HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

WAZIRI NCHEMBA AOMBA RADHI SAKATA LA WALEMAVU KUPIGWA

Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba leo bungeni amefunguka na kuomba radhi dhidi ya vitendo vya jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye ulemavu.

Mwigulu Nchemba amekiri kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kwa watu hao na kusema serikali wamepokea jambo hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili siku nyingine lisijirudie.

"Kwanza naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa, ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie" alisema Mwigulu Nchemba

Mnamo tarehe 16, Juni, 2017 jijini Dar es Salaam jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa ikiwepo kuwapiga na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu ambao walikuwa wamejikusanya katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuwasilisha malalamiko dhidi ya askari wa usalama wa barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katika jiji. Lakini pia walikuwa wakipigania haki yao ya kuwa na maeneo ya kuegesha vifaa vyao katikati ya jiji.

Waziri Nchemba Ataja Sababu Zinazowafanya CHADEMA Wapigwe Marufuku Kufanya Sherehe Vyuoni

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alihoji bungeni sababu za wanafunzi wa CCM kupendelewa kufanya mikutano na sherehe za kumaliza masomo yao huku wanafunzi wa vyama vingine vya upinzani hasa CHADEMA kupigwa marufuku kufanya sherehe hizo.

Akijibu jambo hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema kuwa wanafunzi wa Chama Cha Mapinduzi huwa wanafuata utaratibu ndiyo maana huwa wanapewa ruksa kufanya sherehe hizo pindi wanapomaliza vyuo na kusema hao wengine huwa hawafuati utaratibu ndiyo maana wanakuwa wanazuiliwa.

"Taratibu ziko wazi kama CCM walikuwa wamefuata utaratibu na kupewa mikutano, chama kingine chochote kinachotakiwa ni kufuata utaratibu zile zile waweze kupewa mikutano lakini wengine kama hawajafanya utaratibu hawatapewa tu kwa sababu CCM walipewa bali watapewa kwa kufuata utaratibu, kuna sehemu zingine CHASO hao hao wamepewa mikutano kwa hiyo linalotakiwa ni utaratibu tu wa kupewa mikutano hiyo" alisema Mwigulu Nchemba

Mbali na hilo Waziri Mwigulu Nchemba alisema mikutano ya hadhara haijazuiwa bali imewekewa utaratibu na kusema duniani kote sifa za mikutano ya hadhara ni kama ambavyo inafanyika hivi sasa Tanzania na kusema kuwa mtu aliyeshinda ndiye anaendelea na majukumu ya kuongoza na aliyeshindwa hapaswi kushukuru kwa wananchi.

"Marekani mwaka jana walifanya uchaguzi mmemuona Hillary Clinton anashukuru kwa wananchi? Duniani kote aliyeshinda ndiye anaendesha serikali kwa utaratibu wa kiserikali hili liko wazi duniani kote" alisisitiza Mwigulu Nchemba

Mwigulu Nchemba Awataka Chenge, Werema Waeleze Maslahi Yao Mchanga wa Madini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ametaka wanasheria wakuu wa Serikali wastaafu waeleze hadharani maslahi waliyonayo kwenye kampuni za madini zinazosafirisha mchanga nje ya nchi.
Hatua hiyo ya waziri imekuja siku chache baada ya wanasheria wakuu wastaafu waliofanya kazi kwa nyakati tofauti wakati nchi ikiingia kwenye mikataba ya madini ‘kujivua lawama’ kuhusu udanganyifu uliogunduliwa kuhusa sakata la usafirishaji wa mchanga.

Wanasheria hao wakuu wa Serikali wastaafu ni Andrew Chenge na Jaji Frederick  Werema na amewataka wamwache Rais Dk. Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma zisiliwe na watu wachache.

Mwigulu amesema hayo juzi, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Ndago, Jimbo la Iramba.

Alisema Chenge na Werema kwa nyakati tofauti wakiwa wanasheria wakuu wa serikali, pamoja na majukumu yao mengine, wameshiriki kusaini  mikataba mikubwa mikubwa, ikiwamo ya makampuni ya kuchimba madini.

“Kwa akili ya kawaida tu, baadhi ya mikataba mikubwa, ikiwamo ya makampuni ya madini, haikuwa sawa… ndiyo maana imelalamikiwa kwa muda mrefu.” alifafanua Mwigulu, Mbunge wa Jimbo la Iramba.

Alisema juzi juzi magazeti yameeleza kuwa akina Chenge na Werema wamedai kuwa Rais wetu Magufuli amedanganywa na tume maalumu ya Profesa Mruma.

 “Wao ndio waliosaini mikataba ambayo imechangia Taifa kupoteza mabilioni ya fedha kupitia usafirishaji wa michanga nje ya nchi. Sasa wamegeuka na kuwa upande wa pili wa watu waliosaini pamoja mikataba hiyo mibovu. Nawashauri watoke hadharani…. waeleze wana maslahi gani na kampuni wanazozitetea,” alifafanua zaidi.

Aidha, Mwigulu amesema Chenge na Werema wakishindwa kuweka wazi maslahi waliyonayo, basi ni vema wakakaa kimya na kumwacha Rais wa vitendo aendelee kuinyoosha nchi.

“Hivi ukimpa mtu kazi ya kuuza duka, halafu kila siku awe anakuambia hajauza kitu na huku akilalamika kuwa kila siku anapata hasara. Unamshauri aachane na biashara inayompatia hasara, haachi…anaendelea kuwepo tu, utamwalewaje. Si atakuwa si mkweli, mwongo ananufaika na hilo duka,” alisema.

Akiijengea nguvu hoja yake, alisema Chenge na Werema wanaishi Masaki, jijini Dar es Salaam, hawa hawawezi au watakuwa wamesahau maisha ya Watanzania wengi maskini waliopo vijijini. Hivyo wamwache Rais Magufuli ambaye ameonyesha uzalendo wa kweli, aendelee kulinda rasilimali za umma.

 Alisema kwa wao wanaomfahamu Rais Magufuli, kwa hili la kuchokonoa kwenye madini na kubaini upotevu mkubwa wa fedha za umma, ni mwanzo tu, kazi bado ipo mbele ya kuchokonoa zaidi ubadhirifu na wizi wa mali ya umma katika sehemu mbalimbali.

 Mwigulu ametumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania wazalendo wa madhehebu ya dini mbalimbali waendelee kumwomba Mungu ampe Rais Magufuli afya njema na ujasiri wa kuziba mwinya yote inayotia hasara Taifa letu.

VIDEO: Kauli ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu mauaji ya Viongozi wa Serikali Kibiti

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe.Mwigulu Nchemba amewaonya wananchi wa Kibiti mkoa wa Pwani kutowaficha wahalifu wanaofanya mauaji mkoani humo bali wawafichue ila maisha yaweze kuendelea kama zamani na kudai pasipo kufanya hivyo kuna gharama.

Mhe. Mwigulu amewataka wananchi kutambua kwamba kuendelea kuwaficha wahalifu waliopo ndani ya jamii watambue kuna gharama kubwa ambayo itawafanya maisha yasiweze kusonga mbele.

Mwigulu ameyasema hayo jana Kata ya Bungu wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani mara baada yakutembelea majeruhi na kambi maalum ya jeshi la Polisi mkoani humo kwa ajili ya kupambana na waalifu ambao wanajihusisha na kuua wananchi ,viongozi wa dini na vyama.

Wakati akizungumza na wananchi pamoja na kikosi maalumu kilichopo huko, Mhe. Mwigulu amesema kwamba serikali imejipanga vyema kubana mianya ya wote wanaofanya mauaji hayo na kuongeza kwamba itawatia nguvuni, na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu hao

Nchemba ameendelea kufunguka kwamba  uhalifu unaoendelea kwa sasa maeneo hayo ya Kibiti yanasababisha wasiwasi kwa wananchi na kuongeza kuwa serikali haitawaacha wahalifu  waendelee kufanya mauaji hayo na kuongeza kwamba hakuna ruhusa ya aina yeyote ya mtu kumuua mwenzake kwa misingi yakua na mtazamo tofauti wa dini, chama , kabila na asili.

Pamoja na hayo ameongeza kwamba serikali imeanza kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo na bado wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahalifu wengine.

==>Msikilize hapo chini akiongea

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA 2017/2018


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kushoto ni Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na makamanda wa Jeshi la Polisi muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge la Bajeti ambapo wizara yake iliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akifurahia na baadhi ya wabunge mara baada ya kumaliza kuwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAZIRI MWIGULU AWATAKA WASAIDIZI WAKE KUSIMAMIA HAKI ZA WAFANYAKAZI, PAMOJA NA KUONDOA URASIMU,

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto) na Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara yake kabla ya kufungua Kikao Baraza hilo kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka Wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akizungumza katika Kikao kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018 cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara yake (hawapo pichani) kabla ya kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za Wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto), Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka  wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo, mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahaitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto), Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Waziri Nchemba Atoa ONYO Kwa Wanaotumia Dini Kufanya Uhalifu

Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mwigulu Nchemba, amewaonya waumini wa dini mbalimbali nchini kutotumia mwamvuli wa dini kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo kudhuru maisha ya wengine, huku akitangaza kulegeza masharti ya usajili wa nyumba za ibada

Waziri Mwigulu ametoa onyo hilo jana  alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka lililofanyika  katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo alisema serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo.

Katika hotuba yake fupi Waziri Mwigulu alisema serikali inatambua uhuru wa kuabudu iliyoutoa kwa wananchi wake na inaunga mkono kazi nzuri inayofanyika kupitia ibada, lakini uhuru huo usikwaze wengine, na wala usivunje sheria.

Alisema "Ucha Mungu Siyo Udini", hivyo ni sahihi kwa waumini kumcha Mungu kwa kiwango wanachopenda lakini si kuwashikia silaha watu wengine ili wajiunge na dini zao.

“Wale ambao watatumia misimamo iliyopitiliza kudhuru maisha ya watu wengine, serikali itasimama na kuwahesabia kuwa ni waovu na tutashughulika nao kama wahalifu wengine” Alisema Mwigulu

Katika hatua nyingine, Waziri Nchemba ameagiza taasisi zilizo chini ya wizara yake kulegeza masharti ya usajili wa nyumba za ibada, badala ya kuwapa njia ngumu kwani nyumba hizo ni muhimu kwa ajili ya kumuombea Rais Magufuli na taifa kwa ujumla

"Nimeelekeza watu wangu kuwa waelekezeni watu wanaotaka kusajili nyumba za ibada watimize masharti na muwasajili, hatuwezi kuweka masharti magumu ya kusajili nyumba za ibada halafu tukaweka masharti rahisi ya kusajili bar na kumbi za disco" Alisisitiza Mwigulu

Aliwataka waumini wa dini mbalimbali kuendelea kuliombea taifa, huku akiwapongeza kwa kazi nzuri ya maombi waliyoifanya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

"Endeleeni kuliombea taifa letu, wana maombi mkishaomba, mambo yakawa mema, watu huwa hawakumbuki kama mlisugua magoti… hata wakati wa uchaguzi mliomba ndiyo maana tukapita salama wakati kuna watu walitaka kuona Tanzania inayojidai kuwa na amani, itakuwaje.....

"..Wakati ule walikuwa wameandaa magari ya washawasha na mabomu ya machozi lakini nilipofika wizarani nilikuta yale magari yapo hayakutumika pamoja na mabomu, kazi mlishamaliza wana maombi"

Waziri Mwigulu pia alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wasanii wa nyimbo za injili kuwa serikali itafanya kila iwezalo kulinda maslahi ya kazi zao, huku akipongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli ya kuwaletea maendeleo wananchi licha ya kupingwa na baadhi ya watu na kutolea mifano ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege, elimu bure  na mengine.

MIILI YA ASKARI NANE WALIOUAWA NA MAJAMBAZI MKOANI PWANI YAAGWA RASMI,WAZIRI MWIGULU ATANGAZA KIAMA KWA WATUHUMIWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa heshima za mwisho Dar es Salaam mbele ya majeneza yenye miili ya askari nane waliouawa na majambazi Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani juzi jioni.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Masauni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa pole kwa wafiwa.
Ndugu,jamaa na marafiki wa wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya wapendwa wao.
Maofisa wa Uhamiaji wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Wananchi wakiwa katika shughuli hiyo ya uagaji wa miili hiyo.
Maofisa wa Polisi wakishiriki kuaga miili ya wenzao hao.
Foleni ya kuaga miili hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu wakati wa kuaga miili hiyo.
Mmoja wa ndugu za askari hao akilia kwa uchungu.






Ni kilio kwa kuwapoteza wapendwa wao.
Ni huzuni.


Na Dotto Mwaibale 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga mkoani 
Pwani.

Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam Mwigulu alisema watu hao watakamatwa  wote na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

"Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata" alisema Mwigulu.

Aliwaomba wananchi wa maeneo husika kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwapata wahusika wa tukio hilo.

Katika hatua nyingine Mwigulu ameitaka wizara husika kuhakikisha inatoa fidia kwa ndugu wa askari hao na majeruhi badala ya kuchukua muda mrefu kuitoa.

"Naomba fidia kwa askari hawa tuliowapoteza wakitumikia taifa itolewa haraka bila kucheleweshwa" aliongeza Mwigulu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu alisema watuhumiwa wote waliohusika kufanya mauaji hayo ni lazima watafikiwa na mkono wa dola.

Alisema wananchi wa eneo hilo wanawafahamu wahusika hivyo amewaomba washirikiane na polisi ili kuwapata vinginevyo nguvu itatumika.

Alisema linapotokea tukio kama hilo kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishabikia kupitia mitandao ya kijamii hivyo akatoa onyo kuwa watakao bainika na wao watakamatwa kwa kutenda kosa.

Askari waliopoteza maisha katika tukio hilo la kinyama wametajwa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub


WAZIRI NCHEMBA AWASILI ENEO YALIPOTOKEA MAUAJI YA POLISI WANANE

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewasili eneo yalipotokea mauaji ya askari wanane katika kijiji cha Jaribu, Wilayani Kibiti.
Waziri Nchemba ameambatana na naibu wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.
Nchemba atatembelea kambi za askari polisi wa kanda ya Pwani na katika kata ya Bungu wilayani Kibiti.

RIDHIWANI KIKWETE AUSHANGAA UKIMYA WA MWIGULU NCHEMBA

Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete anamshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuendelea kukaa kimya juu ya matatizo ya kiusalama kwa wananchi yanayoendelea nchini wakati yeye ndio kiongozi mwenye dhamana ya kulitatua hilo.

Akiongea bungeni Jumanne hii, mbunge huyo amesema, “Kumekuwa na malalamiko mengi sana, tumeshuhudia malalamiko mengine yanahitaji majawabu kama siyo majibu ya haraka ili kuondoa hizi sintofahamu walizonazo wananchi.”
“Niwaombe sana hakuna sababu ya mtu kama Mhe. Waziri Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanalalamika juu ya hali yakiusalama katika maisha yao,” ameongeza.
“Mimi binafsi niishauri serikali yangu kwamba unapojibu jambo lolote lile unatoa hali ya wasiwasi,” amesisitiza.

Maagizo Aliyoyatoa Waziri Nchemba Kwa Polisi Kuhusu Kutekwa kwa Msanii Roma

Msanii wa hip hop Roma Mkatolikia alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.

Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.

“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”

Maagizo Aliyoyatoa Waziri Nchemba Kwa Polisi Kuhusu Kutekwa kwa Msanii Roma

Msanii wa hip hop Roma Mkatolikia alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records  na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa  kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.

Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.

“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”

WAZIRI MWIGULU AWAASA ASKARI KUTOWABAMBIKIZIA WATU KESI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi.
Mzee John Samwel Malecela akizungumza wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu Akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
 Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi.
SACP Ramadhani Mungi Msimamizi wa bandari Tanzania na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renata Mzinga wakifatilia kwa makini kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi.

Na Mathias Canal, Dodoma
Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.
Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Amesisitiza pia Askari na Maafisa wa Polisi kutotumia taarifa za watu wanaohasiana kuwa ndio chanzo pekee cha msingi wa shtaka badala yake kufanya uchunguzi kwa kina na kujiridhisha vyema ili kufikia hukumu yenye tija Na haki kwa mtuhumiwa kwani kufanya hivyo kutaimarisha amani na jeshi la Polisi kupata taarifa nyingi za uhalifu kutoka kwa wananchi endapo watajikita katika haki.
Akizungumzia Vita dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe Nchemba alisema kuwa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukamata na kuziteketeza Dawa za kulevya zilizopo mashambani ambapo ametilia msisitizo zaidi kwa Askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi kuendelea kupambana ili kuzikamata Dawa za kulevya zilizopo katika viwanda.
Amesisitiza pia Jeshi la Polisi kuendelea kupambana na kubaini uhalifu sambamba na kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha lengo mahususi la serikali ambalo ni kuzuia uhalifu linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Mhe Mwigulu amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka 2017 inayosema "ZINGATIA MAADILI TUNAPOPAMBANA NA UADILIFU ILI KUIMARISHA USALAMA KWA MAENDELEO YA TAIFA" endapo kama itatekelezwa kwa vitendo itaijenga nchi na kuzidi kudumisha zaidi amani iliyopo kwa wananchi.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu alisema kuwa kikao hicho cha kazi kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kina dhamira kubwa ya kufanya Tathmini ya utendaji wa mwaka 2016 na kuandaa mikakati mizuri ya mwaka 2017 na kupata fursa ya kubadilika kiutendaji kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Hata hivyo amesisitiza zaidi askari wote nchini kutofanya kazi kwa mazoea, Kuacha Urasimu na kujenga uaminifu na weledi katika kazi.
Mangu amesema matendo ya Askari Polisi nchini yanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii hivyo askari Polisi hapaswi kuwa chanzo cha vurugu au kujihusisha na matendo ovu yasiyostahili katika jamii.
Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaombele kwa kujadiliwa katika Kikao hicho itakuwa ni pamoja na Vita dhidi ya Dawa za Kulevya, Vita dhidi ya Magendo, Vita dhidi ya ujangili na Uvuvi sambamba na Vita dhidi ya Ubambikizaji wa kesi kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha Waziri Mwigulu Nchemba kuzungumza na askari hao amelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi kubwa linayofanya ambapo pia ameeleza mpango wa Mkoa katika kupambana na migogoro ya ardhi kwa kuanzisha kamati maalumu ya wataalamu wa sheria kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Kupitia na kushauri ili kuweza kumaliza haraka migogoro hiyo.
Naye Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela alisema kuwa jambo la msingi ambalo askari Polisi wanapaswa kulifanya ni pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata Uhuru wake na kama jambo hilo likitekelezwa ipasavyo Fikra za Hayati Mwalimu J.K Nyerere zitakuwa zimeenziwa kwa weledi.