wa Wadi ya Wawi mwaka 1995.

Mwanasiasa huyo mkongwe Kisiwani Pemba alikuwa mstawi wa mbele katika utetezi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar akiwa miongoni mwa Wazee waliotumikia kwa kiindi kirefu Taifa hili la Tanzania.

Utumishi huo uliweza kumpatia fifa na ushujaa uliopelekea kutunukiwa nishani na Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Nne Dr. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar wa Awamu ya Sita Dr. Aman Abeid Karume.

Mzee Khamis Juma Mkadara aliyefikisha umri wa Miaka 90 ameacha Kizuka Mmoja, Watoto Wanane na Wajukuu 33.

Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Mwanasiasa huyo Mkongwe Mzee Khamis Juma Mkadara mahali pema peponi. Amin.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
8/6/2017.



MWILI WA HALILA TONGOLANGA WAAGWA

Halila Tongolanga amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili. Alikuwa mwanamuziki wa siku nyingi na alifahamika kwanza kwa wengi baada ya kuanza kusikika kibao chake cha lugha ya Kimakonde cha Kila munu ave na kwao, chenye tafsiri ya ‘Kila mtu ana kwao’ ambacho alikirekodi akiwa bendi ya jeshi ya CTU Monduli, iliyojulikana kama Les Mwenge. 
Kwa kifupi ni kuwa baada ya hapo aliitwa kujiunga na bendi iliyokuwa mali ya Dr Alex Khalid, iliyokuwa ikiitwa Makondeko Six. Wakati huo Dr Khalid alikuwa na sehemu kubwa ya burudani iliyokuwa pia na ukumbi na ilikuwa inaitwa Makondeko ikawa na bendi ya watu sita hivyo bendi hiyo ikaitwa Makondeko Six. 
Bendi hii awali ilikuwa ikipiga muziki kwa kufuata nyayo za bendi ya Tatu Nane, lakini Dr Khalid baada ya kuona bendi haina umaarufu kutokana na aina ya muziki iliyokuwa ikipiga, ndipo alipomuita Halila Tongolanga nae akaja na baadhi ya wanamuziki wakajiunga na kuanzisha kundi lililoendelea kutumia jina la Makondeko Six japo wanamuziki walikuwa wengi zaidi ya sita.
Na ndipo katika kundi hili lilikuwa na wanamuziki wengine kama Innocent Nganyagwa, Anna mwaole wakaweza kurekodi tena wimbo wa Kila Munu Ave na kwao na kundi kupata umaarufu mkubwa mpaka baada ya kusambaratika kwa Makondeko baada ya kifo cha Dr Alex Khalid, lakini Tongolanga aliendelea kutumia jina la Makondeko. 
Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Tongolanga katika kundi la makondeko Six, wakiwa wanasubiri kusafirisha mwili wa mpendwa wao.Toka kushoto, Innocent Nganyagwa, Meneja wa bendi, mpiga solo, Waninga 

Tongolanga amefanya kazi nyingi za muziki ikiwemo kuwa mmoja wa kundi lililoundwa na wanamuziki wengine mahiri kama Moshi William, Muhidin Mwalim, Huluka Uvuruge, Kandaya na wengine lililojulikana kama Bana mwambe, ambapo waliweza kutoka nyimbo nyingi nzuri sana wakati biashara ya kuuza album ilipokuwa ina faida.
Tongolanga ameagwa na wapenzi wa muziki ndugu na marafiki, lakini kulikuwa na uhaba mkubwa wa wanamuziki wenzie katika kundi lililokuja kumuaga mwanamuziki huyu. Waliojitokeza hasa ni wanamuziki wale tu ambao waliwahi kupiga nae katika kundi la Makondeko na Bana Mwambe na wanamuziki wengine wachache wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki John Kitime, Katibu Mkuu wa Chamudara Hassan Msumari. Serikali iliwakilishwa na Katibu Mtendaji wa BASATA. 
Katika jambo moja kubwa lililotokea wakati wa kuaga mwili ni kujitokeza kwa balozi wa Msumbiiji Bi Monica Patricio Clemente aliyefika Muhimbili kuaga mwili wa Tongolanga akiwa amesindikizwa na maafisa wengine, na pia Balozi huo alitoa rambirambi zake kama Balozi na alitoa rambirambi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji. Hili lilikumbusha usemi wa wahenga ‘Nabii hathaminiwi kwao.’ Taarifa zilizopatikana pale ni kuwa Tongolanga alikuwa mtu maarufu sana nchini Msumbiji, na aliyekuwa ni msanii muhimu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo.
Balozi wa Msumbiji Bi Monica Patricio Clemente akiaga sanduku lililokuwa na mwili wa Halila Tongolanga

Nilipokutana nae kwa mara ya mwisho akiwa kitandani Tongolanda kwa sauti ya uchovu alinambia alikuwa na mengi ya kunambia, wakati tunasubiri taratib kukamilika za kuanza kusafirisha mwili, Innocent Nganyagwa ambaye alikuwa mmoja ya wanamuziki waliotengeneza kundi la Makondeko Six alinambia Tongolanga alikuwa amepanga kufanya onyesho la ‘Usiku wa Makondeko’ na alikuwa na mipango mingine mikubwa ya kufanya kupitia kipaji chake. Pengine ndiyo hayo aliyotaka kunambia Mungu pekee anajua. 

Shukrani za pekee zimfikie Mbunge wa Tandahimba Mheshimiwa Katani Ahmed Katani, kwani kwa juhudi zake Tongolanga alisafirishwa akiwa hai kutoka Ndanda hadi Dar es Salaam kwa matibabu, na pia ndie aliyeusafirisha mwili wa mwanamuziki huyu kwenda Mchichila kwa ajili ya mazishi.
Toka kushoto Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Nyangamale, Balozi wa Msumbiji nchini, Katibu Mtendaji wa BASATA, Mbunge wa Tandahimba Mhe Katani Katani, afisa wa Ubalozi wa Msumbiji 

Tongolanga anategemewa kuzikwa kijijini kwao Mchichila kesho Junanne 6 Juni 2017.
Mungu Amlaze Pema Halila Tongolanga 
Mpiga Kinanda Geophrey Kumburu, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari 
John Kitime, wanamuziki wa Makondeko Six, Mngereza, Kumburu
Sanduku alilolazwa Halila Tongolanga likitayarishwa kuingizwa kwenye gari la kusafirisha kuelekea Mcjichila 
Sanduku likiingizwa kwenye gari 
Imetayarishwa na John Kitime wa www.tanzaniarhumba.blogspot.com

PICHA: MWILI WA MAREHEMU PHILLEMON NDESAMBURO WAAGWA KATIKA VIWANJA VYA MAJENGO MKOANI KILIMANJARO

Viongozi wa juu wa Chadema, Freeman Mbowe na Edward Lowassa wameupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo.

Ndesamburo alifariki ghafla wiki iliyopita wakati akipata matibabu katika hospitali ya KCMC.
Mwili wa Ndesamburo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi Mjinim,utaagwa katika viwanja hivyo na leo saa kumi jioni utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwamo muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, Frederick Sumaye wapo uwanjani hapo kwa ajili ya kumuaga Ndesamburo.
  Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo lilielekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi waliofika kwenye uwanja  huo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasili atika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa  aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo. 
Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na dini wakiwa wamesimama mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo kuwasili uwanjani hapo



 Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye uzuni mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ulipokuwa unaelekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo. 



  

  

  

MWENYEKITI WA BUNGE AONGOZA MAZISHI YA MAMA WA MTEMVU JUNI 2, 2017

Enzi ya uhai wa Sitti Mtemvu
Mazishi ya Sitti Mtemvu,  mama wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu yaliyofanyika Dar es Salaam,  Juni 2, 2017 katika makaburi ya  Kinondoni ya kiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Mh, Azzan Zungu na kuhudhuriwa na  viongozi mbalimbali akiwepo Wananchi, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Tanzania, Davis Mwamunyange , Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Wabunge wastaafu, Bi Sophia Simba, Mh, Adam Malima, Mh, Idd Azani, Mh, Vita Kawawa, na viongozi wengine akiwemo,  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), MNEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa , Mbunge, Mariam Kisangi, Naibu Meya wa Kigamboni , Naibu Meya wa Temeke, Meneja wa DDC, Meneja wa Dawasco, Mh, Diwani wa Temeke, Kinondoni, Ilala, Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Omary Matulanga na  Mkuu wa Idara ya Utawala UVCCM Taifa,  Omary Mwanangwalu. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog

Gari maalum lililoandaliwa na familia  lakubeba mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa Hospitali ya Lugalo 
Mtoto wa Marehemu Amina Mtemvu (katikati) akisaidiwa na mama mtemvu kushoto na kulia Hellen Mwilima  baada ya kuutambua mwili wakati walipofika katika Hospitali ya Lugalo kuuchukuwa mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwa taratibu za mazishi
Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu ukiingizwa katika gari maalumu ukitokea Hospitali ya Lugalo kuelekea nyumbani kwa taratibu za mazishi
Mwili wa Marehemu Sitti Mtemvu ukishushwa nyumbani 
Wajukuu wa Marehemu Sitti Mtemvu wakiwa wamebeba picha ya marehemu
Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu ukiwasili nyumbani ukipokelewa na waombolezaji ukitokea Hospitali ya Lugalo ukiingizwa ndani kabla ya kutowa heshima za mwisho
Mchungaji Huduma Neno lililopo Mbagala Mgeninani, Yohana Msumule akiongosa kwa Ibada fupi baada ya mwili kuwasili nyumbani  
Familia ikiwa katika huzuni
Wadogo wa Mtemvu na Mh, Mtemvu wakiwa katika majonzi
Mdogo wa Marehem Hamisi Mtemvu akizungumza jambo na ndugu na familia yake baada ya yeye kutowa heshima za mwishi 




Waombolezaji kwa kushirikiana na familia wakiuandaa mwili kwa kuuweka sehemu maalum ya kuagia 
Sitti Mtemvu (kushoto) akizungumza na mama yake mama Mtemvu





Waombolezaji wakiwa wameubeba Mwili wa marehemu Sitti Mtemvu mara baada ya kukiwazili katika makaburi ya Kinondoni Jijini  Dar es Salaam

Mchungaji Huduma Neno lililopo Mbagala Mgeninani, Yohana Msumule akiongosa kwa Ibada fupi baada ya mwili kuwasili nyumbani  
Waombolezaji
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Temeke, Dk. Amaani  Malima (aliye simama kushoto)
Mchungaji Huduma ya Maombezi Mbezi Beach Dar es Salaam, Atilio Komba, ambaye ni Mjukuu wa Marehemu Moris Nyunyusa (kulia) akitowa mahubilr katika makaburi ya Kinondoni kabla ya mazishi ya mama wa Mh, Abbas Mtemvu




Amina Mtemvu akitowa heshima za mwisho kwa kuweka udongo katika kabuli la mama yake

Aliyekuwa Mbunge wa Jibo la Temeke Mh, Abbas Mtemvu akitowa heshima za mwisho akiweka udongo katika kaburi la mama yake Juni 2, 2017 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
Mtoto wa marehemu Sitti Mtemvu,  Herry Mtemvu akitowa heshima za mwisho akiweka udongo katika kaburi la mama yake Juni 2, 2017 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam

Mh, Adam Malima  akitowa heshima za mwisho kwa kuweka udongo

 Mariam Mtemvu (kushoto)  akitowa heshima za mwisho kwakuweka udongo

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), MNEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa akitowa heshima za misho

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sharik Choughule (aliyevaa suti nyeusi) akiweka udongo katika kaburi la mama 






Mkuu wa Majeshi Mstaafu Tanzania, Davis Mwamunyange, (kulia) akimpa pole aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu 







Mh, Mtemvu na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la mama yao


Mh, Malima akiweka shada la maua na mkewe  katika kaburi la mama wa Mtemvu


















Na Kamisi Mussa

Sitti Mtemvu ambaye alikuwa Mama  wa aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu amezikwa Juni 2, 2017 katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, ambapo Bi, Sitti Mtemvu  alipata Elimuya yake ya msingi katika Shule ya Jamiatul Islamiya iliyopo Mtaa wa Lumumba na Aggrey wakati huo ukiitwa New street na Stanley street.

 Marehemu, Sitti alifunga ndoa na Hayati Zuberi Mtemvu 
mnamo miaka ya mwanzoni ya 1950, kipindi ambacho wote walijihusisha na shughuli za kisiasa za kudai Uhuru wa Tanganyika, 

Wakati mumewe alikuwa Katibu wa kwanza wa Chama Cha TANU chini ya Hayati Mwalimu  Nyerere, ambapo  marehemu  Sitti  alijishughulisha na kuwahudumia wanasiasa hao wakati wapo kwenye mikutano ya siri iliyokuwa inafanyika nyumbani kwao

 Kipindi hicho harakati za ukombozi zilikuwa zinafanywa kwa siri majumbani, ambapo nyumba ya 
baba yake Marehemu Sitti iliyokuwa wanaishi ilitumika sana.

Harakati hizo ziliwashirikisha wakinamama, Maria 
Nyerere, Sofia Kawawa, Bi Titi Mohamed na wengine, Marehemu pia alijiunga na vijana wengine kwenye mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika huko Arnatoglo Hall ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa vijana wasomi waliojipanga kutawala Nchi yao.

Hapo ndipo chimbuko la  Chama cha TAA na hatimaye TANU ilipoanzishwa , vilevile alijiunga na Elimu ya 
watu wazima na kusoma Lugha ya Kiingereza. Mnamo miaka hiyo marehemu alisafiri mikoa 
mbalimbali kuanza harakati za kudai uhuru dhidi mkoloni,

Marehemu aliwahi kuwa kiongozi wa ngazi 
mbalimbali katika umoja wa wanawake wa Tanganyika wakati huo na hata na baada ya 
Muungano wa Tanzania. marehemu alifanya kazi Tanzania Cigarette Company mnamo miaka ya 1965 na 1973 wakati huo BAT na Bank of Tanzania na kustaafu mwaka 1973.

 Baada ya kustaafu marehemu alijishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku mnamo mwaka 1987 marehemu alihamia nchini Ivory Coast Abidjan na kufanya biashara ya kuendesha mgahawa 
wa chakula kwa kushirikiana na familia yake.

Marehemu alilazimika kurudi nchni baada ya 
machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini humo mnamo mwaka 1990.Marehemu alifariki mnamo Mei 30, 2017usiku kwa maradhi yaliyosababishwa na tatizo la sukarina umuri mkubwa 

mwisho.