Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Muonekano wa gari alilopata nalo ajali ainaya Toyota Harrier
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye anasumbua na ngoma yake kali ya Muziki, Sharrif Thabit ‘Darassa’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bullyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zimeeleza kuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Harrier ambalo dereva hajajulikana, Darassa alikuwa ameambatana na director wake, Hanscana pamoja na producer wake, Abba Process na wote wametoka salama.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa amethibitisha kupata ajali hiyo na alipopigiwa simu na na mtandao huu alisema hawezi kuongea kwa sasa hivyo atafutwe baadaye.
No comments:
Post a Comment