HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Sikiliza na udownload nyimbo mpya ya Snura Ft. Christian bella - ZUNGUSHA

MAX RIOBA ADAI AMESHINDWA KUFANYAKAZI NA YOUNG DEE KWA KUWA HANA NIDHAM

Young Dee akiwa na boss wake wa zamani Max


Uongozi wa label ya Millian Dollar Boys ‘MDB’ iliokuwa unamsimamia rapper Young Dee, amedai hawafanyi tena kazi na rapper huyo kwa madai rapper huyo hana nidhamu.


Max Rioba ambaye ni mkurugenzi wa label hiyo, wiki moja iliyopita alionekana kulalamika katika mitandao ya kijamii akidai rapper huyo amerudi tena katika matumizi ya Madawa ya kulevya.
Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha FNL cha EATV, Max amedai habari za rapper kurudia matumizi ya Madawa ya kulevya na yeye anaziona katika mitandao ya kijamii kuhu akikiri kutofanya kazi tena na rapper huyo kwa madai ya kuwa hana nidhamu.
“Kwa sasa Young Dee hayupo tena kwangu,” alisema Max. “Sikumfukuza Young Dee kutoka kwangu, nilimwambia aondoke, kuna tofauti kati ya kumfukuza na kumwambia aondoke, sababu ni nidhamu.,”
Pia Max alidai kama rapper huyo atahitaji msaada wa pesa kutoka kwake ataendelea kumsaidia lakisi sio tena kuwa pamoja kama zamani.
“Young Dee akihitaji msaada wa kifedha nitamsaidia, hata binti aliyezaa naye akikwama kifedha mimi nitamsaidia, simchukii Young Dee,” alisema Max.
Katika hatua nyingine Max amedai kwa sasa hadhani kama atakuwa na nafasi tena ya kupokea msanii yeyote na kumsimamia.

MAPENZI YANGU NA JACQUELINE WOLPER YAPO MOYONI – HARMONIZE

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amekanusha kuachana na mpenzi wake Jacqueline Wolper baada ya hivi karibuni kuzagaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wameachana.

Madai hayo yalichukua sura mpya wiki chache zilizopita baada ya malkia huyo wa filamu kudaiwa kufuta picha za mkali huo wa wimbo Bado katika mtandao wake wa instagram.
Akiongea jana katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Harmonize alidai mapenzi yao yapo moyoni na watu wasichanganywe na issue ya kufuta picha instagram.
“Wolper alifuta tu picha za instagram hakufuta mapenzi yetu yapo moyoni,” alisema Harmonize.
Pia muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Matatizo, alidai suala la malkia huyo kufuta picha instagram ni kawaida kwani anaweza kufuta na kuanza kupost mpya.
Wapenzi hao wamebadili utaratibu wa maisha yao kwani huko nyuma walikuwa wanasafiri na kula bata pamoja.

DARASSA ASHAURIWA NA DAKTARI KUTOFANYA SHOO KWA MUDA BAADA YA KUPATA AJALI.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Darasa  akizungumza na na chombo kimoja cha radio hapa nchini amesema
 "Nipo hospitalini Muhimbili sasa hivi nawashukuru sana madaktari wa hapa wamenipokea vizuri wamenipa huduma nzuri sana, wamenicheki kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya sana sehemu za kichwani nashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu kipo poa kabisa kuna damage ndogo wanaifanyia kazi naendelea na matibabu ila nimeshauriwa kupunguza mizunguko kwa wiki moja ili niweze kupumzika na kutibu hayo maumivu ya kichwa"

MWASITI AFUNGUKA BAADA YA KUPATA MANAGEMENT MPYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msanii wa muziki Mwasiti Almas amesema ndani ya muda mchache toka apate management ya kumsimamia tayari ameshaanza kuona mabadiliko makubwa katika muziki wake.

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Kaa Nao’ hivi karibuni, amedai ameanza kuona mabadiliko katika namna ambavyo nyimbo zake zinasambazwa. “Kesema kweli sasa hivi maisha ya muziki wangu yamebadilika sana kusema kweli ndani ya muda mfupi, tayari naona management yangu inafanya kazi yake ipasavyo.
 Mimi sikuwahi kuwa na management serious kama hii kusema kweli mpaka napangiwa vitu vya kufanya usiende kule fanya hivi hii ni dalili nzuri kwamba wapo serious,”

Pia muimbaji huyo amedai ameamua kuachia audio ya wimbo wake kwanza tofauti na wasanii wengine wanavyofanya ili audio ipate nafasi yake na video ipate nafasi yake.

Picha: Belle 9 azindua video mpya ya wimbo wake wa ‘Give IT TO ME’

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Belle 9 akizungumza na waandishi wa habari
Mastaa wa muziki, filamu pamoja na viongozi wa serikali Jumamosi hii walipamba usiku wa uzinduzi wa video mpya ya Belle 9 ‘Give IT TO ME’.
Tafrija hiyo fupi ambayo iliandaliwa na kampuni ya muimbaji huyo,Vitamin Music Group Limited, iliwakutanisha wadau mbalimbali wa muziki pamoja na waandishi wa habari.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ni mmoja kati ya viongozi wajuu waliohudhuria uzinduzi huo.
Akiongea katika uzinduzi huo, Belle aliishukuru team nzima ya Vitamin Music Group Limited kwa kufanikisha tukio hilo pamoja na wadau mbalimbali ambao walijitokeza usiku huyo kwa ajili ya kumsupport. Angalia picha.

Navy Kenzo wakiwa ndani ya nyumba
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Diwani wa kata ya Mwanga Kigoma, Baba Levo


Millard Ayo akishow love na mdau


Joh Makini akiwa na Mx Carter
Mbunge Ridhiwani Kikwete (kwanza kulia) akiwa na mmoja kati ya wafanyakazi wa Vitamin Music Group Limited (katikati) pamoja na Joh Sambila (kwanza kushoto)




Darassa Apata Ajali Kahama

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Muonekano wa gari alilopata nalo ajali ainaya Toyota Harrier

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye anasumbua na ngoma yake kali ya Muziki, Sharrif  Thabit ‘Darassa’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bullyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zimeeleza kuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Harrier  ambalo dereva hajajulikana, Darassa alikuwa ameambatana na director wake, Hanscana pamoja na producer wake, Abba Process na wote wametoka salama.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa amethibitisha kupata ajali hiyo na alipopigiwa simu na na mtandao huu alisema hawezi kuongea kwa sasa hivyo atafutwe baadaye.

SAIDA KAROLI ADAI KUACHANA NA MENEJA WAKE KULIMFANYA APOTEZE MWELEKEO KWENYE MUZIKI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amefunguka kwa kusema kuwa moja ya sababu ambayo ilimfanya apotee kwenye muziki ni kitendo cha kuachana na meneja wake.
Muimbaji huyo ambaye aliachana na meneja wake toka 2007, amedai kitendo hicho kilimfanya ashindwe kujisimamia na kumfanya ashuke kwenye muziki.

“Baada ya kuachana na meneja wangu sikuweza kujisimamia mimi mwenyewe na pia kwa wakati ule ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu muziki una mambo mengi na mimi nimekulia kijijini kwahiyo kujua baadhi ya vitu ilikuwa ngumu sana,” Saida aliiambia BBC.

“Sina nilipo kosea lakini najua kila kitu chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, simaanishi huo ndo mwisho wangu ila kwa kuwa nilianza na mtu, sasa unapomalizana naye ni kama unaanza maisha mapya ndio kitu kilicho nitokea mimi,” aliongeza.
Pia muimbaji huyo amesema kwa sasa anajipanga kuja kwa kishindo na kufanya mapinduzi katika muziki wa asili nchini.